Naiona Yanga yangu ikibomoka vipande vipande baada ya mechi na Rivers Utd

buhoro ksl

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2019
Posts
248
Reaction score
246
Chonde chonde viongozi wangu hasa GSM itilieni mkazo mechi hii na msipoanglia kwa umakini inaweza ikawa chanzo cha nyie kuondoka Yanga.

Atleast yanga hiii inatakiwa kufika group stage caf champions leage.
 
Utopolo Akili Zao wanazijua Wenyewe. Hawatalaumu GSM kwa Kusajili ndombolo ya Solo....! Hapo mchawi atakuwa TFF Watasahau hata kupata hiyo Nafasi 'WAMEBEBWA' na Simba..!
GSM analitaka soko la DRC kwa biashara zake, alichofanya ni kutafuta kujulikana huko kwa mbinu ya kusajili Wacongo kibaaaaaao kwa interest zake kibiashara na si kwa mapenzi au matakwa ya Benchi la ufundi.

Tusubiri muda utaongea tu wacongo watakapokuwa wakishindia Salooon kujiremba na kupakaza pikko msije kumlaumu Karia na TFF
 
Chonde chonde viongozi wangu hasa gsm itilieni mkazo mechi hii...na msipoanglia kwa umakini inaweza ikawa chanzo cha nyie kuondoka yanga.....atleast yanga hiii inatakiwa kufika group stage caf champions leage
Kama kweli wewe ni shabiki wa Yanga, basi utakua umetudhalilisha sana mashabiki wenzako! Kwa huu mtazamo wako, ulistahili kabisa kuwa shabiki wa mbumbumbu fc!

Siku zote mpira una matokeo 3! Sare, kushinda na kufungwa! Hata mbumbumbu mwaka juzi walitolewa hatua ya awali tu na Vibonde UD Songo, huku wakiwa wamefika hatua ya robo fainali msimu uliopita. Huo ndiyo mpira.

Hujaiona hata timu ikicheza, wewe tayari hofu mwili mzima! Wewe vipi bhana!! Unadhani hii ni Yanga ya akina Waziri Juinior Shentembo!! Au striker hatari Sarpong!!! Hii ni Yanga nyingine kabisa! Na itapita hata hiyo hatua ya makundi kwa kishindo.
 
Komaeni wajomba nini mechi ya kwa Mkapa ndo inabeba matumaini yenu ila mkibaki na zile stori zenu za tuna watu ndo mtajua kuwa hata Nigeria uswahili wanaujua vizuri
 
Kama kweli wewe ni shabiki wa Yanga, basi utakua umetudhalilisha sana mashabiki wenzako! Kwa huu mtazamo wako, ulistahili kabisa kuwa shabiki wa mbumbumbu fc!...
Naona mnamshambulia sana mleta mada lakini alichokiongea kinaweza kutokea kwa mashabiki wa Yanga. Yanga inapaswa kuwekeza akili kwenye mechi dhidi ya Rivers Utd lakini mpaka sasa hawajacheza mchezo wowote ule wa kirafiki ili kuona palipo na mapungufu.

Wako bize kujiandaa na wiki ya mwananchi ambayo kimsingi wakifikia kilele hiyo wiki ya mwananchi watabakiza siku chache sana kukabiliana na Rivers United. Wakitolea itawafanya Yanga kuendelea kuishi kinyonge mbele ya watani zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…