Naipataje Bajaj yangu iliyoibiwa

Naipataje Bajaj yangu iliyoibiwa

iamriq_arthur

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2021
Posts
440
Reaction score
1,086
Kuna mtu nlimpa Bajaj ya mzigo kwa mkataba na amekimbia nayo hajulikani alipo, nikipiga simu hapokei na muda mwingne haipatikani kabisa. Ntaweze kumpata mtu huyu?

Mzamini wake ni mama yake mzazi, je mnanishauri nichukue hatua gani ili niweze kuipata bajaj yangu?
 
Aisee pole sana ungefunga GPS mkuu tuko enzi za kidigitali...Enewei pakuanzia hakikisha unampata mshikaji wake wa karibu kabisaaa huyo ukimbana vizuri kwa pesa au kibano atakueleza A-Z ndivyo wanaintelijensia hufanya.
 
Sasa utampigaje rafiki ake wa karibu kama vile yeye ndie aliehusika..?
Sio wewe ndo upige..polisi ndio hufanya hivyo..lakini hata watu mafia hufanya nimekupa mfano tu wa pa kuanzia na sio lazima utumie nguvu unatumia akili thats y nimekwambia unaweza tumia njia kama Pesa kumshawishi akwambie alipo
 
Aisee pole sana ungefunga GPS mkuu tuko enzi za kidigitali...Enewei pakuanzia hakikisha unampata mshikaji wake wa karibu kabisaaa huyo ukimbana vizuri kwa pesa au kibano atakueleza A-Z ndivyo wanaintelijensia hufanya.
Kenge kweli,violence kwa rafiki yake ya nini,anahusika vipi kwenye mkataba wenu
 
Kama ana mke,mchukue mke wake,faster tu atajitokeza,wahindi ndio zao uko India,atahakikisha anampata mke wako ,ili umlipe kwa haraka,ama urudishe chake
 
Kenge kweli,violence kwa rafiki yake ya nini,anahusika vipi kwenye mkataba wenu
Ivi wewe bata unajua hata chochote kuhusu upelelezi?Unajua ukitoka nyumbani ukapotea nani ataulizwa wa kwanza kama sio rafiki wako wa karibu?Unajua rafiki wa mwizi ni mwizi?? Unajua kwenye upelelezi wanabanwa marafiki kabla ya mhusika? Ficha ujinga wako sawa?
 
Kama ana mke,mchukue mke wake,faster tu atajitokeza,wahindi ndio zao uko India,atahakikisha anampata mke wako ,ili umlipe kwa haraka,ama urudishe chake
Mdhamini sio mkewe, unatafuta kumtia kwenye kesi nyingine amekwambia mdhamini ni mama yake, akimtia ndani atataja mwanae alipo au mwanae akisikia mama yake katiwa ndani atageuza na kurudisha Bajaj ya watu

Unaijua kazi ya mdhamini?
 
Back
Top Bottom