Naipenda sana Yanga, lakini South Mhm!!

Naipenda sana Yanga, lakini South Mhm!!

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
2,977
Reaction score
3,798
Ukweli ni kwamba,marumo japo inakaribia kushuka daraja lakini uwezo wa wachezaji wake ni mkubwa kuliko timu yangu ya yanga na sijui tutafanyaje kuwazuia wasitufunge.tutatolewa tu
 
Wao Marumo wabaki na uzuri walionao ila Yanga inakwenda kupata matokeo na kuvuka kuingia fainali.
Swala la wao kuwa wazuri kuliko Yanga lisikusumbue.
Yanga inacheza kibingwa.
Nafurahi maneno yako ya kunitia moyo
 
Ukweli ni kwamba,marumo japo inakaribia kushuka daraja lakini uwezo wa wachezaji wake ni mkubwa kuliko timu yangu ya yanga na sijui tutafanyaje kuwazuia wasitufunge.tutatolewa tu
Yaani chini umemalizia kwa unachokipenda kitokee. Eti Yanga tutatolewa tu. Endelea hivyo hivyo kuombea Yanga itoke.
Jamaa ni wazuri kweli, wana wachezaji wazuri, na wana kasi sana ila Yanga hakupata magoli mawili kwa bahati bali kwa kucheza mpira wa kutafuta matokeo. Hivyo pamoja na hao jamaa kuwa wazuri wanatakiwa watafute magoli mawili ya kusawazisha kwanza huku wasiruhusu goli. Kimahesabu Yanga yupo mguu mmoja ndani kuelekea fainali ila kimpira bado hadi 90 za mwisho. Lakini nimeshaangaa tu aliyekuwa na advantage ndio umemkatia tamaa, ni wazi moyo wako utafurahia endapo Yanga atatolewa.
 
Kimahesabu ni ngumu lakini mimi nimeangalia historia ya michezo yao yote aisee hawa jamaa ni hatari hushambulia kama nyuki wakiwa nyumbani kwao na sijawahi kuona mechi yoyote ambayo yanga ilishambuliwa sana na wakayahimili mashambulizi hayo. Na mara mpira wa dar ulipoisha marumo walianza hapo hapo kuwatisha yanga kwamba mtakuja kwetu na mtatutambua,hiyo ndio hofu yangu vinginevyo hata wakitolewa sina la kuwadai yanga
 
Mkuu mpira ni mbinu na sio kukimbia kimbia uwanjani. Unadhani Marumo Gallants wamefungwa Dar kwa kupenda? Mechi ya Pyramids kule Misri walitoka sare na Pyramids ndio waliosawazisha. Mechi iliyofuata kule South Marumo wamepata goli moja pekee dhidi ya Pyramids. Cha kwanza unaona mzani uliopo kwao wa Yanga ni kama Yanga imewaacha kwa upande wa ubora. Yanga wana kazi ndogo sana kufuzu kuliko wao wanaodaiwa nagoli mawili. La pili Yanga huwa wanacheza vizuri sana away kuliko nyumbani. Mechi ya Al Hilal yanga pamoja na kufungwa goli moja lakini alitawala mchezo, mechi ya club African ndio kabisa Yanga akawatolea huko huko kwao, mechi dhidi ya Monastir Yanga ilitawala mchezo wakafanyika uzembe kwenye set pieces Tp Mazembe, Real Bamako na Rivers wote hawa wameshindwa kumfunga Yanga wakiwa makwao.

Approach nzuri ya Yanga + utulivu ndio itakayoamua mechi, lakini sio mechi rahisi hivyo unavyochukulia wewe kwa hao Gallants, wangeanza kumpiga nyingi Pyramids
 
Kama Yanga ingekuwa inacheza
kwa kuhofia hisoria, basi mpaka muda huu ingekuwa imefungws na Tp Mazembe, Rivers United, As Monastir ya Tunisia, nk

Yanga inacheza kwa malengo. Na jambo hili unatakiwa kulitambua kuanzia sasa.
 
Ukweli ni kwamba,marumo japo inakaribia kushuka daraja lakini uwezo wa wachezaji wake ni mkubwa kuliko timu yangu ya yanga na sijui tutafanyaje kuwazuia wasitufunge.tutatolewa tu
Mbona tuliwafunga, ilikuwaje?
Au waliingiza team B?
Tutasonga mbele usijali
 
Mkuu mpira ni mbinu na sio kukimbia kimbia uwanjani. Unadhani Marumo Gallants wamefungwa Dar kwa kupenda? Mechi ya Pyramids kule Misri walitoka sare na Pyramids ndio waliosawazisha. Mechi iliyofuata kule South Marumo wamepata goli moja pekee dhidi ya Pyramids. Cha kwanza unaona mzani uliopo kwao wa Yanga ni kama Yanga imewaacha kwa upande wa ubora. Yanga wana kazi ndogo sana kufuzu kuliko wao wanaodaiwa nagoli mawili. La pili Yanga huwa wanacheza vizuri sana away kuliko nyumbani. Mechi ya Al Hilal yanga pamoja na kufungwa goli moja lakini alitawala mchezo, mechi ya club African ndio kabisa Yanga akawatolea huko huko kwao, mechi dhidi ya Monastir Yanga ilitawala mchezo wakafanyika uzembe kwenye set pieces Tp Mazembe, Real Bamako na Rivers wote hawa wameshindwa kumfunga Yanga wakiwa makwao.

Approach nzuri ya Yanga + utulivu ndio itakayoamua mechi, lakini sio mechi rahisi hivyo unavyochukulia wewe kwa hao Gallants, wangeanza kumpiga nyingi Pyramids
Maoni ya kutia moyo ntafurahi mno tukishinda au kutoka sare ili tufuzu
 
Back
Top Bottom