Naipenda sana Yanga!

Mkuu huna haja ya kutokwa mapovu rudi kwenye mada
Si swala la povu mkuu. Ni swala la uhalisia kwamba mchezaji yeyote anapojiunga na timu yoyote jambo la kwanza kwake ni maslahi - hata akikataa namna gani. Mapenzi na timu anayoenda yanafuata. Inawezekana mchezaji akaenda timu ambayo awali ilikuwa ni hasimu wake mkubwa, lakini maslahi yakambadilisha akachezea timu hiyohiyo pinzani. Angalia Louis Figo alivyocheza akiwa Barcelona. Nani angethubutu hata kudhani kwamba iko siku angeenda Real Madrid angalau kama mtazamaji tu? Mwangalie alivyoenda Real Madrid. Nani alimtilia shaka kwamba angali na mapenzi na Barcelona? Madhali tumeingia kwenye mtindo wa kusajili wachezaji kwa hela (badala ya ushabiki kama ilivyokuwa enzi za Gossage), huu tunaoudhani kuwa ni usaliti ni jambo tunalopaswa kulizowea: Ajib atatua Yanga, Niyonzima atakwenda Simba, Mrisho Ngasa ameshakwenda Azam na Simba, Louis Figo ameshaenda Real Madrid, Matic ameenda Man U, Neymar ameshaenda PSG.........n.k. Zama za 'nani kaua!' huku wachezaji wakistaafu na ufukara zinatoweka kwa kasi. Nasi wapenzi, washabiki, viongozi na wadau wa vilabu lazima tubadilishe mitizamo yetu kuelekea zama hizi za maslahi (halali) kwanza. Si swala la povu mkuu.
 
Mimi niliona Mpira wa TZ hauwezi kukua pale tu Yanga walipomtoa Hans na kumleta huyu wa sasa cz sijajua hadi Leo sababu za kumtoa yule mzee na kumleta huyu wa sasa ambaye nae ameonekana hana jipya. Inakatisha sana tamaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu kubwa ni tamaa ya kumfunga mwarabu hasa Al Ahly tu basi maana walisikia huyu jamaa huwa anawafunga sana warabu
 
Una Akili sana wewe

Today is weekend, agiza kinywaji chochote nitagharamia.

Kuwapenda wale waswahili wa kashata ni kukengeuka.


Yanga Hoyeeee......
 
Basi nimekuelewa ndugu,kwa hyo Lwandamina ndio dawa ya kuwafunga waarabu eti!? Basi tusubiri waarabu waje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndivyo walivyokuwa wanajiaminisha.

Yanga kipindi kile ilikuwa walikutana na waarabu ilikuwa either atoke sare au wafungwe sasa viongozi ndipo walipopata tamaa ya kumchukua huyo manjino kwa kuwa rekodi yake imaonesha timu nyingi anazozifundisha huwa zinamfunga mwarabu.
 
Nyie pigeni kelele ila mjiandae kisaikolojia mapema maana zisipojirudia tano au zaidi sijui, kama nawaona na kandambili zenu mkienda kupiga mbizi kwenye swimming pool ya kaunda, mnyama unyamani lazima mpakatwe. This is Simbaaa (in Manara's voice)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya kweli maneno ya Kike kawaandikia wanawake wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…