Uchaguzi 2020 Naipongeza NEC kwa utaratibu mzuri wa zoezi la kupiga kura leo

Uchaguzi 2020 Naipongeza NEC kwa utaratibu mzuri wa zoezi la kupiga kura leo

Securelens

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
316
Reaction score
541
Kwa mjibu wa taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo ITV, AZAM, CHANNEL 10, TBC na Online TVs karibu kila kona ya Tanzania zoezi la upigaji kura limeenda vizuri na kasoro nyingi zilizozoeleka kufanyika mwaka huu hazikuonekana na upigaji kura ulifanyika kwa amani na utulivu.

Nawapongeza NEC kwa hatua hii, kamilisheni hatua zilizosalia pia kwa uweledi. Nawaomba watanzania tupuuze madai machache yanayodai kupigwa kwa kura feki.

Kwa utaratibu wa kura za mwaka huu kila kura inayopigwa lazima serial number yake irekodiwe mbele ya mawakala wote. Hivyo hakuna namna kura feki inaweza kupigwa na isionekane wakati wa kulinganisha kura zilizopigwa na zile zenye serial numba zilizorekodiwa. Hivyo tuzipuuze.
 
Mkuu nilibahatika kuwa msimamizi wa kituo ,hivyo ni kweli kabsa haya wanayo ripoti ni kweli na amani imetawala kwa kweli,

Hakika hakuna hujuma wala visingizio kama miaka ya awali.

Hakika kwa hatua hii wilson mahera awe mkurugenzi wa kudumu!!

#jr
 
sijaona cha kuwapongeza maana tangu mwanzo walionekana ni CCM "B"

na pia ni nini maana ya kuzima mitandao kama hakuna kura feki na uchaguzi ni wa huru na haki.
kauli yao ya kuwa wasiamini habari za mitandaoni ni wazi kuwa kuzima mitandao ni kuzima kusambaa kwa habari za kura feki.
 
Sio kila mahali

Nilipokua mie mwananyamala huku kwa kopa karatasi nimepewa zimekunjwa zimeshachanwa kwenye kitabu

Za kuanzia diwani.mpka rais
Mie nilikua nakunjua natiki nakunja kama walivokua wamekunja
 
Kwa mjibu wa taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo ITV, AZAM, CHANNEL 10, TBC na Online TVs karibu kila kona ya Tanzania zoezi la upigaji kura limeenda vizuri na kasoro nyingi zilizozoeleka kufanyika mwaka huu hazikuonekana na upigaji kura ulifanyika kwa amani na utulivu...
Ngoja waje kutoka kwenye 'kulinda kura' ndo utayaoga matusi yao, ukijumulisha na hasira za kushindwa ndo basi kabisa.
 
mkuu nilibahatika kuwa msimamizi wa kituo ,hivyo ni kweli kabsa haya wanayo ripoti ni kweli na amani imetawala kwa kweli,

Hakika hakuna hujuma wala visingizio kama miaka ya awali,
Hakika kwa hatua hii wilson mahera awe mkurugenzi wa kudumu!!

#jr
Naona mmetumwa.
 
Naunga mkono hoja, uchaguzi huu umeendeshwa vizuri sana, ilikuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Atakashinda, ameshinda kwa haki na halali na aliyeshindwa, ameshindwa kwa haki. Mshindwa ampongeze mshindi, maisha yaendelee.
P
Nitumie buku basi nikale
 
Hahahaaaa...
Kwa mjibu wa taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo ITV, AZAM, CHANNEL 10, TBC na Online TVs karibu kila kona ya Tanzania zoezi la upigaji kura limeenda vizuri na kasoro nyingi zilizozoeleka kufanyika mwaka huu hazikuonekana na upigaji kura ulifanyika kwa amani na utulivu...
 
Jina sibadili na harakati zinaendelea mpaka Africa ijikomboe kiuchumi
ndoto za usiku kama tulishindwa kusimama pamoja na gadaffi unafikir kuna mtu mwingine wa kutukomboa.... kabla hujamtaja meko kumbuka kashaomba msaada wa kupambana na corona...
 
ndoto za usiku kama tulishindwa kusimama pamoja na gadaffi unafikir kuna mtu mwingine wa kutukomboa.... kabla hujamtaja meko kumbuka kashaomba msaada wa kupambana na corona...
Ndo hivyo sasa, sisi wenyewe tunapambana mpaka tujikomboe
 
Back
Top Bottom