Pia jamani jana kupitia Citizen saa 3 usiku,kulikuwa na mjadala kuhusu maoni ya kura za maoni kupitia kampuni mbili za utafiti. Pamoja na kuwa hesabu hazikosewi bali watoa takwimu ndio hukosea niliona tofauti kubwa katika matokeo ya hizo kampuni mbili. Nilitegemea tofauti isingekuwa kubwa sana.
Pamoja na hayo yule mbunge wa Gwasi alikuwa muelevu zaidi katika kujibu maswali kuliko Kabando wa Kabando(nafikiri nimepatia majina). Sijui ni makusudi au ni uelewa mdogo wa Kabando(nilimfananisha na Waititu Vs Kidero)alishindwa kujibu hoja na kung'ang'ania fujo za Kisumu,mbona Kenya kote kumetokea fujo za uchaguzi wa kuteua wawakilishi.
Pia upande mwingine Kiono na yule waziri wa ODM sijui Otuama? na Bi Murugi waliongea vizuri,tatizo ni aliyekuwa lecturer sijui anaitwa Kipchumba kakimbilia uanasiasa akawa muda mwingi analalama kuhusu chama chake na muungano wao ni wa ukabila. Hakuna asiejua kuwa Kenya kote ni ukabila na hakuna muungano wowote usio na chembe ya ukabila ndani yake na usiozungumzia mabaya ya wapinzani wake.
Hiyo ni mikakati au propaganda za kisiasa.