Watanzania kum attack Mkenya hapa kwa sababu ya kuonyesha mji wao na uzuri wake ni kuwa unreasonable.Mimi naongea hivi kama Mtanzania. Kila mtu ana haki ya kujivunia chao.
Lakini pia wasifu wa Nairobi ni mkubwa kuliko majumba na uzuri wa vionjo vya macho, unapouza bidhaa yenye upungufu toa disclaimer iliyo fair pia.
Nairobberry, kama sehemu nyingine nyingi, ina mapungufu mengi, kuanzia uhalifu, machokoraa mpaka kukosekana mlinganyo katika kugawana uzuri huu. kwa hiyo tangaza nchi kwa ajili ya kuvutia utalii kama hiyo ndiyo nia yako, lakini pia kumbuka una nafasi ya pekee (pengine kuliko hata Kenya Tourism Board) kuwaeleza watu kinagaubaga mabaya ya Nairobi, unaweza hata kusaidia zaidi kwa kufanya hivyo.