Asee kuna dogo pale Umoja, Nairobi, kampuni yake inaitwa Omosh Fabricators. Anafanya 'finishing' ya nje na ndani kwenye zile hiace ndogo, matatu za Nairobi, wanaziita 'nganya' kwa lugha ya sheng. Amejiamini sana na gari zake ni freshi sana kwa ndani na nje. Vijana wa East Africa, wakenya kwa watz, msidharau kazi zozote zile, kujituma ndo kila kitu, sasa hivi ni miaka zaidi ya kumi yupo kwenye kazi hiyo. Anapiga hela za maana huezi amini. Big up Omosh, namfahamu vizuri sana. 'Inspiration' na ajira anazowapa vijana wenzake, ni kitu cha maana sana.