Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Baadhi ya maeneo ya Nairobi yameanza kukumbwa na mafuriko kufuatia mvua zilizonyesha Jumamosi, Oktoba 31, hali iliyozua maswali kuhusu uwezo wa mifumo ya maji taka na mifereji ya jiji kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa katika msimu huu.
Katika eneo la Parklands, sehemu ya First Avenue karibu na Oshwal School ilifurika, huku wakazi wakishiriki picha na video za magari yakijaribu kupita kwenye barabara iliyofunikwa na maji.
Hali kama hiyo pia iliripotiwa Githurai, ambako maji yalifunika sehemu ya roundabout, huku basi la City Shuttle likikwama kwenye mtaro kando ya Bara bara ya Waiyaki Way.
Tukio hilo limeibua upya maswali kuhusu maandalizi ya Nairobi kukabiliana na msimu wa mvua wlza Oktoba hadi Desemba, ambao Idara ya Hali ya Hewa imeonya unaweza kuleta mvua katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Gavana Johnson Sakaja aliwahi kusema kaunti ya Nairobi imetambua maeneo 227 yaliyo katika hatari ya mafuriko na kuanzisha shughuli za kusafisha mifereji, kuondoa vizuizi na kufungua njia za maji. Kaunti pia ilisema ilikuwa imeanza maandalizi ya kuwahifadhi wakazi wanaoweza kuathirika na mafuriko.
Hata hivyo, mafuriko yanayoripotiwa baada ya mvua za kiasi yanaibua swali kuhusu ufanisi wa hatua hizo na kama mifumo ya kupitisha maji inaweza kuhimili mvua kubwa zaidi.
Wewe unaishi eneo gani Nairobi na hali ikoje huko? Ni maeneo gani mengine ambayo hufurika hata baada ya mvua kidogo? Na kwa mtazamo wako, tatizo ni mifereji kuziba, mipango mibovu ya ujenzi au maandalizi duni ya serikali ya kaunti?