Nairobi tops region with 5 times the number of skyscrapers as DAR es Salaam

Nairobi tops region with 5 times the number of skyscrapers as DAR es Salaam

Nairobi ilipofikia kwa sasa upande wa barabara na miundombinu mingine iko mbali sana. Hayo ma-fly overs ni balaa na nusu. Zamani kuingia Nairobi kama unatokea Arusha ilikuwa tunapita barabara za kawaida tu ila kwa sasa nimeona picha wanazo hadi za juu. Kuhusu majengo pia hatuwezi kushindana nao kwasababu wao wameachia matajiri wengi washushe vitu. Mji wa Nairobi una magorofa mengi yenye apartments za kupanga kwa watu wa kawaida kabisa. Ila bongo ukiona ghorofa ni kwa ajili ya wenye noti ndefu.

Kimsingi kwenye haya mambo ya miundombinu pamoja na majumba Nairobi imeiacha mbali sana Dar. Tatizo la Nairobi ni ule ubepari. Mtu wa kawaida kuja kujenga nyumba ni ndoto za mchana tofauti na Dar. Tayari matajiri wa Nairobi washashikilia ardhi.
 
2023 bado Dar haikaribii Nairobi kwa lolote
 
Back
Top Bottom