Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Bado nipo nashangaa sayari hii, tena nashangaa kiasi kwamba moyo wangu unapata matu matu na hakuna mtu wa kunifariji katu.
Nashangaa sayari hii ambayo mahusiano mengi yanakufa kwa kuwa, ndani ya mahusiano mwanamke anataka apendwe na ajaliwe kwa huba zito kama tamthilia za kikorea na kihindi anazozitizama kwenye runinga halafu mwanamme anataka tendo kali kama video za porno (XXX) anazozitizama kisiri siri kwenye simu yake. Napata wasi wasi mkubwa juu ya hili, na ndio maana mahusiano ya watu wengi hayawezi kusonga sababu ya ujinga wa wapenzi wote wawili.
Bado nazidi kuishangaa sayari hii. Sayari ambayo wana jamii wake ni wapumbavu wapumbavu tena wapumbavu wa kutupa. Yaani wanasimama hadharani wanasema Mwanamke mmoja kuwa na wanaume wengi ni umalaya, halafu mwanaume mmoja kuwa na wanawake wengi ni ulijali.
Sitaki, sitaki nasema tena kwa sauti SITAKI kuamini ujinga huu, kwanin wawe wanawake na wala sio wanaume, yaani mnataka kusema kufuri moja linalofunguliwa na kila funguo tunalitupa kwa masimango wakati funguo inayofungua kila kufuri tunaithamini na kuitunza juu ya mlango. Hapana, jamii yangu badilika.
Badilika jamii yangu, badilika uache kutamani pili pili kwa mvuto mzuri wa nje halafu uishie kulia kwa muwasho wake wa ndani. Badilika utambue kuwa wengine hawana kitu kabisa kwa kuwa wanaogopa dhambi, halafu kuna hao unaowasifu na kuwaita mashujaa kisa wana kila kitu japo wamevipata kwa haramu.
Badilika jamii yangu,😭😭. Badilika tafadhali
Wako katika kalamu AMANI DIMILE

Upvote
0