Naishauri Serikali itoe ruzuku Bima ya Afya ya watoto

Naishauri Serikali itoe ruzuku Bima ya Afya ya watoto

Danos

Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
89
Reaction score
104
Serikali hii yenye fedha nyingi mno kiasi cha baadhi ya watu kujichotea mihela bila aibu hata hofu ya Mungu haiwezi kushindwa kutoa ruzuku kwenye bima ya afya ya watoto.

Nilimsikia waziri wa afya akilalamika kuwa michango ni bilioni 4 wakati matumizi ni bilioni 40 (kwa mwaka?). Serikali hii yenye mifedha mingi ilikuwa ikitoa (na bado inatoa?) bilioni 100 kila mwezi kama ruzuku kwenye mafuta ili yashuke bei ambapo kwa mwaka ni Trilioni 1.2. Sasa kama mchango wa bima ya afya kwa watoto kwa mwaka ni bilioni 4 kuongezea hizo bilioni 36 (tena kwa mwaka mzima na si kila mwezi), kwa ajili ya watoto wetu na afya zao inashindikana nini?

Waziri analalamika kuwa watoto wanaenda kutibiwa private kwa wingi. Hiyo actuarial science haikuwapa sababu kwanini wanaenda huko kutibiwa? Boresheni huduma kwenye hospitali zenu muone kama wataenda huko. Lakini pia private hospitals nazo zinalipa kodi pia. Na mmezipa vibali vya kutoa huduma. Kama vipi mzifute tusiende huko sasa.

Watoto wetu wanapata tabu sisi watu wa vipato vya chini. Fedha nyingi zinaelekezwa kwenye mambo yasiyo na tija kwa wakati huu. Fedha zinaibiwa na kuliwa na wachache ambao hawajali shida za watu wa kipato cha chini.

Hela za bima wanakopeshana wao kwa wao mabilioni ya fedha, wanadai hakuna hela (refer ripoti ya CAG). Hii si sawaa kabisa.

Naishauri serikali iliangalie jambo hili na iache siasa kwenye afya za watanzania. Watoto ndiyo taifa la kesho, kama hatujali afya zao tunategemea taifa gani? Au kwa vile wakubwa ninyi watoto wenu wanatibiwa kwa gharama za serikali?

Toto Afya irejeshwe na kwa gharama ile ile ya 50,400/- kwa mwaka. Kinachopungua serikali hii yenye mifedha mingi ichangie hapo. Ruzuku itolewe kwa ajili ya watoto wetu.

Nawasilisha.

MUNGU LETA UKOMBOZI TANZANIA🙏🏾
 
Ebu ngoja niseme haya kwa mtazamo wangu:-
Unapo zaa mtoto then unampangia serikali, taasisi ama mtu mwingine namna ya kuku saidia majukumi yako sio sahihi kabisa.
Pili mtoto anapo zaliwa haji kwa bahati mbaya na wala sio shida zake. Mtoto wako ni matokeo ya starehe zako mkuu, hivyo tujifunze kuwajibika 100% kwa watoto wetu.
 
Huo ni wenda wazimu kama wa Elimu bure.
Zaa gharamika
Kwa hiyo kwako wewe ni sahihi fedha za umma kufujwa? Sitetei hapa swala la kuzaa na kugharamika. Ninachosisitiza ni matumizi mazuri ya fedha za umma. Badala ya kufuja, wazielekeze kwenye mahitaji kama haya.
Thanks.
 
Ebu ngoja niseme haya kwa mtazamo wangu:-
Unapo zaa mtoto then unampangia serikali, taasisi ama mtu mwingine namna ya kuku saidia majukumi yako sio sahihi kabisa.
Pili mtoto anapo zaliwa haji kwa bahati mbaya na wala sio shida zake. Mtoto wako ni matokeo ya starehe zako mkuu, hivyo tujifunze kuwajibika 100% kwa watoto wetu.
Rudia kusoma tafadhali na elewa ninachokikazia. Matumizi mabaya ya fedha za umma hayafai kuungwa mkono hata kidogo.

Thanks.
 
Back
Top Bottom