Naishauri Serikali ya Tanzania, watu wasiruhusiwe kuingia wala kutoka Dar, Arusha na Mwanza

Haitakua na maana kama serikali itasubiri hadi mambo tavurugike nso ichukue tahadhari
 
hilo jambo lilipaswa kufanywa siku Isabella alipogundulika

kwa sasa 'it's too late'

mbadala ni lockdown 2
 

Hii haiko mbali sana na ukweli:

Si haba kufahamu mfalme Mswati yuko hoi na Corona.

Mkuu unadhani mfalme Mswati alishindwa kununua sanitizer hata za bei mbaya?

Eswatini King Mswati III hospitalised with COVID-19: reports
 
Mkuu ujue tuliwaambia mapema kipindi kile ugonjwa unaletwa kwa ndege na meli toka nje ya nchi... Wangefunga mipaka yote... Kipindi kile...
Kwa sasa lockdown haina faida yoyote zaidi ya kufungia wagonjwa, wenye dalili, asymptomatic carriers na watu wazima ndani ya nyumba...
Na ndo tatizo linaloikumba USA kwa sasa...
 

Mkuu ni kweli kuwa muda wa thamani mno ulipotea walipopuuza kuzuia ndege kuingia (hasa zitokazazo maeneo athirika). Ni jambo jingine kuwa watu hao hao wangalipo kuendelea vita hivi hali ugonjwa umo ndani ya nchi na unaena.

Italy, Spain, Kenya, Rwanda, South Africa, USA, etc walifanya makosa kama hayo.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Wenzetu wameona walikojikwaa. Wamejikongoja na karibu wanasimama.

Sisi kama ilivyokuwa awali kabla ya ugonjwa kuingia mawazo yako kwenye njaa njaa na uchumi. Huku tukijifanya waumini kuliko walioko Saudia, Roma au Israel.

Hiyo ndiyo tofauti yetu. Angalau Ecuador serikali kule imeomba radhi kwa kuchelewa mno kuchukua hatua.
 
Kwahiyo kama ukigundulika unaumwa utaendaje hospitali kama hakuna usafiri?
 
So huna tena solution?
 
So huna tena solution?
Solution ni watu wapimwe kwa gharama za serikali... Wa roll-out mass-testing mitaani hasa hizo sehemu mnazohisi maambukizi ni makubwa...
Wanaoonesha dalili ndo wapelekwe karantini...
Ukiwafungia watu ndani bila kujua nani ana hali gani sioni kama utakuwa umesaidia chochote...!
Unakumbuka yaliyotokea India?? Wahindi walilazimima kutembea kwa miguu kutoka mijini kukimbilia vijijini...
Mkilazimisha lockdowns hapa kwetu mtakuwa mmewakimbiza watu wengi sana kurudi vijijini katika hali isiyo ya kibinadamu kabisa!!
 
Kwahiyo kama ukigundulika unaumwa utaendaje hospitali kama hakuna usafiri?

Mkuu hata huku nilipo kwenye huduma za kila aina hata simu hawapokei bali unaingia kwenye web yao tu ya hospitali na unafuata masharti
Hospitali hakuna kwenda unaambiwa mpaka ushindwe kupumua
Sasa kama nyie huko unatibika hongera zenu
Hili janga ni baya sana kama hawatazuia mizunguko hii kwa muda litakuwa janga kubwa
Fuateni masharti ya wataalamu
Tutaepuka na mengi na maambukizi yatapungua


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

Mkuu walishachelewa... Ugonjwa ushafika kwenye nyumba na vyumba vya watu wengi sana...
Kuwazuia watu kwa sasa ni sawa na kuwafungia na majoka au mafisi ndani...
Sijuhi lakini... Labda wajaribu...
 
Mkuu walishachelewa... Ugonjwa ushafika kwenye nyumba na vyumba vya watu wengi sana...
Kuwazuia watu kwa sasa ni sawa na kuwafungia na majoka au mafisi ndani...
Sijuhi lakini... Labda wajaribu...

Bado hawajachelewa maana wakiachia ndio madhara makubwa zaidi
Mkuu hali inasikitisha sana kwa sasa
Sisi huku tumepigika haswa ila tunawaombea huko lisiwapige


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

Haikuwa rahisi kumfanya Farao kusikia.

Eeh mola wetu, tuna ma Farao hapa kwetu (wanajiita majiwe) hebu sema nao katika ile lugha iliyomfanya Farao akaweza kusikia na kuwaachia waja wako kuondoka utumwani.

Ni hilo tu eeh mola wetu.
 
Haikuwa rahisi kumfanya Farao kusikia.

Eeh mola wetu, tuna ma Farao hapa kwetu (wanajiita majiwe) hebu sema nao katika ile lugha iliyomfanya Farao akaweza kusikia na kuwaachia waja wako kuondoka utumwani.

Ni hilo tu eeh mola wetu.

Mataifa mengi walipuuza hivi hivi wakifikiri ni kaugonjwa kadogo katapita na leo wanalia
Najumuika na wewe kumuomba Mungu pia


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…