Naishi na maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka 14

Naishi na maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka 14

Hivi ndo inavotakiwa watu tuwe katika hii mitandao ya kijamii,watu cku hizi mitandaoni hatufanyi mambo socially kabisa.mtu akitoa wazo watu hawampi support hata ya mawazo na unakuta mtu katoa wazo zuri lenye faida.na hii mambo naiona sana humu Jf.humu kuna watu kazi zao kukatisha wenzao tamaa,nini maana ya social networks, humu mtu anaweza akatimiza mambo mengi coz humu kuna kila aina ya watu so panaweza pakawa ni sources ya watu kupeana connection, kutengeneza urafiki wa karbu,kushirikiana kwa masuala Fulani Fulani, kama hvi mtu kusaidiwa kiushauri hata Katk magonjwa mtu anaweza akapata suruhisho ya tatzo lake sugu.Jf watu wabadirike.wenzetu watatuzidi kwa mengi kama sisi kwa sisi tusipoamua kunyanyuana.
 
Ndugu zangu wana JF nmekua nikisumbuliwa na tatizo la tumbo tangu 2005, tumbo limekua likiniuma kwa maumivu makali sana kwa nyakati tofauti.

VIPIMO/ TIBA
Nmepima vipimo mbalimbali katika hospitali tofauti na kwa nyakati tofauti bila kuonesha tatizo lolote. Baadhi ya vipimo nlivopima ni pamoja na HP piloy kile cha Ulcers, Ultra Sound, Blood, ODG, CT SCAN, Chronophology na vipimo vidogo kama UTI, MINYOO, TYPHOID, na KICHOCHO Lakin vyote haivijawahi ku detect tatizo lolote mwilini

UGONJWA
Maumivu nnayoyapata hua yanabadilika siku hadi siku kwa maana kwamba tumbo linakua na maumivu ya aina tofauti, kuna siku linajaa gas, kuna siku linabana na kufanya nipumue kwa shida. Ila kwa kiasi kikubwa sipati choo kama inavyotakiwa na inapotokea nmepata choo vizuri hali yangu hua nzuri na maumivu hupotea kwa mda

MADHARA
1. kutokana na hali hiyo kuna wakati nashindwa kwenda kazini kati ya mda wa wiki 2 nikiwa ninaugulia ndani hivyo kuathiri uchumi wangu (Nimejiajiri).
2. Hali hii pia imenifanya niwe dhaifu pale nnapokutana na mchumba wangu kitandani
3.Hali hii imenifanya nishindwe kutumia baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo kabla nlikua navitumia.
4.Hali hii imenifanya kuwa mpweke kiasi cha kuhisi nmemkosea nn Muumba wangu
5.Hali hii imenifanya wakat mwingine kujitenga na marafiki zangu
6.Hali hii inanifanya kushindwa kufanya baadhi ya kazi ngumu ikiwa ni pamoja na mazoezi

LENGO LA KUJA JF
Lengo kubwa la kuja kuanika tatizo langu hapa JF, kwanza ni kuomba msaada wa hali kwa maana ya ushauri jinsi gani naweza kuondokana na hili tatizo hatimae na mm siku moja niwe kijana nnayefurahia maisha yangu nikiwa na afya imara lakini pia nipate elimu namna gani hili tatizo naweza kuliondoa

NB:Kama kuna sehemu nmekosea kuandika kwa usahihi nipo tayari kusahihishwa hasa kwa ule upande wa majina ya vipimo. Umri wangu ni miaka 29.

Ahsanteni sana [emoji1488]
Pole sana. Maelezo yako yamenyoka kabisa, na hivyo ni rahisi kupata tiba sahihi. Hata hata hivyo napenda kujua yafuatayo ili niweze kuchangia maelekezo ya tiba.
1)Je, ukipata choo huwa laini au kigumu?
2)Je, mkojo una rangi hani unapokojoa?
3)Je, ni muda gani hasa maumivu yanapozidia, mchana au usiku?
Naomba majibu ya maswali hayo ili nione kama naweza kuchangia maelekezo ya tiba.
 
Choo kinakua dynamic. Kuna siku kigumu na kuna siku laini. Mkojo unakua mweupe pale ikitokea nmekunywa maji mengi ila nkinywa let say 1ltr mkojo unakua Njano.
Maumivu mara nyingi ni usiku na swala la kupata usingizi kwangu imekua mara chache sana zaid nakua najigeuza geuza tu kitandani adi ikifika alfajili ndo napata kdg.
Lakini pia kuna siku linauma mchana kutwa kutegemea kiasi gani nmeweza kupata choo
 
Duuuh Pole sana jamani. Jaribu kufanya water therapy. Unakunywa maji ya uvuguvugu angalau Lita moja alfajiri. Usiyanywe kwa pamoja kunywa Kama chai halafu ukae masaa kadhaa ndio ule kitu chochote healthy. Hebu jaribu. Saratani ya ini umecheki na ya utumbo? Nenda ocean road uone Kama ni negative. Pole sana

Ahsante ndugu Ntazingatia [emoji1488]
 
Hiyo ni gesi tumboni na kukosa choo...

1. Tumia matunda kama mapapai, parachichi, tikiti maji.
2. Pendelea chai ya tangawizi kali, iliki na mdalasini ukiweza weka habat soda.
3. Fanya mazoezi kila mara.
4. Angalia style ya kulala.
5. Usile ukashiba sana.
6. Unakunywa pombe?

1.Pombe sinywi. Mara chache sana nakunywa Sweet Wines
2.Matunda nazingatia sana..mwanzoni yalinisaidia ila siku izi sion impact yake.
3.Style gani nzuri ya kulala mkuu?
 
Sina mkuu
Nice mkuu kama hauna ilo tatizo jaribu kucheza na maji sana na vitunguu swaumu.naamini juu ya hiyo tiba ndugu yangu.fanya kwenda kwa huo utaratibu kama ukipata unafuu utatuletea urejesho humu maana yaweza ikawa solution kwako juu ya tatizo linalokuhusu.Fanya hivyo mkuu
 
Maji na vitunguu swaumu na matunda kama ukiwa na huo uwezo wa kila cku kupata matunda hata aina mbil au tatu itafaa..ila Maji sana tumia na vitunguu swaumu
 
Choo kinakua dynamic. Kuna siku kigumu na kuna siku laini. Mkojo unakua mweupe pale ikitokea nmekunywa maji mengi ila nkinywa let say 1ltr mkojo unakua Njano.
Maumivu mara nyingi ni usiku na swala la kupata usingizi kwangu imekua mara chache sana zaid nakua najigeuza geuza tu kitandani adi ikifika alfajili ndo napata kdg.
Lakini pia kuna siku linauma mchana kutwa kutegemea kiasi gani nmeweza kupata choo
Hali uliyonayo inanafanana sana na hali niliuyokuwa nayo. Nilihisiwa kuwa nina dalili za vidonda vya tumbo lakini kwa vipimo havikuonekana. Baada ya kupata tiba ifuatayo nilikuwa salama kabisa:
1) Omeprazole 20mg capsules kila baada ya masaa 12.
2) Kunywa maji ya vuguvugu kila wakati hasa unapopata choo kigumu. Jihadhari sana na maji baridi.
3) Epuka kukaa na njaa kwa muda mrefu.
Ikikupendeza, nipe mrejesho baada ya kutumia tiba hiyo.
 
Pole sana mkuu, kama wadau walivyosema hapo juu jaribu kuangakia na mfumo wako wa kula.

Unaweza kumtafuta Dr Boaz Mkumbo kwa kumfatilia youtube au fb ili upate muongozo wa lishe.
 
Sawa ndugu...nmeanza juzi doze
Tumia ndani ya wiki moja afu utatupa maendeleo yatavokuwa.dawa inayofaa ndani ya cku tatu lazima uanze kuona mabadiriko so wew Fanya hiyo dose kwa wiki moja,week ikiisha naamini majibu yatapatikana.Allah akujalie ndugu uwe sawa kama zamani.Ameen Ya Rabb
 
1. Sweet wine is good for digestion....
2. Matunda gani unapendelea zaidi? Nimekaa hapa napata matunda ya jioni nmekukumbuka mdau
3. Lala umelalia tumbo au kiupande. Usipendelee kulala umeangalia juu hata upumuaji si mzuri.
1.Pombe sinywi. Mara chache sana nakunywa Sweet Wines
2.Matunda nazingatia sana..mwanzoni yalinisaidia ila siku izi sion impact yake.
3.Style gani nzuri ya kulala mkuu?
 
Tumia ndani ya wiki moja afu utatupa maendeleo yatavokuwa.dawa inayofaa ndani ya cku tatu lazima uanze kuona mabadiriko so wew Fanya hiyo dose kwa wiki moja,week ikiisha naamini majibu yatapatikana.Allah akujalie ndugu uwe sawa kama zamani.Ameen Ya Rabb

Mkuu naona tatizo ndo linazidi cjapata nafuu ata kidogo...kila siku ya leo nafuu ya jana
 
Back
Top Bottom