Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

Jua tu kifo ni tukio la asili, halikwepeki, ponda mali kufa kwaja, subiri kama unavyosibiri X-mas na mwaka mpya
 
Ingekuwa baba na mama wamekufa na wewe ungekufa kabisa eti eeh.

Kifo kipo kinaishi Kama unavyoishi muda wowote cha weza kukukuta.

Vile hujafa ishi kama hutakufa milele,
 
Kifo kinapo kuja haupo tena, ukiwa mzima usiwaze kifo...maana kikija hukioni unakuwa haupo.wanao baki ndio hubaki na hofu.Kifo ni sawa na usingizi.Unapo panda kitandani kulala hujui ni muda gani uli ishia usingizini na huna kumbukumbu yoyote ya jinsi usingizi ulivyo kujia ni sawa na kifo pia.
 
Wewe kuwa tu na matendo mazuri, uliambiwa baada ya kifo kuna maisha mazuri Mbinguni kwa Baba. Kifo ni tukio la asili kama matukio mengine. Subiri kifo kama unavyosubiri mwaka mpya au X-mas.
 
Ahsante mkuu.... Ulichokisema ni sawa kabisa.
Sasa mimi inanitokea tu mawazo ya hofu ya kifo yanatawala akili yangu, japo nafahamu yote uliyoandika hapo.... Sasa nitumie mbinu ipi kuyafukuza hayo mawazo au kuzuia yasije?
mkuu nakushauri kama unaweza kufanya meditation fanya itakusaidia sna mkuu ata kwenye mambo mengne mengi yanayokukabili.
 
mkuu andres umeongea ukwel mtupu , mimi nilikua na hali kama hiyo mpka kuna mda nukahisi nausikia moyo unadunda nikiwa kwenye majukumu yangu , nimetumia zaid ya ml 3 kupima vipimo vyote vya moyo , washauri wa saikologia , nilijipanga kwenda india nikihisi nitakua na tundu kwenye moyo, mtu mmoja simple tu alinisanua ni vidonda vya tumbo nmesakata miti shamba , pombe stress na ulaji mbovu nmepiga chini now nipo poa mno.
 
Hii mbinu ya kushinda hofu ya mauti au mauti yenyewe Naweza kukupatia ila itafanya kazi tu endapo umeokoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…