Naishiwa damu kila mara, nifanyeje?!

Naishiwa damu kila mara, nifanyeje?!

Reptilia

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2018
Posts
867
Reaction score
847
Habari wakuu,

Naombeni kufahamu huu ugonjwa nilionao ni ugonjwa wa namna gani?

Nikianzia hapa ni kwamba toka mwezi wa 6 mwaka jana nilikuwa najihisi kuchoka sana kwa shughuli ndogo ndogo kama kufagia mapigo ya moyo yanaenda mbio hata kufagia ndani tu nashindwa.

Nimeshaongezewa damu karibu mara tatu lakin naona hili tatzo linajirudia tena..

Nimeshapimwa sicklecell imeonekana sina na hili tatizo limeanza mwaka jana tu toka nizaliwe.

Naombeni msaada wakuu hili ni tatizo gani?
 
Nenda kwa madaktari wanaohusika maswala ya damu. Yawezekana kuna shida kwenye chembechembe zako za damu hasa nyekundu ambazo huwa zinahusika. Mimi siyo mtaalam ila narejea sayansi niliyosomeshwa.
 
Uliongezwa damu kwa sababu ulikuwa na upungufu mkubwa wa damu uliokua unahatarisha maisha yako, madaktari waliokutibu walipaswa kukueleza sababu ya upungufu wa damu uliokua nao, Nakushauri uende hospital iliyopo karibu na wewe ukafanyiwe Vipimo watakuambia chanzo cha tatizo ulilonalo, pole sana mkuu
 
Nenda kwa madaktari hongera maswala ya damu. Yawezekana kuna shida kwenye chembechembe zako za damu hasa nyekundu ambazo hawa zinahusika. Mimi siyo mtaalam ila narejea sayansi niliyosomeshwa.
Si ndio maana ameleta tatizo hapa kadhaa viwanja na daktari kuwa Hana damu ndio anataka ushauri
 
Umezaliwa mwaka jana alafu shida imeanza mwaka huu?? Ma friend Growth Hormone yako itakuwa kabambe sana
 
Umezaliwa mwaka jana alafu shida imeanza mwaka huu?? Ma friend Growth Hormone yako itakuwa kabambe sana
Labda ni typing error,hata hivyo haihitaji degree kujua mtu huyu amekosea la msingi ungempa ushauri jinsi ya kufanya sio kukomaa na kosa dogo aliliolifanya,JF ni kwa great thinker tuu lakin nowdays duh
 
Labda ni typing error,hata hivyo haihitaji degree kujua mtu huyu amekosea la msingi ungempa ushauri jinsi ya kufanya sio kukomaa na kosa dogo aliliolifanya,JF ni kwa great thinker tuu lakin nowdays duh
Mkuu jifunze kusoma heading na contents....usiishie kusoma heading tu
 
Rudi kwa madaktari waliokuongezea damu wakueleze sababu. Vinginevyo tupige ramli tukuambie shida inayokusumbua. Jambo ambalo si sahihi.
Nakusihi rudi hospitali ujue tatizo uanze tiba mapema.
 
umezaliwa mwaka jana tatizo limeaza mwaka huu?
 
umezaliwa mwaka jana tatizo limeaza mwaka huu?
 
Kama daktari atakwambia sababu ya wewe kuishiwa damu mara kwa mara ni ipi, Nafikiri hapo tutakusaidia kiundani zaidi.
Kwani umeshapima anemia?
Hauna minyoo?
Huwa una-donate damu?
 
Back
Top Bottom