Naisi kuna mwanamke Anaishi nae

Naisi kuna mwanamke Anaishi nae

yes mai hazbendi....
Miaka mitano ni mingi sana.....
Kuimbiwa nyimboza mapenzi tu....
Hujui anapoishi, hujui hata ndugu yake mmoja?
Kwa wapendanao wenye mapenzi ya dhati hii haiwezekani.....

Come on Asprin,
wewe mwanaume unajua....
Jinsi gani kigezo cha 'nampa talaka mke wangu'....
Au ' nimemuacha mke wangu'
au 'nitamtaliki mke wangu kwa ajili yako' inavyokuwa ni usanii mtupu....
Jinsi wanaume wanvyotumia maneno hayo ili kumlainisha mwanamke......
Ili mwanamke adhani kuwa atamilikwa yeye....

mimi shtukaaaa
hakuna kitu hapo...
Kuwa serious....kama anakuoenda atakupeleka...

Mpeleleze upajue kwake halafu uende wakati mwanaume hayupo.....
Ila hakikisha huna matatizo ya presha kabla ya kufanya hivyo....

usanii mwingine wa wanaume---nilimuoa mke wangu kijijini nililazimishwa na wazazi,ila siwezi kuishi nae,subiria namtafutia kisa nimuache,utamsubiriaweeee holaaaaa!
mimi nakupa mfano live-shemeji yangu wa kuzaliwa tumbo moja na mume wangu alikuwa na msichana kwa miaka minne mapenzi motomoto,mdada akajua ndoa inakuja,inakuja,shemeji ana kaka yake binamu mtu mzima anakaa temeke(nae moto chini balaa),mdada anaambiwa pale ndo kwa baba mdogo aliowalea,na akienda anapokelewa na mwanamke anajua ma mdogo,kumbe shangingi la mjini linakujaga wakijua anakuja,mdada akaanza kuomba kujua kwa mwanaume,anapewa hio sababu ulizopewa ooh pale kuna watoto wa mke wangu tulioachana sitaki wakujue mapema,mpaka washtukie ndoa imeiva.mdada alisubiria weee,mimi kwa bahati siku moja nikapita pale nikitokea msibani(jirani yangu alifiwa na ndugu yake msiba ukawa kama mitaaa minne hivi toka pale)nikawakuta shemeji na mdada,binamu na mwanamke jimama,nashangaa shemeji anajiumauma,mara lile shangingi likasepa(mamdogo feki)kifupi,nilikuwa chanzo cha yule dada kujua ukweli,japokuwa mwanzoni alinichukia sana eti alinijia juu akijua mimi ni hawara wa bwanawake,akanijia juu,ikabidi shemeji aniombe radhi,nami nikampa ukweli wake yule dada palepale,HAKUAMINI ,lakini baada ya kama miezi miwili alidhibitisha nilichomwambia na akanishukuru sana!yule shemeji yangu ana mke na wala hana dalili ya kuachana na mke wake na wana watoto watatu!
huyu mwanaume wako kama anafanya kazi mpeleleze kupitia ofisini kwake,mbona rahisi sana kujua wewe mbona unanishangaza jamani,miaka mitano we hupajui kwake unakubali tu,eti kila weekend anakuja moshi,sasa cha ajabu ni nini?hujui kwamba humu majumbani kuna wanaume wanajifanya wafanyabiashara wa weekend kufuata mizigo ya biashara?yawezekana anamdanganya mkewe anafuata mzigo,kumbe mzigo anatuma tu hana haja ya kwenda!
kifupi huyo hawara yako ni mume wa mtu kwa asilimia tisini!
 
Miaka mi5?? mamito inaonekana unatowa Sex tamu kweli kweli ila hufai kuwa wife,

ukute alioa ndani ya mahusiano yenu hayo, hayo. shtuka!

ayaaaa.....mweee....
bi dada mimi stuka....kama hujamjua vizuri mpenzio ndani ya miezi 5 na nusu tupa kule.....garasha hilo hakuna kitu.....
 
Last edited by a moderator:
ayaaaa.....mweee....
bi dada mimi stuka....kama hujamjua vizuri mpenzio ndani ya miezi 5 na nusu tupa kule.....garasha hilo hakuna kitu.....


nahisi mamito mimi kisha shtuka, hapa anataka tu support ya confirmation.

Ila mimi mamito ukimuacha utakuwa una do na nani? sex mhimu ujue. bora tu uendelee ku do nae

huku unatafuta mchumba, kuwa tu practical, kama umesubiri miaka mi 5 wat is a year ahead?
 
Last edited by a moderator:
acha roho mbaya, mwenzio anataka umwambie ni mchumba. teh teh teh

Mh,hata sielewi muda wote huo alikuwa anamwabia nn wakikutana. haya mahusiano ya sasa yana usanii mwingi sana sasa inabidi mtu uwe sharp kudodosa mapema kama unaona hapaelweki unasepa. to me miaka mitano ni mingi sanaaa miezi tu nshajua ukweli. kuwa mdadisi dada.
 
Mimi wangu alinikatalia katakata kumlia hotelini! Mpaka nilipomwonesha home then ndo nikaanza kujilia kiulaini kabisa kama vile namsukuma mlevi
wapendwa!

Naitaji ushauli wenu boy friend wangu wa miaka mitano hajawahi kunipeleka kwake tangu tuanze uhusiano ni tumekua tukikutana hotelini tu

Yeye anaishi Dodoma mimi naishi Moshi kwa muda wote huo wa miaka mitano

Kinachonifanya niisi anaishi na mtu Nikimuomba twende kwake uwa naniambia kua hatuwezi kwenda kwa sababu ya watoto wanaishi pale mpaka tukishaoana ndio atanipeleka kwake,hao watoto wawili alizaa na mwanamke mwingine alimuacha kwa sababu alimfumania huyo mwanamke akifanya mapenzi na mwanume mwingine nyumbani kwake

Nikimuambia tuachane analia na hataki kabisa kusikia hilo swala

Nifanyaje ndugu zangu ili nijue ukweli?nampenda sna na yeye ananipenda pia haipiti week bila ya yeye kusafiri kunifata moshi kuja kuniona na amekua ni msaada mkubwa sana wa maisha ya yangu(ki ushauli and financially) though simtegemei sana kipesa maana mimi mwenyewe najiweza kipesa
 
umeingizwa chaka shosty..na jamaa kashajua akudanganye anakupenda halafu unajiona the only one!! hebu fanya surprise visit kwake, liwalo na liwe.....
 
Mimi., ningependa kukuuliza nani anamtembelea mwenzie wewe au yeye au both of you exchange visit.
Chengine, kitafute kitabu 'why men marry bitches'
 
Sorry! Ulimaanisha miezi mitano au? You can't be serious kusema miaka mitano! Otherwise na wewe huna mwelekeo unajishikiza tu liwalo na liwe! Pole!
 
Hapo uliposema anakupenda sana,kidogo punguza ncha.Kwasababu,kama ingekua kweli,hao watoto angeweza hata kudanganya ni rafik yake wa kazini,au anything angalau ukapajue kwake,hata mkalala hotelin,au hata

mda ambao watoto hawapo.Incase of anything,coz i believe ur all grown ups,besides you hav a 'us future'ahead of u,so no need to hide anything. Ata ivo hao watoto sindovizuri wakuzoee,au mkioana mtahama makazi muwaache watoto.
Pili,kuna mwenzio mmoja,alikuwa akikohoa,jamaa anatoka Mwanza anamfata Arusha hata kwa ndege,siku bibie alipoamua kufatilia,akamkuta mwenzie kajaa ndani tena mjamzito,na uzuri bibie alienda as a relative wakat jamaa yupo job,akapata ukweli woote..jamaa akadai eti, ni mke wa rafik yake,but mwisho wa siku ukwel ukajulikana na kila mtu life goes on!
Samahani kama nimekuwazisha,au cjaelewa ila muhimu uwetayari 4anything,na do not force,we mwanamke bana,mlainishe kwa kipaji ulichonacho..akuelekeze kwake akigoma,kuondoa doubt moyoni,mpandie uko uko,ila ujipange 4anythng.
Kwa upande mwingine,mhh labda anasababu zaidi ya iyo,nzuri kwa manufaa yako!em jitahidi muondoe vidoa moyoni,isijeathiri how u feel 4each other!


Umenena sweets
 
Duh pole sana dada yangu kwa mtazamo wangu mwambie ukwl unahitaji kwenda kujulikana kwa wazazi kuhusu swala la watoto utamua mwenyewe kuwalea usimwache mwenzako nakuomba.


Asante Emma
 
Mimi., ningependa kukuuliza nani anamtembelea mwenzie wewe au yeye au both of you exchange visit.
Chengine, kitafute kitabu 'why men marry bitches'


Yeye ndio anakuja kwetu zaidi
 
Ah we nawe shtuka bana.usiwe kama mtoto unadanganywa kwa pipi... Eti nkimwambia tuachane analia kutoa machozi yake ni usanii mtupu kama movie za kihindi vile
 
ukipenda chongo huona kengeza! my dia mimi tumia akili hata za kuazima. . . kuna mdada m1 yeye husema hata km atawekwa kuwa small haus atahakikisha anapafahamu kwa huyo mwanaume na anamfahamu mke wa hyo mwanaume. sembuse bf lol. . .
ukiona manyoya!
 
Sasa nimeelewa kwa nini baadhi ya wazazi wameweka utaratibu wa kuwajua ma boyfriend wa mabinti zao. Kama mtu mzima anaambiwa cheap lies na anakubali hao mabinti zetu wadogo itakuwaje?

Haya wenye watoto wa kike punguzeni ukali ruhusuni wawalete wakwe zenu home.... muwasaidie kufanya maamuzi. Si unajua jitu ambalo ni tapeli haliwezi thubutu kuweka mguu ukweni? Maana lazima apigwe interview na ndani ya dk tano ukweli unajulikana.
 
ukipenda chongo huona kengeza! my dia mimi tumia akili hata za kuazima. . . kuna mdada m1 yeye husema hata km atawekwa kuwa small haus atahakikisha anapafahamu kwa huyo mwanaume na anamfahamu mke wa hyo mwanaume. sembuse bf lol. . .
ukiona manyoya!


Naumia jamani
 
acha roho mbaya, mwenzio anataka umwambie ni mchumba. teh teh teh

Miaka 5 na mechi zote kiwanja cha ugenini, jamaa hataki uwanja wa nyumbani na yeye bado hashtuki tu!
 
mimi, kwanza naomba nikusute kidogo kisha nitakwambia cha kufanya, niliwah kuuliza hili swali hapa jamvini tena nakumbuka nilimention na kuquote post ya platozoom. hivi kweli mimi wewe ni mwanamke unayejipenda kweli? Hivi kweli ya Mungu juu ya upendo ipo? Kwanini kwenu mapenzi mpaka yatawaliwe na ngono tu? kwanini lakini kufanya haya mambo kabla ya wakati wake.......!!



yan gfsonwin natamani uendelee maana huyu mdada anasikitsha ye na huyo mchumba wake wanafuata ule msemo wa kiswahili eti "mwanamke ni chombo cha sterehe'' utafkisha hadi miaka kumi hakuna cha ndoa wala pete ya uchumba!! na starehe ikishamuisha anabadilisha line ya simu tu!! uone kama utapata hata chance yakumlaumu!! hayo ni majanga mdada(mimi) anakuahdi ndoa ili uzidi kumsterehesha!! haya mi simo!!
 
Back
Top Bottom