kimsingi, kwa mujibu wa sheria ni vigumu sana suala hilo kutokea, hii inatokana na sheria ya ushahidi ilivyo pamoja na sheria nyingine, kwanza kosa tajwa huanzia polisi kwa upelelezi, kosa huripotiwa kwamba fulani kaua bila kukusudia, jambo la kwanza kwa mpelelezi ni kumuona aliyeuwawa, kama hujamuona marehemu unafunguaje jalada? pili ni kumsaka muuaji, tatu kumpeleka mahakamani, cha kwanza katika ushahidi ni wale walioshuhudia tukio au waliowaona marehemu na muuaji mara ya mwisho, pili ni postmortem report, kwa hiyo ni vigumu sana kuhukumiwa kwa kosa la kuuwa wakati muhusika yu hai!!!