Naitaji msaada wako docta

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Habari

Napenda kuchukua fursa hii kuwajulia hali zenu wadau

Doctor naitaji masaada wako wa ushauri au matibabu kama ikiwezekana
mama yangu anaumwa moyo umepanuka na kujaa mafuta, na vilevile
anasumbuliwa na figo ameshaenda hospitali za watu binafsi zile za
kama docta dondi ametibiwa na kupewa madawa na pamoja na
ushauriwa ale vyakula vya aina fulani ili apone, dozi ya kwanza
alipewa ameshamaliza mwezi na alikwenda hospital kupima wakamwambia
kuwa mafuta yamepungua kiasi fulani kwenye moyo ila tatizo la figo bado

akashauriwa na kupewa madawa mengine ambayo anamaliza mwishoni mwa
mwezi huu na ameambiwa ikifika sikuu ya idd ikimalizika aende kufanyiwa
checkup zaidi , ila bado ananalalamika maumivu kwenye moyo na zile dawa
zimefanya ajisikie vibaya. Naomba ushauri wako tufanyeje au tumpeleke
hospitali ingine akapate matibabu mengine mapya? au ni dawa gani tena
atumie maana kila siku analalamika anaumwa tumbo sasa nasi
tumechanganyikiwa tufanyeje? Naitaji msaada wako pls nisaidie hapa
tumwokoe maisha ya mama yangu kwani bado tunamhitaji

asante.
 
Anatumia dawa gani,unaweza kuorodhesha majina ya hizo dawa?
 
Aje Peramiho: acheni kwenda kwa waganga wa kienyeji matokeo yake mnawapoteza/kuwachelewesha ndugu zenu kwa matibabu yasiyowasaidia. Haya aje tuone shida zake na tumtibu
 
Je, ana uzito na urefu kiasi gani?
Mara ya mwisho kufanya vipimo vya moyo naafuta mwilini ilikuwa lini, na majibu yake yalikuwaje? Ni dawa gani hasa amekuwa akitumia? na kwa muda gani alishawahi kukaa bila dawa?

Mwisho unapatikana wapi (mkoa)?
 
Pia: Ni vyakula gani alivyoshauriwa kutumia? Je anaweza kuelezea mlo wake wa siku japo kwa siku 3? Je anaweza kutembea kwa miguu japo dakika 10?.

Je, ana uzito na urefu kiasi gani?
Mara ya mwisho kufanya vipimo vya moyo naafuta mwilini ilikuwa lini, na majibu yake yalikuwaje? Ni dawa gani hasa amekuwa akitumia? na kwa muda gani alishawahi kukaa bila dawa?

Mwisho unapatikana wapi (mkoa)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…