Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Hizo likes unauza?.....
Maana [emoji23][emoji23]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] wakuu bhana "likes/thanks" ni kama motisha tu kujua kwamba kuna kundi kubwa la watu lipo nyuma yako likiku support kwa namna moja au nyingine.

NB: nimejibu kwa niaba ya mhusika.

Smart guy
Hivi likes zinakuongezea nn??

Naona unaziomba
 
[emoji2][emoji2] Mambo ya kilimo haya acha kabisa, Siku nimeamua kurudi shambani nilienda kumuaga maza,

Alichonijibu "Unadhani Kilimo unachoenda kufanya ni tofauti na kile ulichokua unafanya kwa bibi yako? Haya kila la kheri" baada ya kurudi toka shamba mpaka leo nimetulia zangu kwa mkaburu sina shobo na mashamba kabisa.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]naon umeamua kutulia
 
... Nilipata mzuka wa kuingia kwenye kilimo baada ya kufanya kazi kwenye shamba la matikiti la mzee mmoja hivi. Mavuno aliyoyapata ndio yalinishawishi na mimi kujikita huko.

Kutokana na ka akiba ambako nilikuwa nimekusanya mpaka muda huo, nikatafuta shamba kule kule Songea. Nilibahatika kupata eneo la kukodi sehemu fulani inaitwa Mpitimbi, heka 1. Kuna dogo nilikuwa nimezoeana nae kutokana na mishe za vibarua, huyo ndio nikawa napiga nae. Niliandaa shamba vizuri (robo 3 heka),weka samadi ya kuku, mwagilia kwa muda wa wiki kama mbili alafu ndio nikapanda mbegu zangu. Siku chache baadae zikaanza kuchipua. Ila walitokea wadudu wakaanza kushambulia yale majani mawili ya mwanzo kabisa. Nikajitahidi kupiga sana dawa, hatimaye nikafanikiwa kudhibiti. Hapo ile robo heka iliyobaki wazi,nikaweka maharage ya njano,lengo ni kujaribu kuona mwelekeo wake pia.


Miezi ikakata, tikiti zikatoka vizuri japo sio kwa wingi na ukubwa niliotarajia. Utata ukaja kwenye soko. Nakumbuka mnunuzi alikuja hadi shambani kwangu. Wakati mm gharama toka mwanzo mpaka yanakomaa nilitumia kwenye kama laki 7 mpaka 8, ila hesabu za kuyauza yote hela iliyokuja ni kama laki 3 na 40. Tulizozana sana na yule mnunuzi, ila mwisho wa siku ikawa ndio hivyo. Mpaka leo ile karatasi ya mahesabu na yule mnunuzi ninayo (Badae naweza nikaiweka hapa).

Kule ikabidi nitoke baada ya kuvuna na yale maharage pia ambapo nilipata kilo kama 60 (mimi nilipanda kilo 15), nikatafuta eneo jingine la kulima. Kuna sehemu inaitwa mshangano, kuna bonde la umwagiliaji, nikapata nusu heka. Nikaamua kulima tena tikiti, maana kila nikifikiria yule mzee wa kwanza alivuna fresh tu kwanini mm ishindikane?

Mwanzo mambo yalienda vizuri tu. Dawa nilikuwa napiga kila baada ya wiki au wiki mbili kutegemeana na aina ya dawa. Nakumbuka yalikuwa yamebakiza kama wiki 3 yatimize miezi mitatu, nilienda kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida tu na kupiga dawa. Kama sikuzimia siku ile basi sizimii tena. Nafika shambani, kila tikiti unaloshika linabonyea, kugeuza chini limeanza kuoza. Nilisizi kwa dakika kadhaa, nikakaa na chini kabisa.

Badala ya kuuzia watu, niliishia kumuuzia mfuga nguruwe, kiufupi yakageuka chakula cha mifugo.


Ile kilo 60 ya maharage ambayo nilikuwa nafikiria pengine nije kuyafanya kama mbegu upya maana mwelekeo wa kilimo chake niliuona kidogo mzuri,nilikuwa nayatunza gheto. Nilipoyavuna na kuweka kwenye kiroba,sikuyapiga dawa,siku nakuja kuyacheki nakuta matobo matobo tu,wadudu washapita.


Kutokea hapo nikafulia upya. Nikaanza tena kufanya vibarua. Kuna jamaa akanishawishi sana tulime mahindi maana yanalipa ila sikumuelewa, nikaendelea na vibarua. Kuna siku nikapata tenda ya kuvuna na kupakia tangawizi kwenye lori, maana kuna mteja alinunua sasa anahitaji huo msaada. Nikaenda kupiga kazi, hiyo sehemu inaitwa Madaba. Tunalima na kujaza kwenye maroba, kila ukijaza kiroba kimoja unapewa 5000. Baada ya kama siku 5 kazi ikaisha tukarudi na lori hadi town Magingo kwa mbele kidogo kuna soko la tangawizi . Kufika pale baada ya ukaguzi, nikapata kibarua cha kupakia kwenye lori la mteja. Kazi imeisha, naenda kupokea ujila wangu, nakuta bosi ni faza, yani baba angu kabisa. Kumbuka hapo tokea nilipoondokaga home sikiwahi kurudi wala kuwa na mawasiliano nao. Na toka tunazaliwa,baba alikuwa anajishughulisha na biashara za kununua na kuuza mazao,japo kipindi naondoka nyumbani alikuwa shughuli zake zilikuwa ndani ya mkoa wetu tu,kati ya vijijini na mijini. Na ndio biashara iliyotukuza,kumuona pale maana yake biashara zake zimepanuka.

Tuliangaliana kwa dakika kadhaa, natamani kama nimkumbatie, maana kiukweli baharia nilikuwa nimeshapigika sana. Atleast hata ningekutana na mama katika mazingira yale walau ningepata faraja kidogo, mshua kauzu ananiangalia tu bila kusema chochote.

Nikamwamkia akaitikia vizuri. Ikabidi nimuombe msamaha. Badala ya kuitikia, ananiuliza hapa umekuja kuniomba msamaha au kufata ujira wako? Nikamwambia lengo ilikuwa ujira mzee, ila baada ya kukuona sina budi kuomba msamaha. Mshua ananiambia kama ungetaka kuniomba msamaha ilibidi urudi unifate nyumbani, yani tunakutana tu kwa bahati mbaya ndio unaomba msamaha, tusingekutana je?

Nikawa mpole kidogo. Ila nikamwambia natamani kurudi ila nauli ndio ilikuwa tatizo, lasivyo ningesharudi kitambo. Mshua akasema utarudi nyumbani kama ulivyoondoka, yani nikupe nauli ili tu uje kuniomba msamaha? Kama kweli unania basi tafuta nauli urudi, we si mwanaume? Nikamwambia lakini nauli ya kunitoa nyumbani ulinipa wewe, kwanini usinipe na ya kurudi, maana sina kitu kweli.

Nikimwangalia mshua naona kabisa kuwa ananionea huruma, ila kwa nje ameamua kuleta ule ukauzu wa kiume. Acheni mama aitwe mama tu, pale angekuwa yeye nadhani yale maongezi tungekuwa tunayafanya huku tumekaa sehemu tunakula. Faza alikuwa mkavu usoni hadi na mimi nikaanza kupata wasi wasi kama ule wa kwake wa kipindi kile, kuwa mimi ni mwanae kweli? Ila nilivyokumbuka ile kauli ya mama alafu nikaangalia pua ya baba, nikaona bila shaka huyu ni baba angu.

Baada ya kuniangalia sana, sasa sijui kama na yy alikuwa anawaza kama kweli me mwanae, au alikuwa anaangalia pua ili kuthibitisha kauli ya mama, sijui. Ila alimuita Mfanyabiashara mwenzie aliyekuja nae, wakazungumza pembeni alafu nikaona kapewa hela.

Alirudi kwangu akanikabidhi laki 3 na 50. Akaniambia "Ujue kama ungekubali kuendelea na shule, basi ile hela niliyokupa mara ya kwanza isingetosha, awamu ya pili ilibidi nikupe tena. Sasa hii hela ninayokupa kuna posho yako ya kazi ya leo pamoja na ya mahitaji yako ya shule kipindi kile kama ungesoma. Hata siku moja usijekusema hukusomeshwa.

Nikapokea ile hela, nikashukuru sana. Mshua yeye ananiangalia tu. Nikamuomba tena msamaha. Ila msimamo wake ukawa ule ule, ukitaka kuniomba msamaha rudi nyumbani,maana hujui hata mama yako yupo na hali gani miaka yote umeondoka na hakuna anayejua upo wapi. Kwa mara ya kwanza nikakumbuka kuulizia hali za ndugu zangu kule nyumbani, hasa mdogo wangu wa mwisho na Mama. "Ukitaka kujua hali zao, fanya matumizi mazuri ya hiyo hela, sina haja ya kukwambia hali zao, rudi nyumbani ujionee" ilo ndio jibu alilonipa.


Tukaachana, nikarudi zangu kwenye ghetto langu kule moonlinght. Pamoja na maongezi yote yale na Mzee, ila sikumuomba namba ya simu, sio kwamba sikukumbuka, ila nilikuwa nasubiria walau aniulize kama nina simu. Na yeye hakuniuliza wala kuomba namba yangu. Sio kwamba hakufikiria ilo, nilikuja kujua baadae kuwa nae ilo swala alilifikiria ila hakujishughulisha nalo.

Huwa tunarithi vitu na tabia toka kwa wazazi wote wawili, ila nahisi wanaume tunarithi vingi sana toka kwa baba zetu kuliko toka kwa mama. Ukiona huna tabia unazofanana na mzee wako,muulize mama vizuri pengine huyo baba ni mlezi tu


*** *** *** *** *** *** ***


Kesho yake wakati naendelea kutafakari namna ya kurudi nyumbani, jioni nilienda kwenye kijiwe cha draft sehemu moja inaitwa Bombambili. Story za hapa na pale, kuna jamaa akaanza kuongea kuhusiana kilimo cha mbaazi jinsi kilivyo na hela na soko la uhakika. Baadae nikapiga stori kwa kirefu na yule mdau, tukabadilishana namba.

Niliporudi ghetto, baada ya kutafakari sana nikajiambia inabidi nisubirie msimu wa kilimo ufike nilime mbaazi hata msimu mmoja, nipige hela alafu ndio niende nyumbani.

Nikaghairi kurudi nyumbani kwa wakati ule, nikaanza ushanta ili nipate hela ya kujazia kwenye mtaji. Hutakiwi kujikita kwenye kilimo ikiwa unapresha. Kilichoenda kunikuta sitakaa nisahau kamwe. NILILIMA MBAAZI KIPINDI CHA MAGU.

Analyse #Baharia wa nchi kavu.

........
Dah mpitimbi.... Nilikuwa hapo mwaka jana july
 
Kusema ukweli wanaume wanaosoma hii story Tunatakiwa kuwa kama mshua wake Analyse..yule baba ni watofauti sana sana.

Kwanza hakumlazimisha mtoto kwenda shule hilo ni jambo zuri sana kama mzazi (tukubali tukatae)

Pili baada ya kutomlazimisha hakumfukuza tu kama mbwa nyumbani kama wafanyavyo wazazi wetu wengine,ila alimpa analyse ADA yake atakayoitumia Shule aende AKAILE MWENYEWE (hapa mzee alinawa mikono)

Baada ya kumpa Ada alimwambia achague mawili..kwenda shule au Kujitegemea (analyse alichagua kujitegemea) kwa mtaji wa ADA YAKE(sitegemei kuja kuona analyse anamlaumu baba yake hata kidogo)

Hiyo haitoshi wamekuja kukutana tena na mshua macho kwa macho Mshua akampa tena BAKI iliyobaki kwenye ile ADA YAKE (huyu baba nimemkubali kwa asilimia 5000000)

Kwa simulizi hiiii pamoja na mapito ya kujifunza kupitia analyse ila kuna BABA ANALYSE huyu mzeee nina uhakika leo hii analyse anasimulia haya ila anampenda BABA YAKE kwa kipimo kisichopimika(au uongo Analyse )

Endelea mkuu na simulizi..sema nini mwambie mshua wako (ambae ni baba yangu pia) Kuna mwanae asiejulikana anamkubali vibaya mno,kwa kudhihirisha hilo naomba unambie mtandao wa simu anaotumia mshua (sio namba ya simu) nataka kujua tu mtandao anaotumia kuwasiliana. (ukishafanya hivyo nina zawadi yake nitakutumia PM) tafadhali MFIKISHIE KAMA NITAKAVYOKUTUMIA WEWE.

#Tuendelee #na #story #mkuu
Kabisa mshua wa analyse

Anahtaji zawadi

Zawadi kubwa sana

Siku ya wababa ya leo , naiazimisha kwa baba yake analyse na kwa baba yangu

Advance nakumbuka nlsoma shule tatu

Primary shule tano

nlkua kivuruge sana , ila mzee hakuwahi nikatia tamaa

Teh ..


Heshima kwenu wadingi ...


Leo na mtoto anaitwa theodore ...

Nakumbuka huu msemo pia wa mama" mwanangu utakuja kuwa na watoto

Teh ...

Juzi kaiba penseli za wenzake wote

Kesi bado sijaimaliza
 
Story nzuri ila ya uongo...huyu mchizi story zake za nyuma alishasoma tuition kwa mudy mchikichini na kasoma azania kama sijakosea hapo hapo leo hii alikuwa hapajui dar...all in all muandishi mzuri...big up broda

Yaani humu unaamini kila kinachoandikwa na watu juu yao duh!!!!

Kupindisha ni kama kawa mimi mmoja wao.. sanaaaaaaa nikijiongelea lazima mengine niweke kiutofauti.. ni kuwa mjanja tu
 
""Nikamwambia lakini nauli ya kunitoa nyumbani ulinipa wewe, kwanini usinipe na ya kurudi, maana sina kitu kweli. ""

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
Kabisa mshua wa analyse

Anahtaji zawadi

Zawadi kubwa sana

Siku ya wababa ya leo , naiazimisha kwa baba yake analyse na kwa baba yangu

Advance nakumbuka nlsoma shule tatu

Primary shule tano

nlkua kivuruge sana , ila mzee hakuwahi nikatia tamaa

Teh ..


Heshima kwenu wadingi ...


Leo na mtoto anaitwa theodore ...

Nakumbuka huu msemo pia wa mama" mwanangu utakuja kuwa na watoto

Teh ...

Juzi kaiba penseli za wenzake wote

Kesi bado sijaimaliza
Yaan huyo mtoto km wangu kbs[emoji23] [emoji23] [emoji23]. Mwl alichoka kusuluhisha ikawa kila kesi naitwa shule, loh!
 
Kuna lile shairi tulisoma shule ya msingi la wana ndugu wawili SADIKI NA CHITEMO, sasa CHITEMO alijiongeza kama wewe ulivojiongeza ila ALIPATA TABU SANA.

kuna mdau huku juu amequote baadhi ya MISHORORO ya shairi hilo.
Kama unaweza mkuu weka lile shairi hapa tukumbushane enzi za mwalim
 
Back
Top Bottom