Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...


Mkuu thread yako inanifurahishaga sana, uliachwa huku umetundikwa miguu juu
 
Nukuu
" Utapewa pole jikoni,ila najua ukifika mjini utapost kuwa umejigonga kwenye kiti" Alaf akaangua kicheko.

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Nimecheka sana hapo, mzee ni noma kwa vituko vya ukweli.

Shukrani sana mkuu Analyse kwa stori hii, hakika imejaa funzo kubwa sana miongoni mwetu tunaohustle kwa life, imejaa hekima na burudani tosha za mzee wetu.

Hii ndio faida ya fasihi simulizi(kuelimisha, kuburudisha).

Toka mwanzo hadi hapa story imenasa kichwani kushinda definition fupi ya Colonialism endapo ningekuwa naikariri isinge nasa haraka kama stori hii.
 
HKL ya mtaani imetufundisha mengi. Angeenda shule tusingeyajua haya yote
 
Happy Father's day
 
Ukifika mjini utapost kuwa umeumia sio [emoji28][emoji28]. Story nzuri sana dah nakumbuka kipindi namaliza form 4 nilikua nalala sana ndani na kuangalia TV mda mwingi, siku mzee akanizingua kwamba mtoto wa kiume toka nenda town kaangalia watu wanaishije wanapambana vipi na maisha sio kulala tu kama huna pesa useme nitakua nakupa.
Basi akawa ananipa nauli naenda kuzurura dah sema miaka 2 mbele Mungu akamuita 2013. Hii story imenifanya niwish angekuwepo muda huu labda ningepata vingi zaidi.
RIP dad.
 
Happy Father's day
"Mfanye Mama yako awe na furaha, kisha njoo uniulize najiskiaje"

Ilo ndio jibu alilonipa Mzee nilipomwambia "Happy Father's Day"

Baba yangu anaamini ili familia iwe na furaha, basi Mama inabidi afurahi. Ukitaka kumgusa kila member wa familia, basi wewe mguse Mama.
 
Moja ya story bora niliyosoma mwaka huu though Jf apps yao inanizingua, ila nimejaribu kutumia plan B kupata mafunzo hadi mwisho ..kikubwa ni kupambana hadi mwisho usipo fanikiwa leo utafanikiwa kesho au keshokutwa ..kitu cha pili wakati mwingine unaitaji msaada kwa waliofanikiwa wakuongoze kuelekea njia ya mafanikio usiogope kujishusha.
 
Nilichogundua kua baba ako ni mtu poa sana na we hukulitambua hili tokea mwanzo, hustle zote ulizopitia ni kama ulijitakia tu kwa sababu ulienda kinyume na mtakwa ya baba
Mzee wangu huwa haongei wala kusema kitu ambacho hajaulizwa. Maana kila alichokuwa ananisimulia, nashangaa kuona ni kipya kwangu.

Kuna siku aliniambia "Bila kupitia mambo uliyopitia, kuna vitu usingevitilia maanani hata ningekuambia, wakati sahihi ni sasa"
 
Pamoja sana chief.
 
Kwa 100% alikuwa sahihi nyumba ni Mama
 
Mazingira ya kuongea unapaswa kuyatengeneza wewe maana we ndio unaehitaji kujifunza
 
Wooooh, somo zuri, kwa kweli umetufundisha, I wish mamangu angekuwepo leo....ningekaa nikaongea nae mawili matatu kama ulivyokuwa unaonagea na mshua wako but ndio hivyo hayupo......[emoji24][emoji24]
POLE SANA MKUU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…