Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Muda unazid kwenda kiongoz
Hizi ni picha mbili zinaonesha mahesabiano kati yangu na yule jamaa mnunuzi wa matikiti. Picha ya kwanza palipozungushiwa na bluu hiyo ni bei alafu kushuka chini ni idadi. Mfano matikiti ya yeye kuyanunua kwa elfu mbili yalikuwa manne tu.

Picha ya pili palipozungushiwa na kijani ni hela ambayo aliyotakiwa anipe kulingana na mahesabu. Ilikuwa 318400 (haikufika hata laki 3 na 40)

View attachment 1129113View attachment 1129119
 
Ngoja amalize story ndugu Conclusion kama hizo baadae ww huon utamu wa story na somo mtu analoweza kulipata.
Story nzuri ila ya uongo...huyu mchizi story zake za nyuma alishasoma tuition kwa mudy mchikichini na kasoma azania kama sijakosea hapo hapo leo hii alikuwa hapajui dar...all in all muandishi mzuri...big up broda
 
Story nzuri ila ya uongo...huyu mchizi story zake za nyuma alishasoma tuition kwa mudy mchikichini na kasoma azania kama sijakosea hapo hapo leo hii alikuwa hapajui dar...all in all muandishi mzuri...big up broda
Vyote vyote mim nimekubali jamaa anizungushe tu wikendi nzima...
Story ni tamu kinouma weekend yangu jamaa kaishika
 
Sehemu ya 8:


.... Tofauti na wengi wanafikiria, leo hii ukiniuliza shujaa wangu ni nani katika dunia hii,au ni nani namkubali sana katika ulimwengu huu, kwa kujivunia kabisa nitasema "BABA YANGU" . Huko mbele nitakwambia kwanini au hata wewe utagundua sababu.

Msimu wa kilimo ulipofika, sikuwa na hela ya kutosha kusema iniwezeshe kulima eneo kubwa sana. Nilifanya ushirikiano na jamaa mwingine mmoja, kwa pamoja tukafanikisha kulima heka tano za mbaazi. Shamba tulipata eneo moja lipo manispaa ya Songea, linaitwa Mlilayoyo. Tuliweka juhudi zote na usimamizi wa hali ya juu. Zao lilistawi vizuri sana. Naweza sema kati ya watu wote tuliokuwa tumelima maeneo ya pale, mimi na jamaa ndio tulikuwa na matokeo mazuri. Nakumbuka wakati tunaanza kilimo, bei ya mbaazi ilikuwa juu na nzuri. Kilo moja kuna sehemu ilikuwa inafika hadi 2500.

Msimu wa mavuno wakati unakaribia, ndio zikaja zile tetesi za kushuka kwa mbaazi. Tetesi zikawa kweli, soko likapotea. Ikafika kipindi kisado kinauzwa shillingi 500. Tukashauriana na jamaa tusivune, tusubirie hadi soko likae vizuri kwanza. Siku zikaenda, soko halikai sawa, mpaka mbaazi zetu zikakutana na msimu mpya wa kilimo. Gharama ya kuzivuna ilikuwa kubwa kuliko hata hela ambayo ingepatikana baada ya kuuza, achilia mbali gharama za kuendesha shamba mpaka kufikia hapo.

Mwenye shamba lake anatuuliza, tunampango gani msimu ujao? Tunalikodi tena shamba lake au la? Kama hatukodi, basi tuvune mbaazi tumuachie ardhi yake. Mshirika wangu ananiuliza, tunafanyaje? Nikamwambia me sina cha kufanya , we amua chochote utakachoona nakuachia shamba lote, siwezi kuingia tena gharama za kuvuna. Jamaa nikatemana nae kwa mtindo huo. Nikarudi ghetto pale moonlight.

Kwavile hela niliingiza zote kwenye kilimo, nikawa nimefulia tena. Hapo nilipata somo kuwa kama bajeti ya unachotaka kufanya ni laki 3,alaf na wewe una laki 3 hiyo hiyo, acha. Tulia kwanza mpaka upate hela ya ziada walau mara mbili ya hiyo au hata nusu yake, vinginevyo utakuja kuona watu wanakuchawia huko mbeleni.

Nilianza upya vibarua, hapo nipo choka mbaya. Baada ya kudunduliza na kupata hela kadhaa, sikutaka kujiuliza mara mbili wala kuzurura sana mitaani maana naweza nikakutana na mtu mwingine akanipa fursa. Nikaamua kurudi nyumbani.


* ** ** ** ****

Nilifika nyumbani majira ya usiku. Kabla sijaingia kwenye himaya ya nyumbani kabisa, nilipaangalia kwa muda mrefu sana. Kwa muonekano palikuwa panavutia na maisha hayakuwa mabaya. Nikagonga mlango baada ya kuvuka fensi ya maua na geti kubwa la mbao. Baba ndio alifungua mlango, alivyoniona akaniambia karibu. Yani hakuonesha kama ameshangaa, amefurahi au kushtuka, kiufupi alichukulia kama nilienda dukani sasa ndio narudi.

Asubuhi ya siku hiyo, naskia mama alijichoma na msumali wakati anapalilia maua pale nyumbani, toka hapo hakuweza kukanyaga vizuri chini, alikuwa anachechemea, ila aliponiona nahisi alipata ganzi ya mguu, maana sio kunikumbatia tu, bali pamoja na ndevu zangu alinibeba. Nikapata faraja niliyoitaka, faza nikampotezea. Pale mezani alikuwa ndio anamtengea mzee chai na maandazi (siku zote baba hupenda kunywa chai usiku hata awe ameshiba vipi). Basi ile chai akanipa mimi, Mzee anauliza vipi mbona unagawa chai yangu? Mama hana hata habari nae. Mara kaniletea hiki, mara kile, ilimradi ukarimu. Nilipoenda kulala, kila mara anakuja kunichungulia. Sina uhakika kama yeye alilala usiku ule.

Asubuhi ndio tuliweza kuongea vizuri kama familia. Hapo mama ameshawaambia ndugu zangu wote kuwa nimerudi. Baada ya chai ndio niliweza kukaa na kuongea na mzee. Kitu cha kwanza kuniuliza "Umefata ada?". Nikamwangalia kwa mshangao, ila kilichonishangaza zaidi nilipogundua kuwa hakuwahi kuwaambia nyumbani kuwa tulikutana Madaba, Songea. Ilo lilinishangaza.

Ila aliniambia, "Ulitaka nimwambie mama yako kuwa baada ya kupotea miaka mingi tulikutana ukiwa kibarua ambae maisha bado yamekupiga? Au baada ya miaka mingi kutoonekana, tumeonana ila bado ukaniomba hela? . Nilijua hutorudi ndio maana sikumwambia chochote mama yako kwa kipindi kile, na pia sitoshangaa kama utaondoka tena. Najua tulipoachana maisha yako yaliendelea kuwa magumu na ndio maana hata hela niliyokutumia wala hukunirudishia. Nikajiuliza hela gani alinitumia huyu mzee? Nahisi alijua ninachowaza, akaniambia siku tuliyoachana alichukua namba yangu toka kwa wale vibarua niliokuwa nafanya nao, na alipoona imepita zaidi ya miezi 6 sijaonekana nyumbani alinitumia laki 3 kwenye simu. Nikakumbuka kuna siku iliingia hela, nikajua mtu kakosea kutuma, nikaitoa kwa wakala alaf nikakausha. Mtumaji nae hakunicheki tena. Niliona aibu kichizi.


Baba akaniambia "Ikitokea leo hii Mama yako aseme nyie wote 7 sio wanangu, nitakubaliana nae kwa hao 6 wengine lakini wewe nina uhakika wa asilimia zote ni mwanangu. Mimi na wewe ni mapacha tuliozaliwa katika miaka tofauti, kwa kifupi ww ni mimi". Maneno ya mzee yalinigusa sana kwa mbali machozi yakawa yananilenga hivi. Faza akaniambia "Kama unalia nenda jikoni kwa mama yako" . Mzee wangu kauzu kichizi yani,kwanza toka nakua sijawahi kumuona anasikitika. Nikabaki nashangaa tu maneno yake. Akazidi kuniambia " Tofauti ya ww na mimi, ni kwamba mimi nilirudi baada ya safari yangu kuelekea mwishoni,nilirudi nikiwa shujaa. Wewe ni shujaa lakini safari yako haijaisha,umerudi ikiwa kati"

Kuna mengi sana hatuyajui kuhusu wazazi wetu ambayo yangetufunza na kutujenga, hii inatokana na kwamba tuko bize sana kiasi tunakosa muda wa kuzungumza nao. Misukosuko tunayokutana nayo leo hii, majibu yote yapo kwenye maisha waliyopitia wazazi wetu. Tunatafutaga majibu, lakini majibu sahihi yapo tulipotoka. Baba yangu ni Shujaa wangu,Mimi ni Baba yangu,na Baba yangu ni Mimi, unajua kwanini? Ni kutokana na stori fupi ya safari ya maisha yake aliyonisimulia.


* * * * * *

Kwa ufupi tu ilikuwa hivi. Anasema "Sikuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa darasani, shule niliishia elimu ya msingi hata mtihani wa mwisho sikufanya, nilifukuzwa kwa kosa la kuchoma ofisi ya walimu. Tokea hapo nilikuwa naonekana kama mtoto mtukutu nyumbani, babu yako aliniwekea zamu ya kuchunga kila siku, alaf nyumbani sikuwa napewa upendeleo wowote. Kuna siku nilienda kuchunga,jioni nikarudisha ng'ombe ila nikasepa na mbuzi wote. Nikauza na kufanya mtaji. Heri yako unaondoka nyumbani umepewa hela, tena tukijua kuwa utaondoka. Sijui msoto uliopitia ww, lakini msoto niliopitia mimi baba yako ndani ya miaka minne ya mwanzo nadhani ww ungekufa. Ndani ya hiyo miaka minne ya mwanzo kuna siku niliamua kabisa kurudi kwa babu yako nikaombe msamaha, nilifika mpaka pale, nikaiangalia sana nyumba ila nikaona siwezi kurudi nikiwa hivi, nikageuza na kuondoka. Ndio maana sikuile tuliyokutana Songea, nilijisemea kimoyo moyo, kama huyu ni mwanangu hatorudi nyumbani.

Tokea ile siku niliyogeuza, nilijituma sana kiasi kwamba siku niliyorudi nyumbani, nilirudi na idadi ile ile ya mifugo niliyoondoka nayo ila badala ya mbuzi nilirudi na ng'ombe. Ila pamoja na hayo babu yako aligoma kunisamehe hadi kikafanyika kikao na wazee wa kijiji, ndio nikasamehewa,tena baada ya kuchapwa bakora pamoja utu uzima wangu.

Aliendelea kunisimulia vitu vingi sana, hapo ndio nikajua nilidhani nimesota na kupitia tabu nyingi sana, kumbe ningezifananisha na za mzee, basi zangu zingekuwa ni utangulizi tu. Mgodini niliposhindwa kwenda, yeye alishaenda na alishawahi kufukiwa hadi na kifusi. Baba yangu akitembea huwa anachehemea,mguu mmoja ni kama mfupi. Ananiambia ule ulishavunjika mara mbili kutokana na mbilinge za migodini.

Tokea siku hiyo, kila nnapopitia ugumu wowote, lazima nijiangalie kwenye kioo. Baba yangu ni kioo changu.

* ** * * ****

Kurudi kwangu kulirudisha furaha sana nyumbani. Usiku kabla ya kulala, mshua aliniuliza "Una watoto wa ngapi mpaka sasa? Nikamjibu mmoja wa kiume. Akasema namuhitaji, fanya mpango aje hapa nyumbani.

Najua kuna wadau watashangaa kuona nimesema nina mtoto mmoja wa kiume, wakati katika stori yote sijawahi kuongelea ili swala. Katika hii stori ya safari yangu, nimegusa baadhi ya matukio ya kwenye maisha yangu ila sio yote. Na sijagusia mapenzi kwasababu yamenitesa kichizi, nadhani mwanaume akiwa hana hela mwenendo wake wa mapenzi unajilikana tu,mapenzi yanatesa sana Me kuliko Ke. Kuna msemo mmoja nimeuona juzi kuwa "Mwanaume kama huna hela, kazi ya kulinda mahusiano yako muachie Mungu" hii ni kweli kwa asilimia zote. Kwa ufupi kwenye hii safari yangu, mtoto ninae tena wa kiume.


Nikafanya mpango na taratibu zote, nikapewa yule mtoto. Sasa hivi anaishi na babu yake.

Siku ambayo mtoto alifika pale nyumbani, kesho yake mzee aliniita tukawa na mazungumzo ya hapa na pale. Kisha akatoa bahasha na kunikabidhi, kuhesabu ni milioni mbili. Nikamuuliza za nini. Akasema "Babu yako alinipokea baada ya kufanya kikao na wazee kisha nikachapwa bakora,nimekupokea nyumbani ila sitokuchapa...Safari yako bado haijaisha, nenda kapambane". Nilimwangalia yule mzee sikummaliza.

Wiki moja badae nilikuwa ndani ya bus naelekea Songea. Nikarudi rasmi kwenye kilimo. Safari hii nikalima tangawizi..

Nitarudi kukwambia jambo zuri lililotokea. Katika maisha,Baraka za wazazi ni kila kitu.

....

Analyse #Baharia wa nchi kavu.
 
Story nzuri ila ya uongo...huyu mchizi story zake za nyuma alishasoma tuition kwa mudy mchikichini na kasoma azania kama sijakosea hapo hapo leo hii alikuwa hapajui dar...all in all muandishi mzuri...big up broda
Endelea kuwa na mm chief mpaka mwisho. Hii ni jamii forum. Nilishakutana na mtu aliyepost kuwa ni mkurugenzi wa kampuni ya maswala ya kilimo. Ila tulivyokutana live ndio nikajua kuwa anatamani kuwa mkurugenzi wa kampuni ya maswala ya kilimo.
 
Somehow ulikosea kukataa school,ungeenda halafu ukifika unabadil combination juu kwa juu huko shuleni.
Kuna mjomba wangu mmoja alifaulu kwenda form one miaka ya 90,akaanza form one akisomeshwa kwa tabu na bibi,alipofika form 3 akaanza kugoma shule,huku akidanganya kudaiwa hela kibao shuleni ,bibi kwa tabu akawa anampatia anaenda kula Bata na marafiki zake pamoja na mademu zao.Walipofika form 4 wakasimamishwa shule yeye na group lake lote,wakaambiwa waje kufanya mtihan wa mwisho tu.Ulipofika muda wa mitihan akawa anapelekwa shule na tax na dada yake,ila dada yake akawa anamwambia fulan utakuja juta kwa hili.Akamaliza lakin alifel,leo hii yapata miaka 16,amepigika anajuta hana hamu.Kutwa kutupiga mizinga wajomba na kulalamiki hatumsaidii.
Na ndivo inavokuwa wabongo hatutak kuwajibika kwa makosa yetu ya nyuma. Siku zote tu anatafuta jumba bovu.
 
Endelea kuwa na mm chief mpaka mwisho. Hii ni jamii forum. Nilishakutana na mtu aliyepost kuwa ni mkurugenzi wa kampuni ya maswala ya kilimo. Ila tulivyokutana live ndio nikajua kuwa anatamani kuwa mkurugenzi wa kampuni ya maswala ya kilimo.

Nipo na wewe chief ndio maana ninaifuatilia kwa ukaribu sana, matter of fact nimeis subscribe kabisa, kuna mafunzo mengi, na nikavuyiwa kusoma uzi zako nyingine big up
 
Back
Top Bottom