Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

.. Katika ile Million mbili aliyonipa Mzee, miliona 1.7 yote niliweka kwenye kilimo. Kuanzia kukodi mashamba, kuyaandaa, mbegu n.k. Hiyo laki 3 iliyobaki ndio ilikuwa inanisogeza. Tangawizi nilipanda sehemu moja kule Madaba, Songea inaitwa Balali (ni milimani huko ndani ndani) . Nilipovuna na kuuza, nilipata faida ya milioni 1.5 (baada ya kutoa ile 1.7 niliyowekeza). Toka nianze kufanya biashara, hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza napata faida toka nianze hustling.

Nikaamua kurudi tena nyumbani kwa Wazee. Nilipokelewa vizuri tu. Kesho yake nikaongea sana na Mzee akitaka kujua maendeleo yangu, nikamuelezea hali halisi. Akatikisa kichwa kukuonesha amependezwa na matokeo. Ile siku ambayo alinikabidhi milioni mbili, ilikuwa makubaliano kwamba mambo yakikaa sawa nimrudishie. Kwahiyo baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamkabidhi bahasha ila hakuangaika kuigusa, aliuliza tu kuna nini. Nikamuelezea. Akatabasam tu, alaf akaniambia "Niliposema unirudishie mambo yakikaa sawa, lengo langu ilikuwa ni kukufanya usisahau ulipozitoa ili ikupe motisha ya kuzitumia vizuri, na uzee huu ukinipa milioni mbili napeleka wapi?

Nilimwangalia sana yule mzee ila sikummaliza. Mazungumzo yaliisha.

Baada ya wiki mbili nikaondoka nyumbani nikiwa na ile milioni mbili, pamoja na ile ambayo ilikuwa faida, nikajisemea moyoni "Safari yangu bado haijafika mwisho, ntarudi nyumbani nikiwa mshindi"

Pamoja na kupata faida kwenye tangawizi, ila sikutaka kuendelea nayo maana ilinisumbua pia mpaka kuja kufikia mavuno. Niliamua kuwekeza ile hela kwenye kitu tofauti kabisa na kilimo. Mungu ni mwema mambo yameenda vizuri sana. Badala ya kurudi nyumbani kishujaa, nikaamua kuwa natuma nyumbani msg za kishujaa. Kila mwisho wa mwezi huwa nawatumia Baba na Mama laki mbili kila mmoja kwenye account zao za simu. December 2018 niliwatumia mapema sana,Baba alinipigia simu "Christmas jitahidi huwe hapa nyumbani" .

Nikaenda.

Mazungumzo ya hapa na pale,Mzee akaniambia " Nashkuru kwa unavyotuhudumia mimi na Mama yako,yawezekana hujui uzito wa unachokifanya ila ni kikubwa sana. Ila ningependa kukwambia kitu kimoja,mwangalie sana Mama yako. Vitu vyote ambavyo nimefanya mimi kama baba yako,au magumu niliyopitiaga,yote ilikuwa ni kumtengenezea mazingira mazuri mama yako na wanae ambao ni nyinyi,kama unataka kunipa furaha Baba yako,basi mwangalie sana Mama yako. Furaha yake ni yangu. Nina uwezo wa kuvumilia matatizo 100 yanayonisumbua mimi,ila sitoweza kuvumilia tatizo moja linalomsumbua Mama yako. Kwa hali ya uchumi niliyonayo ningeweza kuwa na wanawake wengine,ila siku zote nilimuahidi sitofanya kitu cha kumuumiza,na kamwe sitoweza".

Nilimwangalia sana Mzee wangu,nikaona kumbe nina mzee jembe kiasi hiki? Ikabidi kama kijana nianze kuongea maneno ya kiustaarabu na mimi. Nikamwambia "Nashkuru Mzee kwa maneno yako uliyoongea,yamenigusa sana. Nitawaangalia siku zote wewe na Mama kwa kadiri niwezavyo. Maana hata ningesema nijaribu kuwarudishia fadhila zenu inagenichukua miaka mingi sana" Kabla hata sijamaliza Mzee akacheka. Ikabidi nimwangalie kwa mshangao. Akasema "Sio tu ungejaribu,ukitaka jaribu alafu hiyo miaka mingi unayosema ungetumia,ongezea na mingine 100 ila hutoweza kulipa fadhila yoyote aliyokufanyia mtu,achilia mbali sisi Wazazi wako. Maana hujui walipoteza nini katika kukufanyia wewe fadhila.Kitu pekee unachoweza kufanya ni kulipa wema kwa wema."....akaendelea " Nenda jikoni kwa Mama ako naona ushaanza kutia simanzi hapa,yeye ndio anaweza kuvumilia mazungumzo ya aina hiyo".

Kwa siku hiyo mazungumzo yaliishia hapo,tuliendelea kesho yake. Mzee wangu siku zote hapendi mtu anayeongea kinyonge nyonge au kutia huruma.

Turudi nyuma kidogo:

MWISHONI MWA MWAKA 2017

Hii ni siku ambayo mambo yangu yalienda ovyo sana. Ni siku ambayo niliamua rasmi kumsusia yule partner wangu shamba la Mbaazi. Hapo nilikuwa nimeshasota sana kwenye kilimo na ujasiliamali. Nishasota kitaa bila kazi baada ya kumaliza chuo. Dunia yote naona ipo kinyume na mimi. Nishasikiliza sana wale motivational speakers wote unaowajua ili kutafuta tumaini ila naambualia patupu. Ndipo nilipoamua kumpigia simu Baba. Naongea nae huku nikiwa na hasira inayotokana na ugumu wa mambo plus huzuni pia. Mzee akaniambia "Kama huwezi kuongea bila kulia, basi mpigie simu Mama ako, au la, kata simu, lia kwanza, ukimaliza nipigie tuongee" Mzee wangu ni shujaa wangu aisee. Nikajikaza tukaongea kidogo, akaniambia fanya mpango usafiri uje tuongee vizuri.

Nikawatembelea. Siku moja baada ya kufika mida ya jioni akaniita tuongee. Mama akatutengea chai, mshua akamimina kwenye kikombe kimoja alafu akamuita Mama. "Huyu mpe juice" Nikawahi kusema, na baridi hii ningependa chai zaidi kuliko juice. Baba akaniambia "Dogo ukishaoa utakuwa huru kutoa mapendekezo ya chakula unachotaka, kabla ya hapo chukua kilichopo". Alaf akamgeukia Mama " Mletee juice". Nikawa mpole. Najua alifanya vile kwasababu siku ambayo tuliongelea habari za mwanangu aliniuliza naoa lini, nikamwambia bado sana.

Anyway, nikakubali juice na kikao kikaendelea. Akaniambia najua una maswaibu yamekukuta, ila kabla hujaniambia na kuanza kutia huruma, ngoja nikuelezee ya kwangu. Akaanza kunipa story ya harakati alizopitia na ndizo ambazo nilikuwa nawasimulia tangia story inaanza Asilimia kubwa ya niliyowasimulia ni mambo aliyopitia Mzee wangu. Kati ya yote, yangu ni asilimia kama 5 tu, na hasa yanayohusu kilimo.

Alipomaliza kunisimulia, nilibaki namshangao. Nikamuuliza "Mbona hujawahi kunisimulia mimi au ndugu zangu wengine?" Akanijibu "Ningekusimulia sa ngapi na ww muda huna,pia naskia role model wako ni Ben Carson? Ambae unajua historia yake tokea anazaliwa hadi anakuwa Neuro Surgeon? " Nikakausha. Akaniuliza unajua leo tarehe ngapi? Nikajbu 8. Hapo ndio nikakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa ya Mama. Nikajishangaa imekuwaje nikaisahau wakati miaka yote huwa naikumbuka? Sikuongea kitu. Akaniambia kuna maswahibu yamekukuta mpaka yamepelekeaa ww kuwa hapa, unaweza kuniambia?

Nikamwambia hapana, nipo sawa sasa. Nitamwambia nini wakati aliyopitia yeye ni kama bahari nzima, na yangu ni tone tu? Alafu pia nilijaribu kuielewa psychology ya Mzee kwann alianza kunisimulia story yake kabla hata hajasikiliza yangu.

Alivyoona sina cha kuongea akaniruhusu niondoke. Wakati natoka nikajigonga kwenye ncha ya kiti. Sikutaka kugeuka nyuma,ila nikamsikia anasema "Utapewa pole jikoni,ila najua ukifika mjini utapost kuwa umejigonga kwenye kiti" Alaf akaangua kicheko.




*** *** *** *** *** ***

Siku moja kabla ya kurudi mjini, Baba ndio alinipatia zile milioni mbili ambazo niliwekeza kwenye tangawizi. Japo sikumuelezea matatizo yangu, ila najua aliyahisi.

Aliniambia yafuataya "Dunia ya leo kila unayemuona anamatatizo yake kiasi kwamba anakosa hata muda wa kukuonea huruma ww. Hivyo unapoongea na watu tegemea sana msaada wao,ila usitegmee huruma yao.

Akaendelea "Huwezi kurudisha fadhila alizokutendea mtu,ila unachaweza kufanya ni kulipiza wema kwa wema.

Akamalizia "Najua utakuwa bize sana,lakini mimi na Mama yako kwa umri tulio nao hatuwezi tena kuongea na simu zaidi hata ya nusu saa,dakika 10 zako kwa siku ukitupigia simu zinatutosha".


Maneno ya mzee yalinigusa sana.

Tukaishia hapo.

Kesho yake niliongea na Mama kiasi,nikawa nagusia kuwa Baba kauzu sana. Mama akaniambia "Toka ujana wake yupo hivyo na ndio njia iliyosababisha akanipata mimi,ni mchekeshaji aliye serious"

Nikajikuta natamani kuijua story ya jinsi Baba na Mama walivyokutana. Kabla sijaondoka nikajaribu kumgusia Mzee ilo swala ,akajibu " Unataka darasa la kutongoza? We ukimpata nipe namba yake,nitamaliza kila kitu" baada ya kuongea hivyo akacheka saaana.


Aisee nilikuwa namiss vitu vingi sana toka kwa Wazazi.

My father,my hero

*** *** *** *** *** ***

Nimejaribu kushare na nyie story ya Baba yangu kwavile najua leo hii kuna mtu anapitia msoto,kuna mtu hana muda wa kuzungumza na wazee wake,anakaribia kukata tamaa,anasubiria miaka 3 ijayo ndio aweze kuongea na wazazi wake n.k

Ili niweze kuwagusa hao wote,imebidi niilete kwa mtindo wa story,kinyume na hapo kuna wengine wasingepata huu ujumbe japokuwa wanauhitaji.

Wazee wetu wanavitu vingi sana ambavyo vingekuwa funzo na mwangaza mkubwa kwetu, ila hatuvijui maana hatupati muda nao. Pata muda na wazee wako. Ongea nao kadri unavyopata muda, usisubiri mambo yawe tight kama ilivyokuwa kwangu ndio ukaongee nao.

Tunayopitia sasa, walishapitia. THE BEST MOTIVATION SPEAKERS ARE OUR PARENTS. THEIR LIFE IS OUR DICTIONARY TRUST ME GUYS.

Najuwa kuna madini mzee hajaniambia yote. Kwa jinsi nilivyokaribu nae siku hizi, ntajua kila kitu.

Mimi ni Baba yangu, na Baba yangu ni Mimi.

Naitwa Analyse ,na hiyo ndio ilikuwa safari yangu na Baba yangu.


See You.

#Baharia wa Nchi Kavu.
Mkuu hongera sana

Vipi, siku hizi bado unaletewa juice ukitaka chai au unapata unachotaka

Umemaliza story yako lakini bado umetuachia maswali mengi

Pia umwongelea mambo ya chuo, japo hujatusimulia kuhusu kwenda chuo au nimekuelewa vibaya

Kwamba story yote uliyotusimulia ni 5% inayokuhusu wewe, ina maana mzee wako ndio aliibiwa furushi mbezi, aliyejifanya fundi bomba, alikwenda kwenye madini Msumbiji, alipigwa hela zake alipokwenda kusaka rupia? n.k

All in all hongera kwa mapambano. Lakini hatuwezi kuwadharau Motivational Speaker kwani hata wewe hapa ume motivate watu japo sio mzazi wao
 
Hapa ndipo huwa nawalaumu wanawake wote niliowahi kuwa nao.

Yaani walishindwa kunisumbua hadi niiende kwa "pyschologist" kama mtoa comment.

Hii hali hutokeaje mzee baba....unaugua ghafla au unazimia?
Hpn nlshndwa kufnya kazi zangu

Hivi wewe unasalitiwa , kesho ndo harusi

What the f*ck

Unaujua uchungu wake
 
Kabisa mshua wa analyse

Anahtaji zawadi

Zawadi kubwa sana

Siku ya wababa ya leo , naiazimisha kwa baba yake analyse na kwa baba yangu

Advance nakumbuka nlsoma shule tatu

Primary shule tano

nlkua kivuruge sana , ila mzee hakuwahi nikatia tamaa

Teh ..


Heshima kwenu wadingi ...


Leo na mtoto anaitwa theodore ...

Nakumbuka huu msemo pia wa mama" mwanangu utakuja kuwa na watoto

Teh ...

Juzi kaiba penseli za wenzake wote

Kesi bado sijaimaliza
Msalimie Theo.
AHAHAHAHAHHAHAHAHAHAHHAHA kajua kunivunja mbavu!n
nimewaza amezikusanyaje zote !dah!
kajua kunitengenezea siku mwanangu!
 
pale kwenye moto uliopeperuka na jani ukuwasha eneo kubwa umenifurahisha sana kwa hilo janga🙂,,, yaani hayo masaibu sie panya alikimbia na moto kwenda kwenye ghala la jirani......siisahau hii siku kwa kipigo...duuu
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂 mbona unanishambulia hivo?
Wewe ndo unasema hayo yeye amesema alipewa hela ya chai!
Jifunze kubalance👇👇👇👇👇👇View attachment 1129578

Duh!!! Post ipi ati u shoboan adi nilisahau ungekewa wako.. kweli Magu karudisha heshima ya pesa nchini..

Shoboan sasa tunajua heshima ya pesa na umekuwa mkimya fulani kwa muda.. wengine ni kama mfano tuendelee kujua kutotumia data tusipohiitaji.. tudakue jobu au kwa majirani.
jifunze kusoma na kuelewa... ulidakia tu nawe uwe umeandika ha ha haaa... na kufikiria nje ya boksi.. mimi huwa narudi

Jionee aibu na kukaa kimya ni.... ukifunzwa sikiliza..

Kuna Mzee mmoja ndio alinionea huruma akaninunilia chai na kunipa nauli ya kunifikisha ubungo, maana jamaa aliyetarajia kunipokea ilibidi nikutane nae ubungo.


aliandika hayo juu

ukaandika haya... nani shoboan.. umechemka embu jiepue kwanza
muda utaisha tena 11 hiyooo


Hiyo sehemu ya kwanza umesema hela uliibiwa mpaka mzee kesho alikusaidia hela ya chai na nauli!

Halafu mwishoni unamalizia kama baada ya kufika ubungo ulinunua vocha umpigie huyo ndugu yako! Hela ulitoa wapi mkuu?
 
.... Ikabidi nianze kufanya kazi kwa malengo ya kusaka nauli na hela ya kuanzia. Nikafanya sana vibarua tofauti tofauti, kwa maeneo tofauti tofauti. Kipindi hicho chote hakuna mtu yoyote ninayemuamini pale Dar, kila mtu namuona mwizi. Sasa kuna kipindi fulani nilikuwa nafanya kibarua cha ujenzi maeneo fulani kule kibaha. Wakati natoka mishe narudi ghetto (nilikuwa nalala kwa fundi mmoja ambae alikuwa bachela),njiani nikakuta lundo la watu wametengeneza umbo la duara. Nikasogea nione nn kinaendelea. Nakuta jamaa wanachezesha nyoka, mara waseme nyoka anawika, mara anapiga mluzi. Kila nikisubiria awike hawiki, mluzi hapigi. Nikasema ngoja nisepe. Yule mchezeshaji nae ghafla akasema "Hiki ninachoenda kukifanya hapa, mchawi hawezi kukaa lazima aondoke" moyo ukalia pa! Nikaona hapa nikiondoka nitaonekana mchawi, ikabidi niendelee kubaki. Huyo nyoka bora angewika basi, hawiki. Mpaka kigiza kinataka kuingia. Wale jamaa wahuni sana, ukiwa na wasi wasi wanakujua. Wakati naondoka ghafla mmoja akaja, akachota mchanga ile sehemu niliyotoa mguu, alafu akataka kuuweka kwenye kikapu huku akisema "Nimmalize?" Kuna washenzi wengine wakajifanya kuniombea msamaha, kumbe lao moja.

Kiongozi wao akaendelea kusema. Kijana umekanyaga sehemu mbaya sana, nisipokusaidia unapotea mazima. NIKAPANIKI. Jamaa akatoa amri, hebu mpelekeni kilingeni mumsaidie. Wakanizungusha sehemu waliyopaki gari lao eti wanaenda kunifanyia dawa. Kufika kule wakanitaitisha, wakanisachi hadi kwenye viatu. Sema waliambulia posho ya siku hiyo tu, maana hela zangu nilikuwa nazificha kwenye ukuta wa chooni kule ghetto kwa jamaa.

Walivyoniachia nikarudi mdogo mdogo hadi kwa jamaa, sema sikumwambia chochote kuhusiana na yaliyonikuta. Siku zikaenda, ujenzi ukaisha. Nikaondoka kibaha. Hapo malengo yangu ilikuwa nifike Songea, maana yule jamaa aliyenipa habari za dhahabu na migodi kwa ujumla alisema kipindi ambacho anakuwa nje ya migodi huwa anapatikana mkoa ule, hivyo aliniachiaga namba ya simu nikifika nimtafute. Kwa vibarua nilivyoshakuwa nimefanya, hela niliyokuwa nayo ingeweza kunifikisha moja kwa moja hadi Songea, ila sikupenda kufanya hivyo. Badala ya kupanda mabasi yaendayo kule, me nikapanda bus lililonifikisha sehemu moja wanaita Mafinga. Lengo la kwenda Mafinga, ni kwasababu wakati nasoma, kuna wadau wazawa wa kule walikuwa wananipa story za biashara za mbao na jinsi zilivyokuwa na hela.

Nilifika Mafinga jioni sana, inaelekea usiku. Kitu kimoja ninachokipenda kwa upande wa mikoani, jamaa ni wasikivu, pia wakiona mtu ni mgeni basi wanamsaidia tofauti na Dar. Sikutaka niingie kichwa kichwa kwenye biashara nisiyoijua, alaf pia baada ya kupata maelezo ya hapa na pale nikagundua mtaji unaohitajika uwe wa kutosha. Nikaachana na biashara ya uuzaji mbao, ila nikaanza vibarua vya upangaji wa mbao pamoja na kuzitreat. Hapa ndio niliamini ule msema wa akili mjini, nguvu peleka bushi. Hii kazi ni ngumu. Maana ndani ya wiki moja nilikuwa nimechubuka mabega yote mawili, yani pametoka sugu. Mwanzoni kazi ilikuwa poa, ikiisha tunapewa chetu, ukilala hoi.

Kuna siku nilichoka kupita maelezo, kiasi kwamba nilivyojiegesha ile jioni baada ya kupewa posho, nikasinzia mazima pale nilipokuwa. Kilichonishtua ni baridi lilizidi kuwa kali pamoja na sauti za watu. Nikajinyanyua kusogea walipo watu, nikaona jamaa wanapakia mbao kwenye toyo. Akili yangu inawaza hela tu, nikawafata nikijua ni jamaa zangu walau nipate kibarua. Walivyoniona wakashtuka. Kuwahoji naona wanababaika. Nikajua hawa ni wezi tu. Hapo ndio niliona umuhimu wa simu, ningekuwa nayo ningempigia Boss kumpa taarifa.

Wale jamaa wote wakakimbia, akabaki mwenye usafiri tu. Uzuri akatokea masai wa godown la jirani. Akampigia boss. Boss akawaka, sina mteja wa usiku, washikeni wasitoke hao. Alikuja mpaka pale usiku ule ule, mwenye toyo akalazwa polisi, kesho yake akasaidia wakapatikana wale wengine. Tokea siku hiyo boss akanifanya kuwa foreman wake, cheo kikapanda. Niliendelea kukomaa pale hadi ilipofika msimu wa mvua, pale shughuli nyingi za miti huko porini zikasimama, na sisi huku mbao zikapungua. Hela ikapungua pia. Sikuona haja ya kuendelea kuwa foreman sehemu isiyo na hela. Rasmi nikaenda Songea.

***** ***** ***** ***** ***

Sikutaka kupoteza muda sana, hela ambayo nilikuwa nayo ilikuwa ni mwanzo mzuri. Kwavile nilikuwa tayari nina simu, nikampigia yule jamaa, hakawa hapatikani. Usiku hapatikani, asubuhi na mchana hivyo hivyo . NIKAWA MPOLE.

.....

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Chief umenikumbusha mbali sana pole aisee
 
Back
Top Bottom