Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

.. Katika ile Million mbili aliyonipa Mzee, miliona 1.7 yote niliweka kwenye kilimo. Kuanzia kukodi mashamba, kuyaandaa, mbegu n.k. Hiyo laki 3 iliyobaki ndio ilikuwa inanisogeza. Tangawizi nilipanda sehemu moja kule Madaba, Songea inaitwa Balali (ni milimani huko ndani ndani) . Nilipovuna na kuuza, nilipata faida ya milioni 1.5 (baada ya kutoa ile 1.7 niliyowekeza). Toka nianze kufanya biashara, hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza napata faida toka nianze hustling.

Nikaamua kurudi tena nyumbani kwa Wazee. Nilipokelewa vizuri tu. Kesho yake nikaongea sana na Mzee akitaka kujua maendeleo yangu, nikamuelezea hali halisi. Akatikisa kichwa kukuonesha amependezwa na matokeo. Ile siku ambayo alinikabidhi milioni mbili, ilikuwa makubaliano kwamba mambo yakikaa sawa nimrudishie. Kwahiyo baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamkabidhi bahasha ila hakuangaika kuigusa, aliuliza tu kuna nini. Nikamuelezea. Akatabasam tu, alaf akaniambia "Niliposema unirudishie mambo yakikaa sawa, lengo langu ilikuwa ni kukufanya usisahau ulipozitoa ili ikupe motisha ya kuzitumia vizuri, na uzee huu ukinipa milioni mbili napeleka wapi?

Nilimwangalia sana yule mzee ila sikummaliza. Mazungumzo yaliisha.

Baada ya wiki mbili nikaondoka nyumbani nikiwa na ile milioni mbili, pamoja na ile ambayo ilikuwa faida, nikajisemea moyoni "Safari yangu bado haijafika mwisho, ntarudi nyumbani nikiwa mshindi"

Pamoja na kupata faida kwenye tangawizi, ila sikutaka kuendelea nayo maana ilinisumbua pia mpaka kuja kufikia mavuno. Niliamua kuwekeza ile hela kwenye kitu tofauti kabisa na kilimo. Mungu ni mwema mambo yameenda vizuri sana. Badala ya kurudi nyumbani kishujaa, nikaamua kuwa natuma nyumbani msg za kishujaa. Kila mwisho wa mwezi huwa nawatumia Baba na Mama laki mbili kila mmoja kwenye account zao za simu. December 2018 niliwatumia mapema sana,Baba alinipigia simu "Christmas jitahidi huwe hapa nyumbani" .

Nikaenda.

Mazungumzo ya hapa na pale,Mzee akaniambia " Nashkuru kwa unavyotuhudumia mimi na Mama yako,yawezekana hujui uzito wa unachokifanya ila ni kikubwa sana. Ila ningependa kukwambia kitu kimoja,mwangalie sana Mama yako. Vitu vyote ambavyo nimefanya mimi kama baba yako,au magumu niliyopitiaga,yote ilikuwa ni kumtengenezea mazingira mazuri mama yako na wanae ambao ni nyinyi,kama unataka kunipa furaha Baba yako,basi mwangalie sana Mama yako. Furaha yake ni yangu. Nina uwezo wa kuvumilia matatizo 100 yanayonisumbua mimi,ila sitoweza kuvumilia tatizo moja linalomsumbua Mama yako. Kwa hali ya uchumi niliyonayo ningeweza kuwa na wanawake wengine,ila siku zote nilimuahidi sitofanya kitu cha kumuumiza,na kamwe sitoweza".

Nilimwangalia sana Mzee wangu,nikaona kumbe nina mzee jembe kiasi hiki? Ikabidi kama kijana nianze kuongea maneno ya kiustaarabu na mimi. Nikamwambia "Nashkuru Mzee kwa maneno yako uliyoongea,yamenigusa sana. Nitawaangalia siku zote wewe na Mama kwa kadiri niwezavyo. Maana hata ningesema nijaribu kuwarudishia fadhila zenu inagenichukua miaka mingi sana" Kabla hata sijamaliza Mzee akacheka. Ikabidi nimwangalie kwa mshangao. Akasema "Sio tu ungejaribu,ukitaka jaribu alafu hiyo miaka mingi unayosema ungetumia,ongezea na mingine 100 ila hutoweza kulipa fadhila yoyote aliyokufanyia mtu,achilia mbali sisi Wazazi wako. Maana hujui walipoteza nini katika kukufanyia wewe fadhila.Kitu pekee unachoweza kufanya ni kulipa wema kwa wema."....akaendelea " Nenda jikoni kwa Mama ako naona ushaanza kutia simanzi hapa,yeye ndio anaweza kuvumilia mazungumzo ya aina hiyo".

Kwa siku hiyo mazungumzo yaliishia hapo,tuliendelea kesho yake. Mzee wangu siku zote hapendi mtu anayeongea kinyonge nyonge au kutia huruma.

Turudi nyuma kidogo:

MWISHONI MWA MWAKA 2017

Hii ni siku ambayo mambo yangu yalienda ovyo sana. Ni siku ambayo niliamua rasmi kumsusia yule partner wangu shamba la Mbaazi. Hapo nilikuwa nimeshasota sana kwenye kilimo na ujasiliamali. Nishasota kitaa bila kazi baada ya kumaliza chuo. Dunia yote naona ipo kinyume na mimi. Nishasikiliza sana wale motivational speakers wote unaowajua ili kutafuta tumaini ila naambualia patupu. Ndipo nilipoamua kumpigia simu Baba. Naongea nae huku nikiwa na hasira inayotokana na ugumu wa mambo plus huzuni pia. Mzee akaniambia "Kama huwezi kuongea bila kulia, basi mpigie simu Mama ako, au la, kata simu, lia kwanza, ukimaliza nipigie tuongee" Mzee wangu ni shujaa wangu aisee. Nikajikaza tukaongea kidogo, akaniambia fanya mpango usafiri uje tuongee vizuri.

Nikawatembelea. Siku moja baada ya kufika mida ya jioni akaniita tuongee. Mama akatutengea chai, mshua akamimina kwenye kikombe kimoja alafu akamuita Mama. "Huyu mpe juice" Nikawahi kusema, na baridi hii ningependa chai zaidi kuliko juice. Baba akaniambia "Dogo ukishaoa utakuwa huru kutoa mapendekezo ya chakula unachotaka, kabla ya hapo chukua kilichopo". Alaf akamgeukia Mama " Mletee juice". Nikawa mpole. Najua alifanya vile kwasababu siku ambayo tuliongelea habari za mwanangu aliniuliza naoa lini, nikamwambia bado sana.

Anyway, nikakubali juice na kikao kikaendelea. Akaniambia najua una maswaibu yamekukuta, ila kabla hujaniambia na kuanza kutia huruma, ngoja nikuelezee ya kwangu. Akaanza kunipa story ya harakati alizopitia na ndizo ambazo nilikuwa nawasimulia tangia story inaanza Asilimia kubwa ya niliyowasimulia ni mambo aliyopitia Mzee wangu. Kati ya yote, yangu ni asilimia kama 5 tu, na hasa yanayohusu kilimo.

Alipomaliza kunisimulia, nilibaki namshangao. Nikamuuliza "Mbona hujawahi kunisimulia mimi au ndugu zangu wengine?" Akanijibu "Ningekusimulia sa ngapi na ww muda huna,pia naskia role model wako ni Ben Carson? Ambae unajua historia yake tokea anazaliwa hadi anakuwa Neuro Surgeon? " Nikakausha. Akaniuliza unajua leo tarehe ngapi? Nikajbu 8. Hapo ndio nikakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa ya Mama. Nikajishangaa imekuwaje nikaisahau wakati miaka yote huwa naikumbuka? Sikuongea kitu. Akaniambia kuna maswahibu yamekukuta mpaka yamepelekeaa ww kuwa hapa, unaweza kuniambia?

Nikamwambia hapana, nipo sawa sasa. Nitamwambia nini wakati aliyopitia yeye ni kama bahari nzima, na yangu ni tone tu? Alafu pia nilijaribu kuielewa psychology ya Mzee kwann alianza kunisimulia story yake kabla hata hajasikiliza yangu.

Alivyoona sina cha kuongea akaniruhusu niondoke. Wakati natoka nikajigonga kwenye ncha ya kiti. Sikutaka kugeuka nyuma,ila nikamsikia anasema "Utapewa pole jikoni,ila najua ukifika mjini utapost kuwa umejigonga kwenye kiti" Alaf akaangua kicheko.




*** *** *** *** *** ***

Siku moja kabla ya kurudi mjini, Baba ndio alinipatia zile milioni mbili ambazo niliwekeza kwenye tangawizi. Japo sikumuelezea matatizo yangu, ila najua aliyahisi.

Aliniambia yafuataya "Dunia ya leo kila unayemuona anamatatizo yake kiasi kwamba anakosa hata muda wa kukuonea huruma ww. Hivyo unapoongea na watu tegemea sana msaada wao,ila usitegmee huruma yao.

Akaendelea "Huwezi kurudisha fadhila alizokutendea mtu,ila unachaweza kufanya ni kulipiza wema kwa wema.

Akamalizia "Najua utakuwa bize sana,lakini mimi na Mama yako kwa umri tulio nao hatuwezi tena kuongea na simu zaidi hata ya nusu saa,dakika 10 zako kwa siku ukitupigia simu zinatutosha".


Maneno ya mzee yalinigusa sana.

Tukaishia hapo.

Kesho yake niliongea na Mama kiasi,nikawa nagusia kuwa Baba kauzu sana. Mama akaniambia "Toka ujana wake yupo hivyo na ndio njia iliyosababisha akanipata mimi,ni mchekeshaji aliye serious"

Nikajikuta natamani kuijua story ya jinsi Baba na Mama walivyokutana. Kabla sijaondoka nikajaribu kumgusia Mzee ilo swala ,akajibu " Unataka darasa la kutongoza? We ukimpata nipe namba yake,nitamaliza kila kitu" baada ya kuongea hivyo akacheka saaana.


Aisee nilikuwa namiss vitu vingi sana toka kwa Wazazi.

My father,my hero

*** *** *** *** *** ***

Nimejaribu kushare na nyie story ya Baba yangu kwavile najua leo hii kuna mtu anapitia msoto,kuna mtu hana muda wa kuzungumza na wazee wake,anakaribia kukata tamaa,anasubiria miaka 3 ijayo ndio aweze kuongea na wazazi wake n.k

Ili niweze kuwagusa hao wote,imebidi niilete kwa mtindo wa story,kinyume na hapo kuna wengine wasingepata huu ujumbe japokuwa wanauhitaji.

Wazee wetu wanavitu vingi sana ambavyo vingekuwa funzo na mwangaza mkubwa kwetu, ila hatuvijui maana hatupati muda nao. Pata muda na wazee wako. Ongea nao kadri unavyopata muda, usisubiri mambo yawe tight kama ilivyokuwa kwangu ndio ukaongee nao.

Tunayopitia sasa, walishapitia. THE BEST MOTIVATION SPEAKERS ARE OUR PARENTS. THEIR LIFE IS OUR DICTIONARY TRUST ME GUYS.

Najuwa kuna madini mzee hajaniambia yote. Kwa jinsi nilivyokaribu nae siku hizi, ntajua kila kitu.

Mimi ni Baba yangu, na Baba yangu ni Mimi.

Naitwa Analyse ,na hiyo ndio ilikuwa safari yangu na Baba yangu.


See You.

#Baharia wa Nchi Kavu.
Simulizi nzuri sana na yenye kufundisha, asante sana Analyse.Nadhan kwa sasa mambo yako yapo vizuri
 
Ila khaaa pamoja na kulizwa Sana dar bado hukukua kiakili.

Yaani babu wa kijijini aweze kuwapata mjerumani na muisrael na vichaa 2 nanyi mkaamini kabisaaa...

Hivi mnalishwagwa uchawi mshindwe kufikiri??
mkuu hayajakukuta, ni sawa uwe umeingia kuiba kitu sehemu hata akija dogo wa vidudu anakujambisha utatoka mbio. hapo mawazo yote ni hazina ya mjerumani not ufikiri wa sehemu na nani anakupatia hivyo vitu
 
Simulizi nzuri na yenye mafunzo hasa kwa mimi kijana ninayepambana ili nifanikiwe.

Moja ya kitu kikubwa nilicho jifunza ni kutokata tamaa umekutana na changamoto upande wa kilimo bei ya mazao kushuka hadi kukata mtaji, mazao kuoza pamoja na changamoto hizo bado hukukata tamaa hata pale ulipopewa mtaji na mzee mawazo yalikuwa upande wa kilimo na baadae ukapata mafanikio.

Mzee wako anakupenda sana na anajua namna ulivyokuwa ukipambana hongera kwa kupata baba mwenye upendo japo hakujionyesha wazi ili ufahamu kuwa anakupenda.
 
Nimecheka sana Baba anauliza km jamaa ni mwanae. Jibu la mama limeniacha na cheka aswa eti pua duuu
 
.... Hakuna kitu kigumu kama kumngojea mtu ambae hujui yuko wapi au anafanya nini. Kwa wakati ule nilishindwa nifanye nini maana sikuwa na plan B. Ikabidi niendelee kuzuga tu mjini pale. Uzuri wa mikoani sehemu za kujiachia ni chache, nakumbuka ilikuwa ni siku ya nane nane, karibia mji wote wa Songea kuna sehemu huwa wanakutana. Kwavile sikuwa na mishe, ikabidi na mimi nijisogeze kwenye viwanja vya nane nane, sina ili wala lile pia sina plan maalum. Nikazungukia karibu vibanda vyote vya maonesho. Mpaka leo hii naamini kama unaishi Songea alafu kuna mtu unamdai ila anakukwepa au umepoteana na mtu kitambo, we kuwa mvumilivu alafu tegea siku ya nane nane utampata tu. Maana hiyo siku ile natoka tu getini, ghafla namuona yule jamaa wa harakati za migodi. Nilifurahi kichizi, japo mwanzo hakunikumbuka ila baadae kumbukumbu ilirudi tukaanza kuyajenga.

Jamaa ananipa story amekutana na majanga kibao kule, mara ya mwisho kwenda walifanikiwa kupata kajiwe kadogo kadhahabu akiwa na mwenzake Mbongo pamoja na Mzimbabwe. Ila utaratibu wao kule ni kwamba mkiwa katika eneo wote mnatafuta, atakayebahatika kupata, basi mnagawana wote kwavile wote mmehangaika. Sasa kisa chake ni kwamba yule Mzimbabwe ndio aliyepata mali, ila kutokana na tamaa hakutaka kugawana na wengine. Kwa hustling za machimboni zilivyo, ni vigumu sana mtu kufanya kazi mfano masaa mawili alaf akaondoka labda upate mali, ukifanya hivyo wengine wengine watahisi umepata tu. Sasa yule Mzimbabwe ili wengine wasimhisi, ikabidi ampe msala yule Mbongo mwingine. Alipayuka tu "We umemeza nini?" . Naskia ile kauli ilishtua wengi pale, maana njia yao kubwa ya kuficha ni kumeza. Yule mbongo akapaniki, ila mzimbabwe akakaza. Raia wengine wakamtaitisha yule mbongo ili aseme kameza nini. Huyu mshikaji wangu kujaribu kutetea, nae akawekwa kati. Wakabebwa wote. Yule mbongo wa kwanza naskia akalishwa madawa fulani ya asili ambayo yanasababisha kuharisha. Aliharisha sana ikafika hatua akawa analia.

Wadau wengine kila wakichambua kinyesi hawaoni kitu, wanaambizana bado hajanya mali huyu tumpe dawa nyingine, mchizi analia tu. Huyu jamaa yangu nae wakambana aseme mali iko wapi. Akijitetea, hawaelewi. Akatokea Mzambia mmoja na sululu, akafyeka vidole vya jamaa. Hapo na mm ndio nikagundua kumbe mshikaji mkono wa kushoto umebaki na kidole gumba pamoja na cha shahada (viwili tu),muda wote ananisimulia sikumtilia maanani nilikuwa napawaza mgodini tu.

Mshikaji anasema mpaka wale wadau walipokuja kushtuka kuwa yule Mzimbabwe hayupo, ndio wakaelewa atakuwa amewapoteza maboya tu. Jamaa yangu anamalizia kunisimulia kwa kusema alivyofanikiwa kutoka kule hajarudi tena hadi leo na hana mpango wa kurudi. NIKASIZI KIDOGO.

*** *** *** *** *** *** ***

Tulibadilishana namba za simu, tukaachana. Nikarudi ghetto, maana nilikuwa nishabahatika kupata sehem ya kujiegesha eneo fulani wanaliita moonlight, nyumba ya bibi mmoja hivi imechoka kichizi, ila hakuna jinsi, maana hela hakuna.

Ikabidi niwe najichanganya na raia wengine, mara leo nimekata nyasi za fensi vizuri, kesho nimesaidia mafundi ilimradi niingize hela. Napambana ili akiba yangu iongezeke. Nikasogea mashambani na kuanza kulima kama kibarua, fanya sana palizi, mwagilia sana bustani za watu mpaka siku moja nilipokutana na jamaa kutokea Namtumbo,sehemu inaitwa Nambecha, aliyenipa fursa nyingine.

Huyu jamaa akaja na story fulani kuhusu hazina iliyoachwa na Mjerumani miaka hiyo. Jamaa alipa ufafanuzi wa kina kiasi kwamba nikamuelewa, mm nikiwa kama baharia wa nchi kavu napigania kupata ushindi, na ushindi wangu ni mkwanja. Nikasema dili ndio ili. Kwa maelezo ya mshikaji, kati ya mali ambazo zina hela moja wapo ni rupia, mekyuri na pasi. Akasema nikifanikiwa mfano kupata pasi, basi maisha ya msoto yanaisha, kiufupi nasahau shida kabisa. Na kulingana na taarifa alizo nazo, kuna babu mmoja yupo Nyasa, huyo ndio mwenye pasi, tukifanikiwa kumpata huyo na kufanikiwa kuipata hiyo pasi ya mjerumani, tunakuwa na uwezo hata wa kununua nchi.

Nikaona miaka yote nilikuwa wapi? Fursa si ndio hii, ngoja nikaisake pasi ya mjerumani. Kilichonikuta, NILIJUTA.


.......
[emoji3] [emoji3] [emoji2] [emoji2]
Kama nakuona mwanang..
 
Nilizaliwa miaka kadhaa iliyopita. Katika familia ya watoto 7,mimi nilikuwa wa 6.

Kama watoto walivyo, nilikuwa mtundu kiasi ila sio mtukutu. Nakumbuka nikiwa darasa la 5,niliitwa mbele na ticha nikafanye swali la hesabu. Nikafanya swali kwa mbwembwe, nilikuwa nasumbuliwa na mafua, kabla sijaondoka pale mbele nikatoa leso ili nijifute. Wakati naitoa, kibox cha condom kikaanguka, darasa zima full kicheko. Ticha wa mathe ndio ticha wa nidhamu..nikaambiwa nitangulie ofisini.

Nikala bakora zangu za kutosha, kisha ndio nikaombwa maelezo, kila nikijitetea hawanielewi. Ukweli sio kwamba nilikuwa na dem au nilishaanza mapenzi, ni ile tu utoto utoto, unaokota kibox cha condom alaf unakaa nacho uangaliage zile picha. Kesi iliisha baada ya mzazi kuitwa.

Miaka ikakata, siku zikaenda. Darasa la saba mwishoni, wakati natoka kujisomea nikiwa na wenzangu wawili, ghafla tukasikia miguno kwenye darasa moja, kuchungulia tunakuta mlinzi wa shule yupo na muuza ubuyu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]. Jamaa akatukimbiza maana ndio alikuwa
anajiandaa kupiga show alaf tumemtibulia.

Kitoto toto, tunakimbia huku tunacheka, nikaenda kuliparamia lori la mchanga wakati navuka barabara. Nikapelekwa hospital na kushonwa nyuzi 18,maana nilipasuka kichwani na usoni. Nikauguza majeraha, baada ya miezi kadhaa nikapona.

Baada ya kumaliza la saba, wazee wakaona nisisome shule za day, wakaamua kunipeleka seminari huko mkoani Iringa, mbali kabisa na mkoa wangu. Sijawahi ona shule ambazo wako strict kama seminari. Sema siku zikakata pia, wakati nipo kidato cha 3,hata mawazo sijui yalitokea wapi, me na rafiki yangu Shedy tukapanga tuuze nguruwe wa kanisa. Nakumbuka tulivibana vizuri ili visitoe sauti (vitoto viwili),kumbe wakati tunaishia, kuna sister akatuona (aliutambua mzura wangu). Wala hatukupigwa, tuliambiwa tutaje tulipowapeleka ili tusamehewe. Tukataja, wakafatwa. Tukashangaa wik end wazazi wetu wamefika, wakakabidhiwa barua zetu za kufukuzwa shule, tukaambiwa tusepe.

Mshua aliongea sana siku hiyo, njia nzima hadi tunafika home. Kwanza hakuninunulia chochote cha kula njiani, maji nilikunywa kwavile yanatolewa ndani ya bus. Kufika home,ilifanywa mipango nikajiunga na shule fulani ya private ili nimalizie O level. Nikiwa kidato cha 4,me na mdogo wangu ndio tukafanya ule msala wa kumfungia dingi kwa nje,alaf tukala ndizi zote..

Kufupisha,fatisha hii link kusoma kilichotokea maana nilishawahi kuandika hiki kisa:



Nikamaliza form 4,majibu yakatoka. Nakumbuka nilipata 3 ya mwisho mwisho huko. Nilikuwa napenda sana hesabu,ila cha ajabu nilipataga D. Na post zilivyotoka nikapangiwa HKL. Afadhali History,sikuwahi kulipenda somo la Kiswahili wala English,leo hii nikasome vishazi na ngeli shurutia ambazo nilivutwa sana masikio lakini sikuzielewa? Nikampanga faza anipeleke private Advance, akagoma. Msimamo wangu ukabaki me HKL siwezina sitaki. Faza akakausha. Baada ya wiki akaniita, akaniambia kati ya vitu viwili kimoja lazima nikiweze "KUSOMA HKL AU KUJITEGEMEA". Kikao kikaishoa hapo, nikaambiwa nikafikirie.

Nikiwa peke yangu chumbani, nikawa natafakari mavitabu, tamthilia, riwaya, ushairi ntakayoenda kusoma Advance, nikaona ngoma nzito ikiwa Mabala the Farmer kilikuwa kinanitoa jasho. Wiki moja baadae mshua akaniita tena, akanipigia hesabu zote za gharama zinazohitajika kuanzia nitakapoenda shule, alaf akanikabidhi cash pamoja na joining instructions ya shule. Akasema

"Vitu vyote utakavyohitaji kununua vimeandikwa humo na hela hii hapa, shule inafunguliwa tarehe 21,itakapofika siku hiyo nisikuone hapa kwangu, either uende shule au hiyo hela iwe mtaji wako wa kuanzia maisha"

Kikao kikaishia hapo. Ndani naona hapakaliki, nikaenda uwanjani kuangalia mpira ili kupoteza mawazo. Siku kama mbili mbele nikiwa nimekaa na washkaji, zikaanza story kuhus Dar es salaam. Kwamba ukijituma, na kuwa mjanja mjanja unafanikiwa. NIKAPATA WAZO LA KWENDA DAR.

Tarehe 15 /05 nikapanda bus kwenda Dar. Kabla sijatoka toka, Maza aliniuliza kama naenda shule, nikamwambia hapana, nachukua uelekeo mwingine.


Nakumbuka Dar es salaam tuliingia mida ya saa tano usiku. Bus ilisimama nikaona watu wanawahi kushuka, na mimi nikabeba vitu vyangu nikashuka. Kufika chini nauliza hapa ndio ubungo? ( Ndio sehem pekee niliyokuwa naijua) . Jamaa akanijibu "Hapa Mbezi dogo". Nikapaniki. Ikabidi nitafute sehemu nikae chini nitafakari vizuri. Kuna gari ilikuwa imepaki, nikakaa kwa chini, nikijiuliza nafanyaje.

Nilikuja kugundua badae chini ya lile gari kumbe kuna watu ndio sehemu yao ya kulala, na niligundua baada ya kile kifurushi changu nilichoweka chini kutoweka "NILIDATA"

•••••••• •••••••••• •••••••• •••••

Kwenye kile kifurushi ndio kulikuwa na nguo zangu pamoja na hela. Nikajaribu kuulizia, hakuna aliyenijali, naishia kutukanwa tu kuwa nawarushia stimu.

Mpaka kuna kucha, sikuupata mzigo wangu. Kuna Mzee mmoja ndio alinionea huruma akaninunilia chai na kunipa nauli ya kunifikisha ubungo, maana jamaa aliyetarajia kunipokea ilibidi nikutane nae ubungo. Kwavile namba zake nilikuwa nazo kwenye karatasi, niliongea nae kwanza kupitia simu ya yule mzee na kumuelezea kwa ufupi yaliyotokea.

Nikapanda daladala hadi ubungo. Kufika, nikaingia hadi ndani mule, nikaazima simu ya mtu, nikampigia tena jamaa yangu kumwambia kuwa nimefika. Wakati namsubiria, nikajiegesha sehemu.

Nikiwa pale, nilishuhudia tukio ambalo siwezi kuja kulisahau. Mbele yangu kulikuwa na Mwanaume wa makamo, kwa mavazi yake ni kama mchunganji, alikuwa anaongea na simu. Akatokea mtu mwingine kwa nyuma yake amebeba makaratasi kibao,ameyabana kwapani huku akiwa anakunywa maji ya uhai, yalipobaki nusu akaenda na kuyamwaga nyuma ya yule mchungaji, kisha akasubiri. Mchungali alipomaliza kuongea na simu, lile jamaa likamuuliza "Nani aliyekuruhusu kukojoa eneo ili?"

Mchungaji akashangaa, nahisi akumuelewa jamaa, ila alipotaka kuondoka, wakaongezeka wengine. Kuna mmoja akampiga kofi, yule aliyemwaga maji akamuuliza " Yani unakojoa eneo la wazi alafu unakuwa mkali?, Twende nae ofisini" Mchungaji akapaniki, wakamwambia atoe faini au akalale ndani. Mchungaji kujisachi, hela hana, atoe simu ili ampigie ndugu yake, simu hakuna. Mchungaji akalia. Ikabidi waazime simu, akampigia ndugu yake ili aje na hela ya faini.

Japo mchungaji alidata, ila mimi nilidata mara 100 zaidi yake. Ikabidi niweke vocha kwenye simu ya mtu tena, piga sana namba ya mwenyeji wangu ila haipokelewi, mwisho wa siku ikawa haipatikani tena. Kucheki muda,saa moja kasoro usiku. Nikazidi kudata.....



***** ***** ******* ******* ******

Imeendelea post #27

Imeendelea tena post #68


Imeendelea tena post #137


Imeendelea tena post #177


Imeendelea tena post #208


Imeendelea tena post #306


Imeendelea tena na kuisha katika post #486

Mkuu ANALYSER me nataka kujua tu yule mdogo wako mliekula ndizi wote sasa yupo wapi anajishuhulisha na nini ikiwemo naww pia, then tudokeze pia uliijuaje JF
 
Back
Top Bottom