Naja na salam kutoka kwa aedes... hodi jamiiforums!

Naja na salam kutoka kwa aedes... hodi jamiiforums!

Logistics

Member
Joined
May 16, 2014
Posts
56
Reaction score
18
habari zenu mabibi na mabwana, ni imani yangu kuwa mu wa afya 'kiasi' chake, nasema kiasi kwa sababu kuu hasa ya janga ambalo limeikumba taifa kwa sasa... janga hili si lingine bali ni la mdudu mbu, mbu mtembea kwenye mwanga aina ya AEDES..

ndugu zangu, nchi yetu iko kwenye hali tete, ni jukumu letu sote kuchukua tahadhari kubwa sana ili tusiweze kuwapoteza wapendwa wetu na wala tusiongeze idadi ya watu wanaogua gonjwa hili lisilo na dawa...

ugonjwa wa dengue una dalili kuu hizi,

  • homa isiyo ya kawaida yenye nyuzi joto zaidi ya 40..
  • joto la mwili kupanda mpaka kufikia degree 40,
  • mifupa kuuma sana (maumivu ya viungo vya mwili..)
  • misuli ya kichwa kuuma hasa usawa wa macho, fizi kutokwa na damu nk.

ndugu zangu, mbu huyu aina ya aedes anazaliana kiajabu sana, yeye uzao wake uko kwenye maji masafi tu yaliyotuama, iwe ni pembeni ya nyumba yako ama ndani mwako pia, jambo la msingi ni kuwa makini sana na mazalia ya mbu hawa...

nb: tahadhari kubwa sana ichukuliwe, unapohisi dalili zozote za malaria, tafadhali usigeuke daktari na nesi kwa kuanza kujitibu, jambo la msingi ni kuwahi kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini tatizo hasa ni nini, hapo ndipo utapewa dawa kulingana na tatizo ulilonalo..

kumbuka, inapofika mida ya jioni kuanzia saa 11 na kuendelea, mavazi yako makuu tafadhali yawe ni yale yanayoziba sehemu zote za mwili kama mikono, miguu yote nk, kwa dada zetu nao wajiangalie sana.. DENGUE HAIANGALII JINSIA, DINI WALA UMBO LA MTU.

Mwisho kabisa, niwatakie mapambano mema juu ya ugonjwa huu... safisha mazingira yako ujiokoe na dengue..
 
Hawa mbu AEDES (Mbu kanga) mbona tunao na tunawaona miaka nenda miaka rudi, cha kushangaza hawakuwa na maradhi haya ya DENGUE sasa sijui wamepata wapi hawa bacteria? inashangaza sana kwa kweli turudi kwenye ibada
 
Back
Top Bottom