Najaribu kufikiri jinsi magaidi wanne wa Mbowe wangewezaje kukata Miti Dar - Iringa

Najaribu kufikiri jinsi magaidi wanne wa Mbowe wangewezaje kukata Miti Dar - Iringa

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Kwa sababu ni makomandoo huenda wangeweza.

Nakuuliza hivi,
Wangetumia mapanga ya kawaida au mapanga maalumu?

Au wangetumia mashine za kukatia miti?

Je, Mabwana misitu wangewaacha tu?
Au wangekuwa wanakata huku wamevalia mavazi ya mabakamabaka kw a hiyo mabwanaisitu wangewaogopa?

Je, Wangekua wanatumia gari kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine? Maana ni parefu Sana kutoka Dar Hadi moro na kutoka Moro Hadi Iringa.

Je, wangetumia gari binafsi au wangekua wanapanda mabasi na mapanga yao mikononi?

Je, wangetumia siku ngapi kufanya Ugaidi huo wa kukata Miti?

Je, wangekua wanapata muda wa kupata kifungua kinywa na chakula cha mchana na usiku?

Je, kama wangekua wanakata huku wanatembea wangepitaje pale kitonga? Wale nyani wakali wangewaacha salama kweli au kwa vile ni ma skauti wenye mafunzo mazito wangepigana judo na manyani?

Au wangetumia ile bastola yao?

Najiuliuliza hivi kwa nini zoezi la kukata Miti ni kwa njia ya Dar iringa tu?
Kwa nini isiwe pia kwa Dar Arusha,Dar Mtwara,Dar Mwanza?
Kwa nini zoezi liselingeendelea Hadi Mbeya,na Ruvuma?

Lol aisee! Shilingi laki sita Mbowe aliwapunja sana.maana kuna wengine walikua tayari Wana biashara. Zao kupata laki sita kwa mwezi hazikua shida.
Au Mbowe aliwaahidi dau kubwa Sana mara baada ya kumaliza kazi ya kukata Miti.

Je, walikua na uhakika gani kama watamaliza salama kazi ya kukata Miti? Maana kuna Miti mingine ina nyoka wakali kama koboko.

Kwa kweli Mbowe ni mbahili Sana huwezi kuwapa watu wanne wakate miti kwa shilingi laki sita.

Sijaona popote kama wangetumia gari binafsi ambalo lingehitaji mafuta na dereva,sijaona panga,Shoka wala mashine ya kukatia miti.

Laki sita kwa watu wanne hailipi bana.
 
Unaposikia Samia anajenga Bwawa la Nyerere umewahi kumuona anabeba mifuko ya Cement site?
 
Halafu eti makomandoo hao walikuwa waifanye hiyo kazi ya ugaidi kwa ujira wa pesa za kununulia nguo na nauli tu? Hakuna sehemu nimeona wala kusikia kuwa kulikuwepo na makubaliano ya wao kulipwa pesa. Ina maana walitaka kuifanya hiyo kazi ya ugaidi bure?
 
Nilikuwa sijui kumbe ni rahisi sana kuwa Gaidi!! Yaani ukituhumiwa tu kupanga miti barabarani ili magari yasipite, basi wewe ni gaidi!

Sijapatia picha wale jamaa wanaopanga mawe barabarani ili kupora abiria wa kwenye mabasi na magari ya mizigo!! Yaani wale watakuwa katika levo za ugaidi wa Kimataifa, kama ule wa akina Osama Bin Laden!!
 
Kwenye maelezo ya watuhumiwa kuna sehemu watuhumiwa walienda kukaa Rau ili wabane matumizi vile pesa walio pewa ni ndogo. Hivi kweli mtu ateseke hivyo kwa faida gani?
Ha ha haa.
Laki sita kwa watu wanne inatosha kuifanya nchi isitawaalike.

Wakati huohuo nchi ina jeshi imara kabisa
Ampapo laki sita inatumika kumnunulia maji ya kunywa kwenye kikao cha siku moja kujadili jinsi ya kuwa kamata hao magaidi.
 
Hii kesi DPP atakuja achana nayo mbele ya safari kabla ya hukumu.
 
Back
Top Bottom