Najaribu kuwaza, kwa kasi hii ukubwa wa Deni la Taifa 2030 litakuwaje? Je, kuna haja ya kuhofu?

Tunashukuru Mods kwa weledi wenu
 
Kama tunakopa Kwa ajili ya miradi ya kimkakati bila shaka ikikamilika basi serikali itasitisha kukopa na faida ya miradi itakuza uchumi utakaowezesha kulipa madeni.

Binafsi sioni haja ya wananchi kuhofu hebu tuwe na imani na viongozi wetu Kwa maelezo yao wanaonekana wana nia nzuri na nchi yetu na deni bado la kawaida ukilinganisha na mwenendo wa uchumi wetu.
 
Hii mikopo ingekua inafanya mambo ya maana angalau ila kama ni haya mambo yakununua V8 na kugawa Hela kama pipi ,nimeona kamanda wa Burkina Faso amewekeza kwenye miradi yenye tija badala ya hayo ma v8 kanunua tractors na kupunguza mishahara ya mawaziri huku akiongeza mishahara ya wafanyakazi kwa 50%, ni kiongozi wakuigwa kwa tunakoelekea hili deni si rafiki hata kidogo na hili kwa % kubwa ni haya mambo ya uchaguzi ,,,kwa ukubwa wa hii nchi Tungewekeza kwenye kilimo ,viwanda na kumalizia viporo VYA miradi yenye tija ,hayo mapikipiki na magari yanatuongezea madeni zaidi
 
Uko sahihi
 
LamamayΓ©ee!
Bado hamjasema mpaka mseme.
 
Kikubwa ni kua sisi wananchi hatulipi linalipwa na serikali.
Kumbuka kodi zenu ndizo zitakazolipa hayo madeni.
Mapato yanayokusanywa ndio yanalipa hilo deni.
Mkishindwa mjiandae shilingi yenu kuporomoka zaidi kwasababu ya hilo deni.
Halafu tuone ataumia serikali ama wananchi?
 
Ingekua tunatozwa direct kwa ajili ya kulipa Deni hapo ingekua mbaya
Bro itizame Kenya deni la taifa linavyowaumiza.
Deni likifikia above 45% ya GDP sio himilivu tena.
Hii ina athari mpaka kwa raia mitaani refer kwa Kenya.
Msijidanganye hamtaumia mazeeh.
 
Kikubwa ni kua sisi wananchi hatulipi linalipwa na serikali.
Aisee we jamaa unaishi shimoni? Mi nimetoa elfu 20 kwa wakala nikakatwa 1800 zikaniuma nikaangalia makato nikaona tozo ipo kubwa na ya kutosha sasa we unasemaje wananchi hatulipi deni? Hizo tozo zinaenda wapi kufanya nini? Kataa mikopo unalipa wewe!!
 
Kagame alijisemea ukiwa kiongozi kwenye nchi yenye rasilimali kama madini na gesi na bado unaenda kuomba misaada na kukopa kila siku basi ujue kabisa una matatizo ya akili
 
Mbona huzungumzii Ukubwa wa Uchumi wa Nchi?

Mwigulu ameweka wazi kwamba hoja iwe hela zimekopwa zimetumika wapi na sio kukopa au Ukubwa wa deni.

Hata hivyo sababu zilizochangia Ukubwa wa deni ni depreciation of Shiling na kuongezeka Kwa riba kwenye masoko ya Nje yaani floating rates, tofauti watu kudhani Kila deni likiobgezeka basi Serikali imechukua Mkopo Mpya,huo ni upotovu unaosababishwa na ujinga tuu wa kitoelewa mambo.

Mwisho Kuna Rais hajawahi kukopa? πŸ‘‡πŸ‘‡
 
βœοΈπŸ“πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘ŠπŸ‘πŸ€πŸ™πŸ’πŸŽπŸ™‹β€β™‚οΈπŸ›‘οΈ
 
Harafu inakuja panya moja inasema tz tukope tu maana tunakopa kwa asilimia 5 kuna majinga hii nchi na inatakiwa aje kiongozi kauzu hawa machawa wote awatie ndani na kufukuza kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…