Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

Kipindi niko mdogo niliumwaga tetekuwanga( huu ugonjwa ukipona unabaki na mabaka mabaka mwili mzima kama fisi), nakumbuka baada ya kupona bimdashi alikua anatumia kiazi mbatata anakisugulia kwenye madoa na yalipotea yote kabla hata mwezi mmoja kuisha. Jaribu na wewe kutumia labda inaweza kukusaidia pia
Maganda ya viaz pia ni tiba yaan vyakula vya sasa vinatuathiri sana lakin tukizingatia ulaji wa chakula bora na kuepuka madawa ya madukani itatusaidia sana
 
Unasumbuliwa allergic reaction nenda hospital kubwa wataifanyia damu na sehemu ya ngozi yako culturing na watakaa watasuggest dawa za kukusaidia
 
Tatizo lako haliwezi kuisha kwa dawa za kupaka nje tu ni ngumu na tena acha kabisa.
Tatizo lako kwa kadri ya maelezo yako linasababishwa na mfumo wa homoni ktk mwili wako. Ipo tezi ambayo imeshindwa kuregurate amount of homorne to be secreted in normal form then inakuwa promoted kwa kiwango kikubwa na kuleta madhara kwako.
Tambua kuwa hisia zote tupatazo mwilini ziwe za raha,maumivu,huzuni,kucheka,hamu ya mapenzi na nyinginezo ni matokeo ya tezi kukojoa homoni vitu kama jasho na kuviingiza ktk mfumo wa damu ambapo moyo unaposukuma damu kuzungusha mwulini huzungusha na hizo homoni na ndipo tunapata hisia nilizotaja hapo juu. Kiwango cha homoni lazima kisizidi wala kupungua. Kitendo cha homoni kuzidi huweza kuleta madhara ktk miili yetu yaani alergy.
Tatizo lako linatibika sana tu ila inabidi ukutane na doctor ambaye asiwe na papara akague mwili wako vizr na kususpect vipimo ambavyo vitahusisha damu na kiwango cha homoni. Usikimbilie madaktari njaa.
Uko wapi now.
 
Mamboz,

Jamani kama mnakumbuka nilikua natafuta mchumba na hali yangu niliyonayo, wengi walijitokeza wakidhani natania labda, walihisi mimi ni mzuri sana ila natania.

Kusema ukweli nipo kama nilivyosema na nimerudi tena kuomba msaada kwa anaejua dawa ya makovu tafadhali, sio ya ajali yani yanatokea tu hata nikijikuna kovu linabaki, pia nikiumwa na mdudu lazima kovu libaki,nikijikwaruza kidogo bas kovu hilo.

Wanaume pia hawaniangalii hata mara mbili, niko mpweke, sina hata mwenza.

Nachukia sana ngozi yangu na sijui shida ni nini, naomba tafadhali kwa anaejua dawa ambayo itanifaa.

Wanawake wenzangu nisaidieni, kina baba, kina kaka naombeni mnitajie dawa itakayoondoa makovu haya jamani.

Bio oil nimejaribu haifanyi kazi, aloevera hua napaka sioni matokei, limao pia hakuna kitu.

Najisikia vibaya sana, mda mwingine hua nikijiangalia nalia tu, why me?

Msaada wenu ndugu zangu tafadhali.
Nadhan humu sitaweza kukusaidia bila kukuona na kupata taarifa chache kutoka kwako sjui upo tayari
 
Njia nyingine ya uhakika kwa wenye uhakika.

Amua kuokoka kweli kutoka moyoni, nenda kwenye kanisa la watu waliookoka KWELIKWELI kama T.A.G au E.A.G.T kisha wambie watumishi UNATAKA KUOKOKA, kisha watakuongoza kupokea wokovu.

NB: Si kila tatizo linaweza kutibiwa kwa dawa. Mengine yanasababishwa na nguvu za giza hivyo JINA LA YESU PEKEE LINAWEZA KUKUOKOA.

Kama kweli umeamua kuokoka kutoka moyoni, wambie wakuombee tatizo lako la ngozi, watakuombea utapona kama una imani kwamba Mungu anaweza pia kama umemaaishisha kumfata Mungu/kudumu katika wokovu mpaka mwisho wa maisha yako.

NB: Usiende kuokoka kama unakwenda kujaribu utapona au la! Bali nenda kaokoke kwa kumfata Mungu bila kujali kama atakuponya au hatakuponya. Kwani Wokovu utakupeleka mbinguni. Pia Ukiokoka Mungu anaweza kukuponya magonjwa na matatizo yako yote.

Wokovu si dini, bali ni mabadiliko ya NAFSI yanayofanywa na Mungu kwa yeyote anayempokea Bwana Yesu ili amuokoe na dhambi na jehanamu ya moto.
By
Kwa hiyo hayo makanisa ndo ya wokovu!! Acha kufagilia kanisa unalo sali Yesu hajawahi kuwa na dhehebu
 
Tatizo lako haliwezi kuisha kwa dawa za kupaka nje tu ni ngumu na tena acha kabisa.
Tatizo lako kwa kadri ya maelezo yako linasababishwa na mfumo wa homoni ktk mwili wako. Ipo tezi ambayo imeshindwa kuregurate amount of homorne to be secreted in normal form then inakuwa promoted kwa kiwango kikubwa na kuleta madhara kwako.
Tambua kuwa hisia zote tupatazo mwilini ziwe za raha,maumivu,huzuni,kucheka,hamu ya mapenzi na nyinginezo ni matokeo ya tezi kukojoa homoni vitu kama jasho na kuviingiza ktk mfumo wa damu ambapo moyo unaposukuma damu kuzungusha mwulini huzungusha na hizo homoni na ndipo tunapata hisia nilizotaja hapo juu. Kiwango cha homoni lazima kisizidi wala kupungua. Kitendo cha homoni kuzidi huweza kuleta madhara ktk miili yetu yaani alergy.
Tatizo lako linatibika sana tu ila inabidi ukutane na doctor ambaye asiwe na papara akague mwili wako vizr na kususpect vipimo ambavyo vitahusisha damu na kiwango cha homoni. Usikimbilie madaktari njaa.
Uko wapi now.
Noted!
 
Back
Top Bottom