Najihisi kukata tamaa lakini sitokata, nitapambana

Berlin

Member
Joined
Jun 27, 2014
Posts
66
Reaction score
96
Natumai mko salama. Ningependa kushiriki nanyi wana Jf kuhusu hali yangu ya kifedha na biashara yangu. Biashara yangu imekuwa ikifanya kazi kwa mwaka sasa, lakini mapato yameanza kupungua kutoka kiwango kilichokuwa awali hadi kufikia nusu (ni miezi mitano sasa) Nina mfanyakazi niliemlipa kila siku, na pia nina kodi na mahitaji mengine ya kila mwezi. Kwa sasa, sina kazi nyingine zaidi ya biashara hii, ambayo inaonekana kuwa na changamoto kubwa.

Nina umri wa miaka 27, na hali yangu ya kifedha ni ngumu sana. Madeni ninayokabili, pamoja na malipo ya kodi na mahitaji ya kila mwezi, yanayonikosesha raha na amani (inafika hatua simu inakuwa DND muda wote) Ninaishi kwa hofu kuhusu madeni, ikiwa ni pamoja na malipo ya kodi ya mwenye frame, ambayo inasababisha mtafaruku wa kiakili.

Natamani nisikope tena lakini shida zinanirudisha kule kule, madeni kila kona hadi maduka ya mangi ya mtaani.

Nimejaribu mbinu mbalimbali za biashara, ikiwa ni pamoja na online presence , maoni ya wateja, huduma bora, na mapitio ya wateja, lakini bado sioni matokeo mazuri. Nimejaribu kusali sana na kutoa sadaka, lakini hali bado ni ngumu.

Soma Pia: What do you see yourself in the Midst of Poverty, Suffering and Despair; Katikati ya Kukata Tamaa

Bahati mbaya sana sina sehemu nayoweza pata msaada wowote.

NB:Nina miliki salon ya urembo wa wadada (nywele,make up,kucha ,lashes,dread repairing).
 
Mkuu hiyo ni hali inayopitiwa na miongoni mwa wa Tanzania wengi, usijali hauko pekeyako hasa kwenye rika hilo wanapitia wengi sana hali hiyo. nakusihi usikate tamaa endelea kupambana endelea kuomba kwa imani yako na jipe matumaini kua siku moja kila kitu kitakua sawa tu.
 
Natumai mko salama. Ningependa kushiriki nanyi wana Jf kuhusu hali yangu ya kifedha na biashara yangu. Biashara yangu imekuwa ikifanya kazi kwa mwaka sasa, lakini mapato yameanza kupungua kutoka kiwango kilichokuwa awali hadi kufikia nusu (ni miezi mitano sasa) Nina mfanyakazi niliemlipa kila siku, na pia nina kodi na mahitaji mengine ya kila mwezi. Kwa sasa, sina kazi nyingine zaidi ya biashara hii, ambayo inaonekana kuwa na changamoto kubwa.

Nina umri wa miaka 27, na hali yangu ya kifedha ni ngumu sana. Madeni ninayokabili, pamoja na malipo ya kodi na mahitaji ya kila mwezi, yanayonikosesha raha na amani (inafika hatua simu inakuwa DND muda wote) Ninaishi kwa hofu kuhusu madeni, ikiwa ni pamoja na malipo ya kodi ya mwenye frame, ambayo inasababisha mtafaruku wa kiakili.

Natamani nisikope tena lakini shida zinanirudisha kule kule, madeni kila kona hadi maduka ya mangi ya mtaani.

Nimejaribu mbinu mbalimbali za biashara, ikiwa ni pamoja na online presence , maoni ya wateja, huduma bora, na mapitio ya wateja, lakini bado sioni matokeo mazuri. Nimejaribu kusali sana na kutoa sadaka, lakini hali bado ni ngumu.

Bahati mbaya sana sina sehemu nayoweza pata msaada wowote.
Kwanini unasali na unatoa sadaka lakini bado unakwama mambo yako ?
Unasoma neno (biblia) kila siku ?
 
Biblia ninasoma ila sio kila siku
Ukisoma biblia kama gazeti haiwezi kukusaidia lakini nimetambua shida yako ni moja bado haujapata neema ya kuwa Ile zawadi ya Roho Mtakatifu wewe unahitaji kujipatanisha ni Kristo ili uanze kujua mambo gani inatakiwa kuyafanya baraka huwa zinaanzia katika ulimwengu wa Roho kila jambo unalolianzisha piga magoti omba Mungu akupe kibali
Kasome matendo 1: 1-4
Shika mstari huo usitoke kinywani mwako nenda kanisani Katoe sadaka ndio uanze kufanya hicho ulichoomba Mungu akupe kibali
Utafanikiwa sana hakuna mchawi atayeweza kukuzuia
 
Ameen,nitafanya hivi
 
ushauri mzuri na wenye tija ungeupata kama ungeongeza baadhi ya mambo kama/-

hali yako ya kifamilia(una mke, watoto au wanaokutegemea)

aina ya biashara na location mkoa au wilaya,...

ujuzi wako binafsi na malengo. .....

by the way,....changamoto unazopitia wengi tunapitia tofauti ni mitazamo tu,... NEVER GIVE UP...🙏
 
Back
Top Bottom