A
Anonymous
Guest
Naona kabisa nimepoteza pesa yangu. Na bora pesa, muda wangu ambao siwezi kuurudisha ndiyo kitu kinaniumiza.
Nilianza pale chuoni mwaka 2022, kozi ya miaka 3. Mwaka 2025 nilifanikiwa kumaliza mitihani na practicals zote, ikabakiwa na research pekee. Ila bahati nzuri, mwezi wa 7 huo huo nikapangiwa supervisor wangu.
Tukawa tunawasiliana na amekuwa akinielekeza nini cha kufanya, ila cha ajabu ana tabia ya kutunga matatizo kwenye kazi. Tokea nimefika Chapter 2 mwaka huu mpaka sasa, nimerudishwa zaidi ya mara 12, na kila ukirekebisha kitu anakuja na tatizo lingine.
Nilipoona hii shida, ilibidi nisafiri nije kumuona. Nilijadiliana naye shida ni nini, hakuniambia cha maana zaidi ya, “Wewe fanya ninachokuambia, la sivyo utaanza upya na tutafute supervisor mwingine.”
Nimeongea na kila kiongozi pale Open, maana sikutaka kuondoka bila kuhakikisha nasema jambo langu kwa kila kiongozi pale ili nauli yangu isiwe imeenda bure na mkuu wa idara ajue kabisa.
Ila cha ajabu, hakuna kilichobadilika. Nilipoenda nilichukua namba ya mkuu wa idara kwa ajili ya kumshirikisha shida, ila siku hizi naye hapokei simu. Kwa mawazo yangu, wanateteana, na baada ya kuongea na wenzangu inaonekana wanajua tatizo na kwao ni poa.
Nimekuja kushare hapa, sio vitisho ama kitu gani, ila nataka dunia ijue kwamba niliandika mtandaoni na nilifuata utaratibu wote kwa sababu hawa walimu wetu wana tabia ya kudemonize wanafunzi, tuonekane sisi ndiyo tatizo.
Huyo mkuu wa idara anajua na supervisor anajua kila kitu.
Siku si nyingi nitaamua nitakachoamua, kwa sababu sioni wa kunipa msaada.