jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Great one..hongera kwa mapambano.Mkuu , ni msaada gani unahitaji ? kama msaada wa mawazo nitakuelezea jinsi nilivyojaribu kwa upande wangu.
Huwa hamna msaada wa mtu anamleta mshikaji huku zaidi ya mke wako au watoto wako na uwe umekamilisha taratibu zote za uhamiaji, hata ndugu yako ni vigumu kumleta, sana sana utamtumia hela ya nauli na gharama za viza halafu yeye ajichanganye mwenyewe kuitafuta safari.
Mimi sikulipiwa nauli na wazazi wangu wala kupata koneksheni sababu wazazi hawakuwa na uwezo wala ushawishi wa kunitafutia koneksheni wanazopataga watoto ambao wazazi wao walikuwa na kazi au ushawishi serikalini.
Haya twende..........
Kwanza, nilitafuta hela sababu ndio msingi wenyewe kama unaitafuta safari, nilifanya kazi mikoani maporini nikawaachia mji wa Dar wenyewe wenye hela... japo nikulia na kusomea tokea utotoni...
Nilipiga kazi miaka kadhaa kwenye makampuni ya migodini Kakola Bulyanhulu na kuweza kukusanya hela ya nauli ya safari, tuko pamoja.....
Nikarudi Dar kuitafuta passport, na kuanza kutafuta viza , Nikaenda ubalozi UK wakati huo upo askari monument round about,Samora ave, nikapigwa chini.... na hela kuombea ikaliwa...
Nikaenda ubalozi wa Norway, nikapigwa chini....
Hapo majaribio yote nimetengeneza barua ya mwaliko feki na benki statement ya ukweli lakini na pia hati ya nyumba feki ... yaani we acha tu, vituko kwa kwenda mbele miaka hiyo , hivi velelezo vinahitajika ili uwe na sababu ya kusema wewe utarudi na huwezi kukimbilia kwao, ndio hivyo lakini miaka hiyo ya tisini watu walikuwa wanatusua kimagumashi hivyo hivyo....
Nikaenda ubalozi wa US, wakati huo upo kona ya selander kwenda kinondoni, nikapigwa chini tena....
Nikaona isiwe tabu, nikaamua kutafuta viza ya nchi za ulaya njaa kama Portugal na Spain, mungu si athumani ya Spain ikakubali miaka hiyo ilikuwa rahisi sana kusema unaenda kutembea kama utaonyesha bank statement na pia Spain ni Shenghen Viza inayokuwezesha kutembea za Ulaya Magharibi yote isipokuwa UK, lakini pia unaweza kukukataliwa na nchi binafsi kama wakikuona mbabaishaji...
Nilikaa Spain wiki kadhaa nikiangalia hali inavyokwenda, Nilikuwa Madrid, lakini ni mji mkubwa sana na wamejaa latinos wa marekani ya kusini, na hamna kazi kwa mweusi kama mimi, na wala sijui kispanish, baadae nikapa fununu kuwa Barcelona kidogo poa na kuna weusi wengi mno, nikaamua kujivuta Barca, kufika ni kweli sio weusi tu hata wahindi wanaongea kiswahili nilikutana nao, wana maduka ya kuuza vitu kwa watalii, yaani maduka ya kimachinga, lakini akili hainipi kwamba nimefika ulaya,mimi najua akilini mwangu ni kuanzia France na kwenda mbele ndio ulaya ya kweli , ndio hapo nikaanzia kusafiri nchi moja baada ya nyingine,
Baada ya kukaa siku kadhaa ndani Barcelona, Nilipata msomali anajua kibongo akanikatia tiketi ya kwenda Holland, sababu unatakiwa uonyeshe kitambulisho kama unasafiri nje Spain, nikamkunjia ya soda.....
Kutokea Barcelona Spain nilichukua treni ya usiku kwa tiketi ya kwenda Holland, inapita France na Belgium, hapo nimepewa data kuwa Holland sio kubaya kujilipua.....
Kipande noma kilikuwa ni Border ya France ndio kuna ukaguzi wa passport mara kwa mara unakuwepo, ndani ya behewa kwenye vyumba vya treni, ndani ya chumba niko na Mguinea na Msenegali, wao safari yao wanaishia France na wao ni magumashi hawana vitambulisho wala makaratasi, bora mimi nilikuwa na viza ya shenghen, lakini kiukweli wanaweza kukudaka na kukurudisha Spain kama hueleweki unaenda France kufanya nini bila sababu na uwezo wa kusema wewe ni mtalii..
Hao washikaji ndani humo usiku mzima ni wanaomba sana maombi na kusoma qurani sana...
Mara mlango ukagongwa, wote viroho paaa! tunajishauri tufungue au labda tuuchune watadhani tumelala..
Aliendelea kugonga kwa sana huku akiongeza nguvu, tukaona isiwe tabu tusijezua tukio wakajaa mlangoni kwetu, ile kufungua, kumbe ni ukaguzi wa tiketi , tukajipapasa na kutoa , akaziangalia na kutusemesha kifaransa, wenzagu wakajibu , mimi mweupe hiyo lugha, nikala jiwe, akagonga na kunirudishia tiketi yangu, alivyoondoka , tabasamu wote likatupiga na washikaji waliokoteza vijineno viwili vitatu vya kiingereza na tukawasiliana kwa furaha, na kurudi kulala.
Mara Kuamka tuko France, Stesheni ya Paris Gare de Lyon, kwa mimi natakiwa nitoke stesheni niende kutafuta stesheni za Metro Subway (treni za chini ya ardhi) , kutafuta treni ya kunipeleka mpaka Paris Gare du Nord, ambapo nitakutana na treni za kwenda Amsterdam, Uholanzi.
Washikaji wale wawili wa Guinea na Senegal walikuwa kama wamepata kiwewe , kwa furaha ya kuingia Fra, itakuwa walikuwa na Ndugu au Jamaa pale, maana nawauliza msaada wa kwenda nitapotaka kufika hata hawana time na wanajibu kihivyo hivo kimkatomkato na nilikuwa nawafata stesheni nzima kila kona wananiona gozigozi kweli, lakini nilijua pia ni lugha ndio tunapishana kwa hiyo sikutilia maanani na kuvaa uso wa mbuzi na kuendelea kuwafata nyuma....
Wakamvagaa Mama mmoja mweusi wakaongea nae kifaransa na kumwelezea anielekeze ninapohitaji kwenda, Mama kidogo kiingereza kinapanda ndio ikawa furaha yangu, akaniambia nimfuate , tukaagana na wale jamaa na tukatoka nje ya stesheni na kukata mitaa kadhaa ndani ya baridi kinoma ndio akanipeleka stesheni ya Metro, tukaingia ndani akanioyesha na kuniambia nifate direction ndani ya Metro station ya kwenda kwenye platform ya treni za kunipeleka Saint-Germain-en-Laye.
Nilivyofika stesheni ya Paris Gare du Nord , na kutokujua kwangu nikaenda upande wa treni za UK
na sijui kwamba treni za UK, ni lazima uwe na passport ya nchi yeyeto ya Ulaya (Umoja wa Ulaya EU) ndio unaweza kwenda UK bila Viza, mara Polisi hawa hapa mbele yangu, na hii ndio mara yangu ya kwanza kuongea na kuhojiwa na polisi wa ulaya maana Spain, Polisi hawana time na mtu yeyeto labda mpaka ulete upuuzi....
Wakaniuliza kwa kifaransa , mimi sielewi nikasema ninaweza kuongea kiengereza tu, na wao wako kamili, wakaanza kuniuliza maswali kwa kiengereza, walitaka kujua nina safari kwenda wapi na wakataka kuona tiketi yangu,
Nikawatolea tiketi , baada ya kuona nimekosea platform, ndio wakaniambia hapa sio sahihi na wakiambia niwafate, wakanipeleka mpaka kwenye platform ya treni za Amsterdam, na treni ilikuwa tayari imeshaanza kupakia abiria , yaani ni kama walinisaidia sababu ningechelewa kidogo, ingebidi nisubiri zaidi masaa sita tena stesheni mpaka treni ingine iwe tayari kuondoka, na pia kutokuniuliza passport ilikuwa kama natembelea angani juu unajimu wa "nyota zenu"......
Na ukweli mpaka leo sikumbuki nilikula nini njiani, sababu njaa ilikuwa kama imezimwa akilini mwangu kwenye safari yote......
Nikaingia ndani ya treni, hii ilikuwa ni ya kukaa kwenye siti staili ya kajamba nani....
Mara Belgium hii hapa, lakini sikuhitaji kushuka kubadili treni , niliioona Belguim juu kwa juu tu kupitia dirishani, tukaingiia Amsterdam Centraal Centraal mida ya jioni......
........Lakini pia sikupenda maisha ya Holland, ndio nikaanza adventure ingine ya kuitafuta UK.................
Kilichofuata hapo ni historia.......
Naona niishie hapa........
Mwandiko wangu ni wa kama bata kapita , lakini natumaini utanielewa.........
#MaendeleoHayanaChama