Najisikia vibaya hii inasababishwa na nini?

Mpauko

R.I.P
Joined
Jan 19, 2019
Posts
2,323
Reaction score
3,428
Habari wanajf...

Leo najisikia vibaya mno, asubuhi kilianza kichwa pekee nikameza panadol kikatulia..

Jioni hii najisikia vibaya sana, hata kueleza siwezi ila najisikia vibaya kwelikweli, masikio yanalia ziiiiiii, kichani sijisikii kuwaza lolote, kichefuchefu, homa na hali ya macho kuona kiza kiza, tumbo kama lina njaa kali ngawaje nimekula, yaan kufupi kila kitu najisikia vibaya..

Hali hii ni nini hasa?

Kujisikia vibaya kusikoeleweka wala kuelezeka kunasababishwa na nini?

NOTE:ni baada ya kupunguza nywele kwa kitana na wembe, je kuna uhusiano baina ya kuvutwavutwa kwa nywele na hali hii?

Nimi suruhisho maana hali hiii nakera
 
Kuvutwa nywele labda kichwa lakini sio kuonaa..Kama macho yanauma hasa kwenye mwanga mkali bhasi jaribu kucheki dengue..
 
Nenda kajimwagie maji, kula chakula cha usiku,meza panadol halafu ulale

Kesho asubuhi utaamka mzima kabisa....pole
 
Nenda dispensary ya karibu wakupime BP, mapigo ya moyo, pumzi, kipimajoto, kunywa glass ya maji.
 
Kuepusha ninge, kesho nenda hospitali kwa doctor jieleze kama hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…