---jamani watu wa galilaya na yeriko hebu punguzeni hasira kidogo ili tuweze kuelewana.
najua kila mtu anataka mabadiliko ya kimaendeleo,sasa basi kabla hatujamkosoa rais wetu kuwa hatimizi wajibu wake, hebu tujitizame sisi wenyewe kwanza.
--chukulia mfano wa mtu x,mtu x ni mmoja wa watu wengi wenye hasira na rais kwa sbb aliwaahidi maisha bora na yeye mtu x anadai hayaoni hayo maisha bora aliyoahidiwa,sasa mtu x huyu kaajiriwa lkn 76% ya muda na akili yake yote anawekeza mtandaoni ambako anashinda akimchimbua rais wetu vibaya na kumtupia lawama nyingi.
mtu x amesahau kuwa na yeye ni FISADI sbb analipwa kwa masaa ambayo hajafanya kile alichokubaliana na mwajiri wake bali alishinda ofisini akiitumia internet ya muajiri wake kushinda online mtandaoni!
mtu x amesahau kwamba anachokifanya kushinda mtandaoni kinakwamisha maendeleo yake,ya kampuni yake na taifa kwa ujumla lkn yeye anajiona yuko safi sbb hana raia wanaomkodolea macho ndio maana yuko mstari wa mbele kulalamikia wengine badala ya kuwajibika na kujituma ipasavyo!
hata ktk nchi tajiri,watu wanajituma na kuwajibika hata kwa kufanya kazi 3 ili waweze kulipa madeni ya nyumba nzuri na magari waliyokopa,lkn hawashindi mitandaoni kuanzia asubuhi wanapoingia maofisin na kushinda online 24/7 wakitegemea marais wao wawaletee maendeleo!
hata ktk nchi tajiri wapo ombaomba na masikini wasio na sehemu hata ya kulala,hawa ni sawa na mtu x,hata rais wetu akituletea maendeleo ya aina gani watu kama mtu x bado hawatayaona,maana mtu x yeye hajitumi anasubiri rais amtangazie magari na nyumba za bure zinagawiwa ndio akurupuke kutoka huko mitandaoni anakoshinda online akipiga soga akisubiri maisha bora toka kwa rais.
---hata kama rais hajatekeleza ahadi zake zote,bado haifanyi tum-disqualify,hata rome haikujengwa siku moja,maisha bora kupatikana ni jukumu la kila mtanzania,anza kwanza kujiletea maendeleo ktk serikali yako,onyesha mfano kuwa una machungu yakupata maendeleo,do something kujikomboa na kuwakomboa wengine kwa kuwapa ajira,sio tu ushabiki wa kisiasa kama ushabiki wa simba na yanga.
--mie sina imani na mtu mwingine zaidi ya JAKAYA MRISHO KIKWETE maana kama tu viongozi wa dini tunaotegemea watuongoze kufika peponi wanatusaliti kwa kubaka kunajisi na kudanganya waumini wao ili wawaibie in form of sadaka si hao wengine wanaojifanya wema leo ndio wataipeleka nchi yetu pabaya kabisa!'bora shetani umjuaye kuliko malaika usiyemjua'.
tumchagueni tena rais wetu KIKWETE ,tusiwachague watu wanaojifanya wema leo hawana nia njema na nchi yetu!
mtu x ataendelea kulalamika akisubiri wali wa mchuzi kutoka kwa rais badala ya kujituma,akishituka atakuta wenzie tuko mbali tukifaidi maisha bora tuliyojitafutia wenyewe pamoja na rais wetu!
C.C.M IKO JUUUUUU
KIDUMU CHAMA CHETU CHA MAPINDUZI!