Najivua Gamba baada ya kupata

Najivua Gamba baada ya kupata

kalawetu

Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
19
Reaction score
2
Bila shaka JFs wote mu buheri wa afya. Wahenga waenziwe kwa msemo wao wa mficha uchi hazai. Mwenzenu najivua gamba baada ya kumpata diaresti ambaye nilimsaka kupita foramu hii ya jamii. Nilipata shaka wakati ninaipachika ukutani ukizingaitia kwamba mtu mwenyewe alitakiwa awe wa nchi jirani. Nimempata pia nawashukuru sana walioukubali huu muungano wa afrika mashariki kwani nadhani utakuwa umerahisisha mtu kwenda popote ndani ya nchi hizi 5. Yaani hapa furaha tele moyoni, mguu na njia nyumbani kuangalia ile akiba yangu ili nitoe mahari, si huo ndo utaratibu jamani?
 
Kuwa makini na matapeli wa mapenzi na usiingie kichwa kichwa kabla ya kuchunguza kila kitu
Yaani usiache jiwe lolote halijageuzwa kwenye uchunguzi wako katika kuhakikisha kuwa huyo mpenzi ni real
Mapenzi ni shule so kama unaanza shule huwezi kuanzia la saba kurudi chini
bali unaanzia nursery kwenda juu
Akili kumkichwa
 
Hongera sana mkuu. chukueni muda wa kujuana zaidi na yote yatakua sawa. kila la heri.
 
Hongera mkuu..., ila chukua muda kujiridhisha ili baadaye usije ukatamani kulirudia hilo gamba ulilovua.
 
hongera mkuu!
Nakutakia kila la heri, na uwe umempata anayekufaa.
 
Hongera na Mungu akusaidie broda.
 
he ulipata yule mnyarwanda??? basi na mie naweza kabisaaa kuopoa mzungu humu...LOL
 
hongera sana mkuu,ila kua makini akianza na haari kua ana check sijui ya dola laki ngapi anataka ahamishie tz,usimchekee itakula kwako.
 
Vijana wa sikuhizi bana!!!! Eti mtu wamejuana miezi miwili tu tena mtandaoni eti tayari wameaminiana? jaman ukikosea katika kuoa/olewa lazima uharibikiwe maisha yako, TAKE CARE kijana usijeteseka.
 
Kuwa makini na matapeli wa mapenzi na usiingie kichwa kichwa kabla ya kuchunguza kila kitu
Yaani usiache jiwe lolote halijageuzwa kwenye uchunguzi wako katika kuhakikisha kuwa huyo mpenzi ni real
Mapenzi ni shule so kama unaanza shule huwezi kuanzia la saba kurudi chini
bali unaanzia nursery kwenda juu
Akili kumkichwa
Kweli kabisa brother, najitahidi kukusanya takwimu za kutosha kabla ya kula kiapo.
 
Vijana wa sikuhizi bana!!!! Eti mtu wamejuana miezi miwili tu tena mtandaoni eti tayari wameaminiana? jaman ukikosea katika kuoa/olewa lazima uharibikiwe maisha yako, TAKE CARE kijana usijeteseka.
Ndiyo, najitahidi kuteki great care mzee, na siku zote mawazo ya wazee ni mazuri sa na yapaswa kuzingatiwa. Asante sana kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom