Bila shaka JFs wote mu buheri wa afya. Wahenga waenziwe kwa msemo wao wa mficha uchi hazai. Mwenzenu najivua gamba baada ya kumpata diaresti ambaye nilimsaka kupita foramu hii ya jamii. Nilipata shaka wakati ninaipachika ukutani ukizingaitia kwamba mtu mwenyewe alitakiwa awe wa nchi jirani. Nimempata pia nawashukuru sana walioukubali huu muungano wa afrika mashariki kwani nadhani utakuwa umerahisisha mtu kwenda popote ndani ya nchi hizi 5. Yaani hapa furaha tele moyoni, mguu na njia nyumbani kuangalia ile akiba yangu ili nitoe mahari, si huo ndo utaratibu jamani?