Huenda hayo masomo yako yame-kubias. Engineers wachache nilio interact nao kikazi wako very structured kwenye utendaji wao, na arts nyingi ni less structured. Arts ina fields nyingi na zote zina contribution katika maisha yetu. Ukisha fanya kazi zako kawaida hupenda kujipumzisha, jiulize ni fani gani hukuburudisha-mara nyingi na kwa watu wengi ni arts. Mawasiliano-hufanyika kwa kutumia lugha na kwa Tanzania kwa mfano ni kingereza na kiswahili. Kuna miito ya kufundisha kwa kutumia lugha ya kiswahili huko mbeleni-ni hao hao maprofessor wa kiswahili wanao weza kulifanikisha hilo. Umuhimu wa wachumi na wanasheria hauhitaji kuongelewa zaidi. Kama uko kwenye science ambayo inapeleka product zake kwa communities kuelewa soko likoje unahitaji social scientists. Upokeaji wa chanjo ya polio duniani ni mfano mzuri-kule Nigeria mambo yalikwama hadi watu wa sociology and anthropology walipofungua njia ndio madakitari wakafanikiwa.
Nimesoma science na baadae program ya maendeleo ya kilimo (arts), hivyo kwa kiasi nina uwelewa wa kutosha unaonifanya niwathamini watu wa arts, ingawa enzi hizo tuliona wao si kitu na kuwaita nguini.