Tumgeukie huyo Kikwete wako
JAKAYA MRISHO KIKWETE
1.Mtanzania pekee aliyewafanya wapinzani uchwara walie kuomba uongozi.
Kama unaongelea wapinzani uchwara, basi wewe una uongozi uchwara.Tafadhali tuambie kafanya nini kwa wapinzani ukweli, na sio wapinzani uchwara. You do not judge a leader's ability by how he works with his easiest challenges, but how does he work with his hardest ones.
2.Mtu pekee ambaye mafanikio yake kimaendeleo yanapingwa kwa porojo.(bila takwimu)
Mafanikio gani ? Takwimu zina tabia ya kuweza kudanganya vizuri tu.Ninaweza kuwaita watu wa Kikwete 100 na kuwauliza maswali ambayo yako favorable kwa Kikwete, wakatoa majibu ya kumpendelea Kikwete na kutoa headline kwamba katika survey fulani Kikwete amekubalika 100%. Mafanikio ya Kikwete zaidi ya mafanikio yakutegemewa kwa wastani wa kawaida yako wapi? Hizo shule zisizo na walimu wala majengo ? Hizo ahadi zisizotimilika ? Hebu tupe hayo mafanikio ya Kikwete tuweze kuyajadili. Inaonekana katika kuwashutumu watu kumpinga Kikwete bila takwimu, wewe ndiye unasema Kikwete ana mafanikio bila takwimu.
3.Mtu pekee katika Tanzania ya leo aliyekubali kuacha sheria iwashughulike wanadhirifu wa mali za umma.
Kikwete majuzi kawapigia kampeni Mramba na Lowassa, watu ambao uchafu wao unajulikana na umeelezwa vya kutosha.Kasema Lowassa hakufanya makosa anachafuliwa tu. Kwa kuwapigia kampeni na kutoa kauli kama hizo kuhusu watu hawa, wengine ambao kesi zao bado ziko mahakamani, Kikwete kashaingilia uhuru wa mahakama . Unawezaje kusema kwamba Kikwete kaachia mahakama imshughulike mtu kama Mramba ? Hivi Kikwete kama ana interest ya kumuona Mramba anashinda ubunge ili CCM ichukue kiti, kweli Kikwete anaweza kuwa serious kwa vita dhidi ya rushwa? Kama alikuwa serious kwa nini alimfanmyia kampeni Mramba ambaye kesi yake iko mahakamani na Lowassa ambaye kajiuzulu katika wingu la rushwa ?
4.Rais wa Tanzania 2005 - 2015.
We have lowered the bar so low now to the extent that almost anybody can be president, and this presidential clout business, to seriously thinking people at least, will not be a distinction by itself. What did he do as president ? Watanzania tuna tatizo la kutoa ofisi ambazo mtu kazishika kama distinction. Ofisi ambazo mtu kazishika si distinction. Ukitaka kutuonyesha distinction tuonyeshe huyo mtu kafanya nini katika ofisi hizo.
5. Aliyegeuza ilani ya CCM na mafanikio yake kuwa kama moto ambao kila mpinzani anaogopa kuukaribia.
CCM haina hata itikadi, much less ilani. Ilani gani ? Mafanikio gani ? Sio wewe uliyelaumu watu kumpinga Kikwete bila takwimu, sasa mbona unataka kumtetea bila takwimu na kuvunja sheria yako mwenyewe ?