Elections 2010 Najua baadhi inawauma lakini huyu ataendelea kuwepo

Well done Jembe Jipya. Sishangazwi na coments zako. Kazi ya jembe ni kuchimbia mihogo na majimbi. Sasa kidogo JK kakuzidi upeo wa kufikiria kakuletea power tiller, ndio maana unamwona kila kitu. Mwenzetu utawaza Jembe la mkono mpaka lini? Tembelea mashamba ya walowezi mliowauzia ardhi kule simanjiro ukaone mashine za kisasa kiasi zinavyolima. Ekari moja kwa dakika moja.
So kwa bongolala kama wewe sishangai kuota maendeleo kwa jembe la mkono.
 
Kama kuna kitu serikali ya CCM imefanikiwa katika nchi hii, ni kuwatia ujinga wananchi wengi. MMoja wao ni wewe. Kuwasamehe wezi wa mali ya umma ni kuwashughulikia. Kama yeye ni bora basi watanzania wanaowachoma moto vibaka wa simu ni wachawi.
Nafuu uwe mjinga unaweza elimika, lakini upumbavu loooooh.
Kwa taarifa tu baada ya mpendwa kiongozi wetu kutoa orodha ya mafisadi na wizi wa EPA pale mwembe yanga, watu wawili wa kwanza kuipinga walikuwa ni Kingunge Ngombare Mwiru (The very first day) na Jakaya Mrisho Kikwete (The following day). JK alisema "Kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba usingizi. Maneno ya wapinzani ni sawa na kelele za mlango tu hayatunyimi usingizi". Ama kweli chema chajiuza kibaya chajitembeza. Mabilioni yooooooooooote kwa ajili ya kunadi mlivyotekeleza sera!!!!!!!!! Mbona waliotekeleza sera wanauzika kirahisi tu.
Kama kweli JK atashinda mueleze aende ikulu akafanye kazi zake tu ushindi ni lazima.
 
5. Aliyegeuza ilani ya CCM na mafanikio yake kuwa kama moto ambao kila mpinzani anaogopa kuukaribia.

CCM haina hata itikadi, much less ilani. Ilani gani ? Mafanikio gani ? Sio wewe uliyelaumu watu kumpinga Kikwete bila takwimu, sasa mbona unataka kumtetea bila takwimu na kuvunja sheria yako mwenyewe ?


Kuna kipindi Mr Ben alikiri ilani yao haitekelezeki ingawaje kidogo kulikuwa na afadhali sasa huyu ambaye amevurunda mpaka hicho kidogo alichoachiwa ndio wa kusifiwa hivyo. Watanzania wengine ndio wanaotufanya tubaki hapa tulipo kutokana na upeo wa uelewa.

 

Wewe ni mtu pekee usiye na upeo wa kubaini kuwa una tatizo. UMECHEMSHA HATUDANGANYIKI
 
KWENYE NYEKUNDU HAPO NI UTATA MTUPU, LEO UNAMFIKISHA MTU MAHAKAMANI KESHO KWENYE JUKWAA LA SIASA UNAWAAMBIA WATU WAMCHGUE AWE KIONGOZI:mad2:, HUU NI UJINGA MTUPU.
 


😛hone:Balozi wa Marekani :cell:Obama :A S 100: Mr. Prezidaaaaa
Hadi uchaguzi ufike tutavunjika mbavu zetu lol!:laugh::laugh::laugh:
 
Njaa mja wa laana, na mwenye njaa utamjua tu kwa maneno na matendo yake.
KAKA UNA NJAA
 
Naam, inatuuma sana kwa sababu mwaka 2005 tuliahidiwa "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" lakini leo hii tunaona hakuna maisha yoyote bora bali maisha yanazidi kuwa magumu kupindukia! Na inazidi kutuuma sana kwa sababu zinafanywa na zitaendelea kufanywa kila aina ya mbinu kuwalaghai wananchi ili warudie makosa ya kuchagua kiongozi ambaye alitoa ahadi ya uongo! Yapo mengi mno yanayofanya wengi sana ituume iwapo rais aliyetudanganya mwaka 2005 ataendelea tena kutuongoza!
 
Kuna watu mwezi huu wamechachamaa sana kutuma post za kijinga naona wametumwa.
Sisi umu jamvini sio wadanganyika kwaiyo usitegeme kwamba unaweza kutudanganya ili umfurahishe boss wako ccm.
Maendeleo yaliyoletwa na CCM;uvutaji na uhuzaji wa madawa ya kulevya,Rushwa yakupindukia,Ufisadi,Mikataba mibovu inayomnufaisha sana mwekezaji na kumumiza sana Mtanzania mwenye mali yake,Umalaya sio wazee wala vijana mana wanapata pesa za wizi kwaiyo azina uchungu kuzifanyia uwasherati,Bei za vitu kupanda,Uwenda wazimu,naomba mengine muongezee wana jamvini.

Atudanganyiki tulishakataa.
 

Kiranga,

Hebu tufanyie hisani wasomaji wako utuandikie kwa lugha ya taifa. Manake vingi vinaweza kuwa 'lost in translation' kisha ujumbe ukashindwa kutufikia walengwa bure.
 

Kosa lake moja tu .......huwa anaikosoa Chadema. Akiacha hilo tu nafikiri ataonekana Hero wa JF saa zote :confused2:
 

Hilo la kuongea na ubalozi ni ukweli. Huwezi ukatangaza umeongea na balozi wakati hujaongea naye, ubalozi sio wababaishaji, wangeweza kumwumbua. Kama ni usanii labda timing. Huenda JK alijua balozi ataongea naye juuu ya nini na akamruhusu wakati ule ambao ungeweza kuwa mzuri kwake kwenye kampeni.

Pia ni kweli Obama kaisifia Tanzania wakati anahutubia UN.
 

Akiwalima CHADEMA mnamtukana, akiwalima CCM mnamshangilia. You can't have your cake and eat it too.

Kiranga ni mtu makini na mwenye hoja na lazima muheshimu michango yake hata kama inailima CHADEMA.
 
Watu wa Europe wanapenda waafrika tuendelee kuwa mazuzu ili watutawale vizuri.ndo maana utashangaa kiongozi anafanya ujinga katika nchi flani na wao wanamsifia.ukiwa mwerevu tu unakuwa adui yao kama raisi wa Iran au wa Korea Kaskazini.hapo ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Akiwalima CHADEMA mnamtukana, akiwalima CCM mnamshangilia. You can't have your cake and eat it too.

Kiranga ni mtu makini na mwenye hoja na lazima muheshimu michango yake hata kama inailima CHADEMA.

Umakini wa kukomaa na Regia Mtema?? Umakini wa kutaka Slaa aoneshe umahiri wa ukatibu-muktasi? Nay thanx
 
Umakini wa kukomaa na Regia Mtema?? Umakini wa kutaka Slaa aoneshe umahiri wa ukatibu-muktasi? Nay thanx

I could dispute all that vehemently in the Kiranga tradition. But for a moment, let us not get distracted.

Kiranga is not running for president, Kikwete is. This thread is about Kikwete, not Kiranga.

Hebu tumchambue Kikwete na tuache side stories za Alfu-Lela-U-Lela ambazo zina hadithi ndani ya hadithi mpaka tutapotea katika labyrinth hili lisilo mwisho.

Kiranga is a nobody in the Tanzanian scheme of things.Tumjadili Kikwete kama alivyoletwa na mchangiaji wa kwanza.
 

Nina wasiwasi huenda huyu ndiye yule 'Acting Editor' wa Daily Noise ambalo juzi liliandika upupu katika tahariri yake. Kilichoandikwa hapa ni sawia kabisa na kilishoandikwa katika tahariri ya gazeti la sirikali.
 

Really? why won't try me?

Suala la JK mi nilishamaliza kuchangia.
 
Really? why won't try me?

Suala la JK mi nilishamaliza kuchangia.

I just don't want to make this one more thread about Kiranga. Like I said, Kiranga is an insignificant figure in the great scheme of things.

Kama ulishamaliza kumchambua Kikwete ahsante, ningependa kuona wengine ambao hawajamaliza wanafikiri nini kuhusu hii topic.
 

Utani mwingine haufai kabisa. Mbona watutania wewe? Are you serious na haya usemayo? Unafikiri sisi hatuoni kinachoendelea TZ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…