wanawake wengi wanasamehe na kusahau....pia, ndoa nyingi ambazo baba ni kinara wa kutoka nje ya ndoa, mkewe akitoka ni rahisi kusamehe kwasababu anaona kama sawa tu kwasababu yeye pia hutoka nje ya ndoa...ila kuna aina hii ya ndoa ambayo baba hajawahi kutoka nje ya ndoa, na hategemei kutoka nje ya ndoa...au mama hajawahi kutoka nje ya ndoa na hategemei kutoka nje ya ndoa..mmojawapo akitoka nje ya ndoa, kidonda chake huwa ni kukubwa sana, na kama anatoka kabila fulani hivi, unaweza kumkuta ananing'inia au kama sivyo makabila mengine, atakucharanga mapanga au atakuwa chizi...cha muhimu kuelewa ni kwamba, kutoka nje ya ndoa ni dhambi kubwa ambao Mungu huwa anaadhibu, dhambi zote ni sawa lakini Mungu anasisisita uzinzi akisema kuwa, ni dhambi tofauti na zingine kwasababu inafanyika ndani ya mwili pale mnapoingiliana, mnajiunganisha na ni dhambi ambayo huwa haiendi bila mapigo mbele za Mungu kama mtu hatatubu kwa kumaanish akuiacha. pili, kwa wale waliotendwa awe mwanaume au mwanamke, jua kuwa, kusamehe ni lazima, na usiposamehe, Mungu pia hatakusamehe.
kama vile unavyoona inauma sana unapotendwa na mkeo au mmeo, hivyohivyo inamuuma sana Mungu pale unapomsaliti kwa kukubali mambo ya kishetani badala ya kumwamini na kumsubiri yeye...imagine mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji akiona kuwa ndo suluhisho badala ya kwneda kwa Mungu, that means, mganga ni muhimu kwake na ana nguvu kwake kuliko Mungu..tusi gani hilo? ni mambo gani tumefanya kwa kumsaliti Mungu, na ni madhambi mengi sana watu tunafanya waziwazi na Mungu anatuona hata akiwa ameshatuonya...lakini Mungu anatuvumilia kwa neema yake, anatusamehe....Mungu akihesabu maovu ni nani atakayesimama? USIPOWASAMEHE WATU MAKOSA YAO YA MUNGU WETU WA MBINGUNI HATATUSAMEHE SISI MAKOSA YETU...kusamehe hakuna option...