Najua ni suicide mission, ila nimeamua kurudisha mbegu za asili shambani

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
478
Reaction score
1,025
Imekuwa ni agenda na mpango wa siri ili kuepuka vikwazo vya kimamlaka at early stage ila mpango unaenda sawa na hapa ulipo no turning back. Ni muda sasa tangu mbegu zetu za asili kupotea katika mzunguko baada ya mamlaka kuchezewa akili kwa kujua au kutokujua na kuruhusu wazungu kuteletea mbegu chotara ambazo hizo huzaa mara moja na baada ya hapo ukirudisha iyo mbegu shambani haiwezi tena kuota au wakati mwingine isizae kabisa hivyo wakulima kubaki wakilipa bila msaada.

Huu mpango ulichezwa vizuri na wazungu kuhakikisha wanazipoteza mbegu zetu za asili zilizokuwa zinavumilia ukame, zinatoa mazao mengi na hapo hapo mkulima anaweza chagua mbegu katika hayo mazao ambayo msimu unaofata hurudishwa shambani na kuota tena.

Walituaminisha mbegu zetu ni duni, hazizai ipasavyo, wakatuambia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani ,mbegu zetu haziwezi kuhimili mabadiliko hayo hivyo mbegu zao (GMO) ndo suluhusho pekee. Wakatufanya watumwa kwa kutegemea mbegu zao, wakatuletea na mbolea zao ambazo bila kutumia hizo hupati mazao, mbolea hizo zikapelekea kuiharibu rutuba ya udongo hivyo tumejikuta tumebaki na ardhi usiyoweza kufanyia kazi bila kuweka mbegu ya mzungu na mbolea ya mzungu.

Wakulima wamebaki maskini wakitegemea mfumo huu ulioandaliwa rasmi kuwafanya watumwa katika ardhi yao wenyewe. Leo mbegu na mbolea hazigusiki, mkulima analia na serikali, serikali inalia na wazungu Ili kupata mbegu na mbolea.

Serikali zetu zimekosa watu wenye maono na upendo halisi kwa nchi yao inafika mahali nchi inauza wananchi wake kwa wazungu kuwafanya watumwa. Wazungu wanakuja na agenda zao za kujinufaisha, viongozi wanasaini mikataba bila kufikiria kwa undani mwisho wa siku wananchi wanabaki stranded kwenye maisha yao.

Nimefanikiwa kuzunguka na kupata mbegu za asili na kwa kuanza nimeotesha ekari 1000 za mahindi, ekari 1000 za maharage na ekari 1000 za alizeti. Nashukuru Mungu zimeota vizuri na wakati wa kuvuna ukifika regardless gharama zote zilizotumika nita package maavuno yote, kwenye mfumo wa 1kg, 5kg, 10kg, 25kg, 50kg na 100kg, lengo ni kuwapatia wakulima mbegu za asili kwa gharama ya shillingi elfu 1000 kwa kilo 1 na nyie mkienda kulima huko, mkivuna muhifadhi mbegu zenu Ili mwakani msirudi tena kutafuta mbegu. Mbegu Hizi zikifanikiwa kuuzwa kwa wakulima million moja naamini baada ya miaka 5 mbegu zetu zitakuwa zimerudi mashambani kwetu. Hii itasaidia kupunguza magonjwa na maradhi yanayosumbua sasa kwenye JAMII zetu yanayosababishwa na kutumia mbegu za GMO ikiwepo kansa na kisukari. Mikakati imeanza na aina tatu ya mbegu ila huku tuendako tunakuja mpaka na mbegu za mbogamboga aina zote zile za asili, migomba, karanga, ufuta, na nyingine nyingi tu ambazo zimepotea hata GenZ hawazijui wala hajawai kuziona.

Watakaoniunga mkono basi twende pamoja na wanaopinga pia subirini matokeo.

Matajiri na supplier wote wa GMO tusichukiane haya ni mapinduzi katika kilimo na hakuna mwingine wa kufanya zaidi yetu wenyewe.

Msiulize mashamba yako wapi maana sitawaambia wahuni wasije kuharibu ila mavuno yakitoka ntawaonyesha na namna ya kupata ntawaambia kikubwa tulindane tu maana tunaenda kuharibu ugali wa watu..

Stay tuned.....stay connected.....mambo yote ni hapa hapa.
 
Attachments

  • Screenshot_20250329-132712.png
    Screenshot_20250329-132712.png
    767 KB · Views: 48
Tatizo nafaka au hayo mazao yakiingia sokoni hakuna mtu atauliza hii ni GMO au hii ni ya asili...
Hawa wakulima wanaotumia GMO wanapata mazao mengi zaidi ndani ya muda mfupi, hawa wenye mbegu za asili wakiona hivyo inabidi na wao watumie GMO kukimbizana na soko na kipato...
 
Ni mpango uliosukwa Ili kuhakikisha tunabaki watumwa kwa namna yoyote Ile ndo maana hapa tulipo tunaona kama ni too late ila everything is possible
 
Kama ni Kwa chakula chako tu fresh ila kibiashara ni big No
Yes, lengo ni kupata chakula Bora kwenye level ya kaya na ukitaka kufanya commercial farming unaweza pia kwa wale wenye uhitaji wa kuuza vyakula Bora kwa watanzania na nje pia
 
Tatizo nafaka au hayo mazao yakiingia sokoni hakuna mtu atauliza hii ni GMO au hii ni ya asili...
Hawa wakulima wanaotumia GMO wanapata mazao mengi zaidi ndani ya muda mfupi, hawa wenye mbegu za asili wakiona hivyo inabidi na wao watumie GMO kukimbizana na soko na kipato...
Kwanza ni muhimu mtofautishe GMO na Hybrid.
Kwa Tanzania GMO zimepigwa marufuku! Mbegu zilizopo ni hybrids. Wakati GMO zinaweza kuunganisha DNA ya mmea na DNA ya kiumbe chochote kile... Hybrid seeds nyingi ni matokeo ya kulazimisha uchavushaji miongoni mwa mimea ya jamii moja Ili kupata kizazi bora zaidi chenye sifa mchanganyiko kuendana na mahitaji... Hybrid seeds ni mazao mashambani.
GMO seeds ni mazao ndani ya maabara! Yaani kifupi ni kama zile robots za Elon Musk!

Mbegu za asili zinaitwa Heirloom Seeds kimsingi hizi zinarithishwa kizazi hadi kizazi!

Soma zaidi hapa: GMO, Hybrid, Organic, and Heirloom Seeds. What’s The Difference?

Wakati ambapo Kenya wameruhusu GMOs, Tanzania inapingana na GMO. Na kati ya vitu ambavyo mamlaka ya kudhibiti mbegu TOSCI (TOSCI | Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu - Mwanzo) kwa kushirikiana na TPHPA (TPHPA | Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania - Mwanzo)
wanasimamia vizuri ni kudhibiti GMOs zisiingizwe nchini.
NI IMANI YANGU KWAMBA GMOs BADO HAZIJAINGIZWA NCHINI! KAMA UNA UTHIBITISHO WEKA HAPA NINA KAZI NAYO!

CC Upekuzi101, and 100 others
 
Hyo opv kwa mvua ipi?bora gmo unaweza kuoketeza wameclassified ktk level mbalimbali ipo ya mda mfupi na mda mrefu
 
ni katika kauli na sheria za nchi.. kama mirungi inavyopigwa marufuku, bangi, cocaine n.k lakini mtaani vipo na watu wanatumia.
Tanzania haijawahi kuwa seriously kupambania maslahi ya wananchi wake, vinywaji fake, vyakula visivyo na ubora mtaani vingi, tbs ndio hao wanakula rushwa..

GMO zipo sana masokoni na waTanzania wanalishwa sana tu, tusijidanganye..

Tofauti yetu na Kenya, wao wamehalalisha na wameamua kukubali..
 
Kwanza ni muhimu mtofautishe GMO na Hybrid.
Kwa Tanzania GMO zimepigwa marufuku! Mbegu zilizopo ni hybrids. Wakati GMO zinaweza kuunganisha DNA ya mmea na DNA ya kiumbe chochote kile... Hybrid seeds nyingi ni matokeo ya kulazimisha uchavushaji miongoni mwa mimea... Hybrid seeds ni mazao mashambani.
GMO seeds ni mazao ndani ya maabara!

Mbegu za asili zinaitwa Heirloom Seeds kimsingi hizi zinarithishwa kizazi hadi kizazi!

Soma zaidi hapa: GMO, Hybrid, Organic, and Heirloom Seeds. What’s The Difference?

Wakati ambapo Kenya wameruhusu GMOs, Tanzania inapingana na GMO. Na kati ya vitu ambavyo mamlaka ya kudhibiti mbegu TOSCI (TOSCI | Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu - Mwanzo) kwa kushirikiana na TPHPA (TPHPA | Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania - Mwanzo)
wanasimamia vizuri ni kudhibiti GMOs zisiingizwe nchini.
NI IMANI YANGU KWAMBA GMOs BADO HAZIJAINGIZWA NCHINI! KAMA UNA UTHIBITISHO WEKA HAPA NINA KAZI NAYO!

CC Upekuzi101, and 100 others
Umemjibu vizuri sana mleta uzi. Shida mleta uzi kakurupuka na tangazo la Gwajima akaona aje aanzishe uzi apate ujiko.

Acheni kufata mkumbo wa wanasiasa. Wenzenu ndio kazi zao majukwaani
 
Kwanza ni muhimu mtofautishe GMO na Hybrid.
Kwa Tanzania GMO zimepigwa marufuku! Mbegu zilizopo ni hybrids. Wakati GMO zinaweza kuunganisha DNA ya mmea na DNA ya kiumbe chochote kile... Hybrid seeds nyingi ni matokeo ya kulazimisha uchavushaji miongoni mwa mimea... Hybrid seeds ni mazao mashambani.
GMO seeds ni mazao ndani ya maabara!

Mbegu za asili zinaitwa Heirloom Seeds kimsingi hizi zinarithishwa kizazi hadi kizazi!

Soma zaidi hapa: GMO, Hybrid, Organic, and Heirloom Seeds. What’s The Difference?

Wakati ambapo Kenya wameruhusu GMOs, Tanzania inapingana na GMO. Na kati ya vitu ambavyo mamlaka ya kudhibiti mbegu TOSCI (TOSCI | Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu - Mwanzo) kwa kushirikiana na TPHPA (TPHPA | Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania - Mwanzo)
wanasimamia vizuri ni kudhibiti GMOs zisiingizwe nchini.
NI IMANI YANGU KWAMBA GMOs BADO HAZIJAINGIZWA NCHINI! KAMA UNA UTHIBITISHO WEKA HAPA NINA KAZI NAYO!

CC Upekuzi101, and 100 others
ni katika kauli na sheria za nchi.. kama mirungi inavyopigwa marufuku, bangi, cocaine n.k lakini mtaani vipo na watu wanatumia.
Tanzania haijawahi kuwa seriously kupambania maslahi ya wananchi wake, vinywaji fake, vyakula visivyo na ubora mtaani vingi, tbs ndio hao wanakula rushwa..

GMO zipo sana masokoni na waTanzania wanalishwa sana tu, tusijidanganye..

Tofauti yetu na Kenya, wao wamehalalisha na wameamua kukubali..
 
Imekuwa ni agenda na mpango wa siri ili kuepuka vikwazo vya kimamlaka at early stage ila mpango unaenda sawa na hapa ulipo no turning back. Ni muda sasa tangu mbegu zetu za asili kupotea katika mzunguko baada ya mamlaka kuchezewa akili kwa kujua au kutokujua na kuruhusu wazungu kuteletea mbegu chotara ambazo hizo huzaa mara moja na baada ya hapo ukirudisha iyo mbegu shambani haiwezi tena kuota au wakati mwingine isizae kabisa hivyo wakulima kubaki wakilipa bila msaada.

Huu mpango ulichezwa vizuri na wazungu kuhakikisha wanazipoteza mbegu zetu za asili zilizokuwa zinavumilia ukame, zinatoa mazao mengi na hapo hapo mkulima anaweza chagua mbegu katika hayo mazao ambayo msimu unaofata hurudishwa shambani na kuota tena.

Walituaminisha mbegu zetu ni duni, hazizai ipasavyo, wakatuambia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani ,mbegu zetu haziwezi kuhimili mabadiliko hayo hivyo mbegu zao (GMO) ndo suluhusho pekee. Wakatufanya watumwa kwa kutegemea mbegu zao, wakatuletea na mbolea zao ambazo bila kutumia hizo hupati mazao, mbolea hizo zikapelekea kuiharibu rutuba ya udongo hivyo tumejikuta tumebaki na ardhi usiyoweza kufanyia kazi bila kuweka mbegu ya mzungu na mbolea ya mzungu.

Wakulima wamebaki maskini wakitegemea mfumo huu ulioandaliwa rasmi kuwafanya watumwa katika ardhi yao wenyewe. Leo mbegu na mbolea hazigusiki, mkulima analia na serikali, serikali inalia na wazungu Ili kupata mbegu na mbolea.

Serikali zetu zimekosa watu wenye maono na upendo halisi kwa nchi yao inafika mahali nchi inauza wananchi wake kwa wazungu kuwafanya watumwa. Wazungu wanakuja na agenda zao za kujinufaisha, viongozi wanasaini mikataba bila kufikiria kwa undani mwisho wa siku wananchi wanabaki stranded kwenye maisha yao.

Nimefanikiwa kuzunguka na kupata mbegu za asili na kwa kuanza nimeotesha ekari 1000 za mahindi, ekari 1000 za maharage na ekari 1000 za alizeti. Nashukuru Mungu zimeota vizuri na wakati wa kuvuna ukifika regardless gharama zote zilizotumika nita package maavuno yote, kwenye mfumo wa 1kg, 5kg, 10kg, 25kg, 50kg na 100kg, lengo ni kuwapatia wakulima mbegu za asili kwa gharama ya shillingi elfu 1000 kwa kilo 1 na nyie mkienda kulima huko, mkivuna muhifadhi mbegu zenu Ili mwakani msirudi tena kutafuta mbegu. Mbegu Hizi zikifanikiwa kuuzwa kwa wakulima million moja naamini baada ya miaka 5 mbegu zetu zitakuwa zimerudi mashambani kwetu. Hii itasaidia kupunguza magonjwa na maradhi yanayosumbua sasa kwenye JAMII zetu yanayosababishwa na kutumia mbegu za GMO ikiwepo kansa na kisukari. Mikakati imeanza na aina tatu ya mbegu ila huku tuendako tunakuja mpaka na mbegu za mbogamboga aina zote zile za asili, migomba, karanga, ufuta, na nyingine nyingi tu ambazo zimepotea hata GenZ hawazijui wala hajawai kuziona.

Watakaoniunga mkono basi twende pamoja na wanaopinga pia subirini matokeo.

Matajiri na supplier wote wa GMO tusichukiane haya ni mapinduzi katika kilimo na hakuna mwingine wa kufanya zaidi yetu wenyewe.

Msiulize mashamba yako wapi maana sitawaambia wahuni wasije kuharibu ila mavuno yakitoka ntawaonyesha na namna ya kupata ntawaambia kikubwa tulindane tu maana tunaenda kuharibu ugali wa watu..

Stay tuned.....stay connected.....mambo yote ni hapa hapa.
Good ✔️
 
Tatizo nafaka au hayo mazao yakiingia sokoni hakuna mtu atauliza hii ni GMO au hii ni ya asili...
Hawa wakulima wanaotumia GMO wanapata mazao mengi zaidi ndani ya muda mfupi, hawa wenye mbegu za asili wakiona hivyo inabidi na wao watumie GMO kukimbizana na soko na kipato...
Hivi anaewadanganya bongo kuna gmo ni nani? Au hamjui maana ya mbegu za gmo ? Mbegu zilizopo bongo zinaitwa hybrid seed na sio gmo km mnavyodhani
 
Unachozungumza ni sawa na kusema kisa serikali imepiga marufuku mirungi , bangi na cocaine ndipo iwe sababu mtaani havipo.
Kwa Kenya kuitambua GMO, tayari Tanzania ipo, na wewe hapo umeshakula GMO vya kutosha.

Hii nchi haijawahi kuwa serious kwenye afya ya wananchi wake hususani ulaji.

GMO zipo kibao mashambani na zipo kibao masokoni.. tusidanganyane..
 
Ni mpango uliosukwa Ili kuhakikisha tunabaki watumwa kwa namna yoyote Ile ndo maana hapa tulipo tunaona kama ni too late ila everything is possible
Kwanza nani amekuanbia Tanzania kuna mbegu ambazo ni GMO?! Unapuyanga tu kuandika pumba
 
ni katika kauli na sheria za nchi.. kama mirungi inavyopigwa marufuku, bangi, cocaine n.k lakini mtaani vipo na watu wanatumia.
Tanzania haijawahi kuwa seriously kupambania maslahi ya wananchi wake, vinywaji fake, vyakula visivyo na ubora mtaani vingi, tbs ndio hao wanakula rushwa..

GMO zipo sana masokoni na waTanzania wanalishwa sana tu, tusijidanganye..

Tofauti yetu na Kenya, wao wamehalalisha na wameamua kukubali..
Naomba ushahidi ama uthibitisho.. Please nisaidie! Nina kazi nayo!
 
Hivi anaewadanganya bongo kuna gmo ni nani? Au hamjui maana ya mbegu za gmo ? Mbegu zilizopo bongo zinaitwa hybrid seed na sio gmo km mnavyodhani
Alete ushahidi au uthibitisho! Kuna mahali kuna fedha za bure!
 
Nazitamani sana mbegu za asili za mahindi, zimepotea kabisa!! Nakuunga mkono, wakulima wengi wakikuunga mkono tutaokoa mbegu zetu za asili.

Mbegu nyingi sana za asili zimepotea zimebakia GMO.
 
Kwanza ni muhimu mtofautishe GMO na Hybrid.
Kwa Tanzania GMO zimepigwa marufuku! Mbegu zilizopo ni hybrids. Wakati GMO zinaweza kuunganisha DNA ya mmea na DNA ya kiumbe chochote kile... Hybrid seeds nyingi ni matokeo ya kulazimisha uchavushaji miongoni mwa mimea ya jamii moja Ili kupata kizazi bora zaidi chenye sifa mchanganyiko kuendana na mahitaji... Hybrid seeds ni mazao mashambani.
GMO seeds ni mazao ndani ya maabara! Yaani kifupi ni kama zile robots za Elon Musk!

Mbegu za asili zinaitwa Heirloom Seeds kimsingi hizi zinarithishwa kizazi hadi kizazi!

Soma zaidi hapa: GMO, Hybrid, Organic, and Heirloom Seeds. What’s The Difference?

Wakati ambapo Kenya wameruhusu GMOs, Tanzania inapingana na GMO. Na kati ya vitu ambavyo mamlaka ya kudhibiti mbegu TOSCI (TOSCI | Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu - Mwanzo) kwa kushirikiana na TPHPA (TPHPA | Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania - Mwanzo)
wanasimamia vizuri ni kudhibiti GMOs zisiingizwe nchini.
NI IMANI YANGU KWAMBA GMOs BADO HAZIJAINGIZWA NCHINI! KAMA UNA UTHIBITISHO WEKA HAPA NINA KAZI NAYO!

CC Upekuzi101, and 100 others
Kuna Hybrid yenye Terminal Gene ?
 
Back
Top Bottom