Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 142
Udereva si tatizo, e ndugu yangu sikia
Fungua na masikio, hoja hujaipatia
Sio waja mbio mbio, dereva wanidhania
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu
Mabovu wayatetea, njiani kusafiria
vipi tatuelezea, safari kikudodea
Ni mabaya mazoea, vundo kuukodolea
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu
sindano mwana wa ganzi
Yakuonea wataka ligi,na kikombe kuchua.
Sio kama siiwezi,hilo kaa ukijua.
Nataka kui maizi,kindaki ndaki kujua.
Sasa nakupa mji,hoja kunifumbilia.
Mashairi yamekua yananivutia siku zinavyozidi kwenda....mmmh
nikazane kujifunza...
Mi mashairi hua yananiletea usingizi afu yananifanya niskie njaaa.
Gari hili si la kwangu, ndugu ninakuambia
Liliona toka tangu, nikataka jipandia
Na wala si la mafungu, kweli ninakuapia
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa
Kupanda la pili si hoja, ubora ndo zingatio
Mengi ya sasa viroja, kufika ndo kusudio
Sitaki safari moja, nizugishwe na vilio
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa
kwa nje yanavutia, machoni tatamania
Mikono ukishatia, ndani kujichunguzia
Tashindwa kuaminia, tafiti utanambia
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa
sindano mwana wa ganzi
Gari linalotembea,
Linaloingizwa gia,
Usukani shikilia,
Safari yaendelea.
Safari utaifika, piga konde moyo wako.
Kishaingia garini,
Uendapo safarini,
Siangalie nyumani,
Safari iko mbeleni.
Gari likisha tumika, Siyo limekongoroka.
Ya nyuma kuyawazia,
Moyo wajiumizia,
Wala hitosaidia,
Safari yakungojea
Magari yalotumika, Bado yapo safarini.
Garini kishaingia,
Nyuma acha angalia,
Safari itaishia,
Nyumani kutakukwaza.
Safari iko mbeleni, siyo nyuma utokako.
Gari kijinyakulia,
Safari hakikishia,
Gari sevisi fanyia,
Safari itanogea.
Gari yake ni sevisi, Na siyo uzuri sura.
Gari linalotembea,
Linaloingizwa gia,
Usukani shikilia,
Safari yaendelea.
Safari utaifika, piga konde moyo wako.
Kishaingia garini,
Uendapo safarini,
Siangalie nyumani,
Safari iko mbeleni.
Gari likisha tumika, Siyo limekongoroka.
Ya nyuma kuyawazia,
Moyo wajiumizia,
Wala hitosaidia,
Safari yakungojea
Magari yalotumika, Bado yapo safarini.
Garini kishaingia,
Nyuma acha angalia,
Safari itaishia,
Nyumani kutakukwaza.
Safari iko mbeleni, siyo nyuma utokako.
Gari kijinyakulia,
Safari hakikishia,
Gari sevisi fanyia,
Safari itanogea.
Gari yake ni sevisi, Na siyo uzuri sura.
Hakuna ligi yoyote, ewe matuka sikia
Na fani ni yetu sote, huoni twafurahia
vipi unipe kikombe, na mji watoa pia
Hoja ni kutofikishwa, kama nilivyodhamiria
Utaonaje furaha, gari yakuzimikia
Mimi kwangu ni karaha, wepesi sitasikia
Kweli hata ukihaha, injini imejifia
Hoja ni kutofikishwa, kama nilivyodhamiria
sindano mwana wa ganzi
Mwenye kuanza safari,nia kwisha jitilia.
Kufika ame hiyari,hiyo ndio kidunia.
Miguu ama gari,kufika ndio dhamira.
Hato kwama vuli,kipupwe yake masika.
Safari namna hizi,gari yako nunua.
Yenye kupendeza machoni,na kupanda pia.
Chagua rangi thamani,nyeupe au kahawia.
Mifumo kwenye injini,vyema uka somea.
Ukilimiliki gari,utajua na kutumia.
Kasi kwenye lami,na matope kudemea.
Salama na makini,safarini wa tanua.
Sio lile la kukodi,ingawa lina vutia.
Nadhani hiyo ndo itakua njia pekeee mkuu asante kwa ushauri.Hahaha......nakushauri ufanye hivi, chapa msosi afu ukimaliza unalala.......swaaaaaf
Nadhani hiyo ndo itakua njia pekeee mkuu asante kwa ushauri.
we lipande tu, that is your fate!
Sanda nimekusikia, yote uliyo usia
Sawa nitakusudia, la kwangu kujipatia
Niache ya kudandia, safarini sitafika
Wapi naweza pata, la injini siyoguswa
Sitaki eti lolote, moyoni sitaridhia
Au la kwenye matope, mjini yana kadhia
Kuna yale kiokote, kinunua tajutia
Wapi naweza pata, la injini siyoguswa
Nataka liwe jipya, mashine kichungulia
Hapa nina uhakika, dunia tazungukia
Nitaondokwa mashaka, sababu nalijulia
wapi naweza pata, la injini siyoguswa
Siwezi nunua gari, iliyokwisha tumika
Na kila siku si shwari, sipana ninajitwika
Nyingi kikiri kikiri, wabaki wataabika
wapi naweza pata, la injini isoguswa
sindano mwana wa ganzi
Polepole elezea, kipi kilicho vutia
Kwa gari silolijua,nini umekimbilia
Ulipenda ya njiani,sasa yamekutokea
Sio yote yavutia,mengine vimeo pia
Umakini wa viwango,hiyo ndiyo zingatia
Achana na maringo,hayo ndo yazuzua
Waparamia korongo,ni kwanini wajutia
Sio yote yavutia.mengine vimeo pia.
Gari zuri kwenye yadi,hilo ndilo lazuzua
Yapo mengi kwa idadi, na ndani yametulia
Nje na ndani maridadi,jinsi yanavyovutia
Sio yote yavutia.mengine vimeo pia.
Teh tehe tehe! lol