Najuta kulipandia........

Najuta kulipandia........

Kloro wacha vioja, naomba nisaidie
Mwanzo ulitoa hoja, jipya nijipatie
Vipi tena wakoroga, lazama jichukulie
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Safari siwezi fika, kwa gari ilo chakavu
Je vipi likipinduka, nikavunja zangu mbavu
Nataka la uhakika, mimi dereva shupavu
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Gari zilizotumika, vishindo hazihimili
Vipi utasafirika, kuweka gia ya pili
Mwishowe taghadhibika, yanini nijikatili
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

kila niliyoliona, zamani lilitumika
Ukitaka piga kona, gari lafanya koroma
Kwa kweli mtaminyana, bado gari litagoma
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Hivi mpya ziwapi, kote nimehangaika
Mengi ya sasa makapi, yaani ni patashika
Maisha sasa mafupi, madereva twatabika
Mwanzoni ulinambia jipya nijipatie




Hahaha mkuu kloro nachapa usingizi nitarudi kesho tuendeleze hii mada
 
Mimi dereva makini, hapa ninakuambia
Nimefuzu marekani, vitendo nimepitia
Na walipo nisaili, vyeti walinipatia
vipi wapindisha mada, dereva wanidhania

Udereva nilifuzu, na sasa nahudumia
Mimi si kama mazuzu, mtaalamu wa gia
Mfano ndizi mzuzu, kisimamishwa walia
vipi wapindisha mada, dereva wanidhania

Nimeendesha angani, hata vifaru vitani
Malori barabarani, na meli za bandarini
Mimi bingwa wa medani, mebobea ujuzini
vipi wapindisha mada, dereva wanidhania

Litazame lile gari, na mengi utagundua
Lilikuwa ni hatari, mashine ilizingua
Sikuwa nayo hiari, hata nilipo kagua
Vipi wapindisha mada dereva wanidhania

vipi taendesha gari, kwa kati lachuruzika
Uko wapi ufahari, huenda ningedhurika
Hebu wewe tafakari, je ni kweli ningefika
vipi wapindisha mada, dereva wanidhania


Tehetehe.......mkuu nimependa mistari yako naona una wasi wasi na dereva

Nina wasiwasi na derevea...

Dereva e ndugu yangu, eleza ulikosoma,
Elmu yatoa ukungu,sharti uishike vema,
Ni kama wa ndizi mkungu, hakika utasimama,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Vyuo vya uchochoroni, na NIT hapo ubungo,
Vingine vya redioni, havichemshi ubongo,
Hawapo barabarani, kuonesha kwa vitendo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Leseni kila aina, wewe yakwako ni ipi,
Ulipata kiaina, eleza lipata vipi,
Tupe ujumbe kwa kina, sije lipata ka pipi,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Kuna za makaratasi, leo zipo za kuswapu,
Karatasi ka patasi, lazima pige pushapu,
Najua hata wa Nkasi, lifika zama kishapu,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Alikuletea mjomba, jasho hata hukutoa,
Ukiendesha ka komba, kote kote unayumba,
Hata nyepesi ka pamba, wasiwasi nakushika,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?

Lengo kukuelimisha, haya mambo ni mafunzo,
Naona ulichemsha, mtaani meacha gumzo,
Jaribu kubadilisha, mbinu kuondoa mzozo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
 
MAGULUMANGU

Sindano mwana wa ganzi, magulu ninakuita
Nasubiri zako tenzi, uniondoe utata
Na sote tuwakufunzi, je nani wakutupata
E ndugu magulumangu, mistari sijapata

Mistari sijapata, nini unachongojea
Irushe yako karata, zinifike zako hoja
kichelewa takufata, lengo ni tuwe pamoja
E ndugu magulumangu, mistari sijapata

Sindano mwana wa ganzi
 
Kloro wacha vioja, naomba nisaidie
Mwanzo ulitoa hoja, jipya nijipatie
Vipi tena wakoroga, lazama jichukulie
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Safari siwezi fika, kwa gari ilo chakavu
Je vipi likipinduka, nikavunja zangu mbavu
Nataka la uhakika, mimi dereva shupavu
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Gari zilizotumika, vishindo hazihimili
Vipi utasafirika, kuweka gia ya pili
Mwishowe taghadhibika, yanini nijikatili
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

kila niliyoliona, zamani lilitumika
Ukitaka piga kona, gari lafanya koroma
Kwa kweli mtaminyana, bado gari litagoma
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie

Hivi mpya ziwapi, kote nimehangaika
Mengi ya sasa makapi, yaani ni patashika
Maisha sasa mafupi, madereva twatabika
Mwanzoni ulinambia jipya nijipatie

Jipya likipatikana, hilo la mwanzo chaguo
Kwavile adimu sana, umethibitisha hilo
Iweje tena wakana, lilotumika chipuo
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Ulikiri kudanganywa, eti jipya latoka japani
Mapesa ukanyang'anywa, kumbe lavuja jamani
Sasa nini kitafanywa , nimekwama klorokwini
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Kuna yale ya zamani, madhubuti nakwambia
Jinale volkswageni , kwa safari aminia
Hata kipata Nissani, Wala hutoijutia
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Karata nairejesha, kwako ewe wa ganzi
Meshindwa kusuluhisha, ni gumu lako chaguzi
Nachelea kuchemsha, bora fanya maamuzi
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
 
Ninaomba nielewe, sinione mtukutu
Na wala sina kiwewe, nazijua jadi zetu
Iweje mwenzangu wewe, huoni palipo kutu
Na kama sijafikishwa, nini faida ya gari

Vipi ninakwenda moro, gari laishia kibaha
Huoni kuna kasoro, nimepoteza shabaha
Mimi sitaki viporo, kufikishwa ndo raha
Na kama sijafikishwa, nini faida ya gari

Safari kufika nusu, huo sawa na mkosi
Hata upate mabusu, kalimati na misosi
safari haijakifu, ila gari lapiga. 'misi'
Kama sijafikishwa, nini faida ya gari

Kuna hoja umetoa, kuhusu yale ya zama
Yale kweli yako poa, hata ukiyatizama
mashine hazina doa, hata chini ukizama
Na kama sijafikishwa, nini faida ya gari

Labda ungenieleza, lazama tapata wapi
Nisije nikateleza, nikauziwa makapi
Fanya na kupeleleza, tujue ni pesa ngapi
Na kama sijafikishwa, nini faida ya gari


sindano mwana wa ganzi



Jipya likipatikana, hilo la mwanzo chaguo
Kwavile adimu sana, umethibitisha hilo
Iweje tena wakana, lilotumika chipuo
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Ulikiri kudanganywa, eti jipya latoka japani
Mapesa ukanyang'anywa, kumbe lavuja jamani
Sasa nini kitafanywa , nimekwama klorokwini
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Kuna yale ya zamani, madhubuti nakwambia
Jinale volkswageni , kwa safari aminia
Hata kipata Nissani, Wala hutoijutia
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?

Karata nairejesha, kwako ewe wa ganzi
Meshindwa kusuluhisha, ni gumu lako chaguzi
Nachelea kuchemsha, bora fanya maamuzi
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
 
U wapi asprini

Mkongwe ninakuita, mtaalamu wa fani
Mbona hapa hujapita, wewe mwalimu wa ghani
Mwenzio leo najuta, nilikumbwa tafrani
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini

Malenga wameshasema, mengi kunisaidia
kweli sijisikii vyema, mchango nahitajia
Hiki sasa ni kilema, injini zinafojiwa
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini

sindano mwana wa ganzi
 
Ninauliza wakuu, hapa mwajadili nini?
Hoja hii kuukuu, nimeikuta njiani,
Nashindwa kuwanukuu, nitakwamia njiani,
Hili gari gari gani, mnalojadili hapa?

Ni gari la matairi, Ya mpira au chuma,
Gari ni la kifahari, Au mpaka kusukuma?
Je ni gari ferari, Au haya ya kubuma?
Hili gari gari gani, mnalojadili hapa?
 
kweli wewe ni great thinker.

Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari hili lavutia, kwa hilo nakubalia
Rangi yake kahawia, machoni imetulia
Wengi wanaliwazia, na sifa kulisifia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kilitazama kwa mbele, pembeni limetanuka
Utapatwa na vipele, mwilini kusisimka
Natetemekwa vidole, nikipanda sita shuka
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kwa nyuma linapendeza, napenda wake mbinuko
Na mwendo likiongeza, lapepea kama puto
Ni kweli sijalikweza, gari hili moto moto
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Muda nilipo patia, gari hili nilipanda
Tena nikashikilia, katikati nikatanda
Kelele nilisikia, ila gari halikwenda
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari lilikakamaa, lilishindwa nifikisha
Pale nilipo tazama, mafuta linavujisha
Si kama nalisakama, mashineni kulitisha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Nimebaki na majuto, gari limekinaisha
Sina tena ule moto, wa gari kulipaisha
Mwili bado umzito, bora nisinge liwasha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Bora kupanda bajaji, popote wajipitia
Hazina mwingi mtaji, injini ni ndogo pia
Beteri ukisha chaji, wajitambia na njia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

KLORO na SPRINI, mwaonaje hii hoja
SHOSI naye WAKIJIJI, mchango wenu nangoja
MAGULU uko kundini, LIZZY pia tupamoja
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Na wote nisowataja, msiache kuchangia
Nipeni nyingi faraja, hoja sitapuuzia
Safari niloipanga, katu haikutimia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia


Malenga wenu

Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)
 
U wapi asprini

Mkongwe ninakuita, mtaalamu wa fani
Mbona hapa hujapita, wewe mwalimu wa ghani
Mwenzio leo najuta, nilikumbwa tafrani
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini

Malenga wameshasema, mengi kunisaidia
kweli sijisikii vyema, mchango nahitajia
Hiki sasa ni kilema, injini zinafojiwa
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini

sindano mwana wa ganzi

Salamu Yakuonea, Sikukukwepa garini,
Linifika ya dunia,Nikaenda safarini,
Mpendwa kumfukia, kwa udongo kaburini,
Mungu amlaze pema, Kaka yangu kwa amani.

Tukirudia hojani, Gari kuzungumzia,
Hilo gari ni la nani, naomba kuulizia,
Je ni lako la ndani, au umekodishia,
Shuka upande jingine, Safari yaendelea.

Sikutie ajalini, gari ulokodishia,
Au peleka sokoni, kama lako linunua,
Likuumize kwanini, Uteseke na dunia,
Nunua gari jingine, Safari iendelee.

Magari tele dukani, hilo acha ng'ang'ania,
Kakuasa klorokwini, nami ninamuungia,
Epukazo tafurani, na gari nalosumbua,
Chukua gari jingine, Safari yakungojea.
 
Hilo gari used au brand new?? Natania bana

Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa
didy service station iko kwa ajili yako
 
Pole yangu sipirini, kwa kaka uliyezika
Huo kweli mtihani, najua wataabika
wala siwe majozini, kwa mola ameshafika
Pole ewe ndugu yangu, kwa kaka uliyezika

Apangalo mola huwa, vitabu vina andika
Si lazima kuugua, mauti yakishafika
Tuzidishe zetu dua, apate kupumzika
Pole ewe ndugu yangu, kwa kaka uliyezika

nimebanwa kidogo nitarudi na mada ya gari.........

sindano mwana wa ganzi


Salamu Yakuonea, Sikukukwepa garini,
Linifika ya dunia,Nikaenda safarini,
Mpendwa kumfukia, kwa udongo kaburini,
Mungu amlaze pema, Kaka yangu kwa amani.

Tukirudia hojani, Gari kuzungumzia,
Hilo gari ni la nani, naomba kuulizia,
Je ni lako la ndani, au umekodishia,
Shuka upande jingine, Safari yaendelea.

Sikutie ajalini, gari ulokodishia,
Au peleka sokoni, kama lako linunua,
Likuumize kwanini, Uteseke na dunia,
Nunua gari jingine, Safari iendelee.

Magari tele dukani, hilo acha ng'ang'ania,
Kakuasa klorokwini, nami ninamuungia,
Epukazo tafurani, na gari nalosumbua,
Chukua gari jingine, Safari yakungojea.
 
Hivi kweli viloja,walai na waambia.
Kati sijawai ona,wala masikio kusikia.
Dereva ana lalama,ati gari kumfia.
Na uliza tena,chuo gani umepitia?

Aibu wala huna,majigambo una yatia.
marekani umesoma,vyeti wame kugawia.
Vyombo vyete waendesha,Huku umesimamia.
Wasiwasi nime tia,Ngandya kumkumbatia.

Jitulize tuli kijana,darasani sasa nakutia.
Bora ngeshika supana,boliti kuzi fungua.
Uwoga uka ondoa,matatizo garini kuchungua.
Maji kwenye rejeta hiyo yake asilia.

istizahi ukazifanya,gari kulitukania.
Injini ili kupozwa,maji yana hitajika.
kau kau rejeta,gia hazita ingia.
kabla ya kuendesha,gereji ungepitia.

kupanda na kuendesha,haitoshi nakuambia.
Gari lako ukipata,mifumo utaijua.
upozaji wa rejeta,umeme taa kuwashia.
Oili kuongezea,vyuma visije chubua.
 
Gari hili si la kwangu, ndugu ninakuambia
Liliona toka tangu, nikataka jipandia
Na wala si la mafungu, kweli ninakuapia
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa

Kupanda la pili si hoja, ubora ndo zingatio
Mengi ya sasa viroja, kufika ndo kusudio
Sitaki safari moja, nizugishwe na vilio
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa

kwa nje yanavutia, machoni tatamania
Mikono ukishatia, ndani kujichunguzia
Tashindwa kuaminia, tafiti utanambia
Lipi sasa nitapanda, mengi mechakachuliwa


sindano mwana wa ganzi


Salamu Yakuonea, Sikukukwepa garini,
Linifika ya dunia,Nikaenda safarini,
Mpendwa kumfukia, kwa udongo kaburini,
Mungu amlaze pema, Kaka yangu kwa amani.

Tukirudia hojani, Gari kuzungumzia,
Hilo gari ni la nani, naomba kuulizia,
Je ni lako la ndani, au umekodishia,
Shuka upande jingine, Safari yaendelea.

Sikutie ajalini, gari ulokodishia,
Au peleka sokoni, kama lako linunua,
Likuumize kwanini, Uteseke na dunia,
Nunua gari jingine, Safari iendelee.

Magari tele dukani, hilo acha ng'ang'ania,
Kakuasa klorokwini, nami ninamuungia,
Epukazo tafurani, na gari nalosumbua,
Chukua gari jingine, Safari yakungojea.
 
Mikono nilizamisha, mashine kuikaguwa
Ndani yake ilitisha, wachina mechakachuwa
Hapa nakuhabarisha, nyingi sasa zazingua
Magari haya ya sasa, sipende kuaminia

Punguza kunilaumu, je hoja hujaijua?
Uache kunishutumu, sitaki la kushitua
mashine mejaa sumu, je waweza kupumua
Magari haya ya sasa, sipende kuaminia


Sindano mwana wa ganzi


Hivi kweli viloja,walai na waambia.
Kati sijawai ona,wala masikio kusikia.
Dereva ana lalama,ati gari kumfia.
Na uliza tena,chuo gani umepitia?

Aibu wala huna,majigambo una yatia.
marekani umesoma,vyeti wame kugawia.
Vyombo vyete waendesha,Huku umesimamia.
Wasiwasi nime tia,Ngandya kumkumbatia.

Jitulize tuli kijana,darasani sasa nakutia.
Bora ngeshika supana,boliti kuzi fungua.
Uwoga uka ondoa,matatizo garini kuchungua.
Maji kwenye rejeta hiyo yake asilia.

istizahi ukazifanya,gari kulitukania.
Injini ili kupozwa,maji yana hitajika.
kau kau rejeta,gia hazita ingia.
kabla ya kuendesha,gereji ungepitia.

kupanda na kuendesha,haitoshi nakuambia.
Gari lako ukipata,mifumo utaijua.
upozaji wa rejeta,umeme taa kuwashia.
Oili kuongezea,vyuma visije chubua.
 
Fumbo fumbia mjinga,
Mwelevu huling'amua
Tungo weka tata,
Vifungo ukafungia
Wala sizo palapata,
Kwa ukweli zimetua.
Wala sio kwadhihaka.
Sanda nina zisifia.
Ugwiji mie sina,
Wakijiji ani jua,
wala sikupata hinda
Hoja zako kufumbua,
Mabano siku fungua,
Gari uchi kuwachia,
Tenzi zangu maridhia,
Lako gari kusifia,
Ila kigugumizi napata,
Udereva hujajua.
 
Udereva si tatizo, e ndugu yangu sikia
Fungua na masikio, hoja hujaipatia
Sio waja mbio mbio, dereva wanidhania
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu

Mabovu wayatetea, njiani kusafiria
vipi tatuelezea, safari kikudodea
Ni mabaya mazoea, vundo kuukodolea
Mbona nilisha eleza, udereva nimefuzu


sindano mwana wa ganzi


Fumbo fumbia mjinga,
Mwelevu huling'amua
Tungo weka tata,
Vifungo ukafungia
Wala sizo palapata,
Kwa ukweli zimetua.
Wala sio kwadhihaka.
Sanda nina zisifia.
Ugwiji mie sina,
Wakijiji ani jua,
wala sikupata hinda
Hoja zako kufumbua,
Mabano siku fungua,
Gari uchi kuwachia,
Tenzi zangu maridhia,
Lako gari kusifia,
Ila kigugumizi napata,
Udereva hujajua.
 
Back
Top Bottom