Najuta kulipandia........

Najuta kulipandia........

Ninazidi kukushukuru, Kwa yote unayosema
waniongezea nuru, matuta kwangu umwema
Sidhani ninakufuru, ningependa lile jema
Gari nitalichunguza, safari nikiridhia

vipi watoa hoja, eti niache chunguzi
matuta acha viroja, si kwa gari zetu hizi
Dereva sio mmoja, zaendeshwa kiuwizi
Gari nitalichunguza, safari nikiridhia

kuna zibebazo taka, na zile za mnadani
Hizi zote ni mashaka, nimezishusha thamani
sio bora kupata, safari ni burudani
Gari nitalichunguza, safari nikiridhia

kuna makubwa malori, shehena yajibebea
sijaona yake kheri, biashara mebobea
Ni kama chungu shubiri, sithubutu jizolea
Gari nitalichunguza, safari nikiridhia

Kuna zile gari ndogo, zinaitwa gari bubu
zajali kitu kidogo, wengine waziabudu
Wateja wake vigogo, wazisifu zina mudu
Gari nitalichinguza, safari nikiridhia

Sindano mwana wa ganzi


Sindano mwana ganzi,sije leta msiba.
Ukayaleta majonzi,chozi silo tiba.
Kwa kuleta weredi,injini kuzi chunguza.
Waweza leta ufundi,wenzio kwisha chakachua.

Walikuwapo wakwezi,mabingwa wa kupalamia.
Miembe na minazi,wako juu kudandia.
Matawi yakawa telezi,ahera kwenda mapema.
Magari sio nazi,ikivunjwa unaona.

Japo kwenye yadi,utacheza patapotea.
Yapo ya toka enzi,rami yana chubua.
Jaifongo na Bedifodi,yang'aa kama Korola.
Upwa injini si kazi,dukani wenda nunua.

Waweza pata uchizi,ukweli kuja fahamu.
Kuna yale Mashangingi,bei milioni mia.
Injini ni za Bajaji,zile kutoka India.
Bora kuacha chunguzi,safari unapo ridhia.
 
Ha ha ha ha ha ha!unaogopa Malori ya kubeba shehena sio!!!???.....na ya kubeba taka he he he he he nayale ya mnadani................!!!!!lol

Umeniacha hoi!
 
Gari kama la kwangu ni wajibu kulifanyia service, si kila gari unayopanda unaifanyia service, kuna hizi taxi, gari za tours, mabasi ya humu humu mjini (daladala) na hata ya mikoani, hivi jamani ni nani anayepaswa kuhakikisha yako ktk hali nzuri kimatumizi? , nafikiri ni wamiliki wenyewe ndo wanapaswa kuyafanyia service, sie kazi yetu ni kupanda tu, haha haha......


Haha, we unajua kupanda tu?
 
Magari ya mnadani unapotaka kulinunua ndugu yangu kuwa muangalifu, mara nyingi yana hitilafu ndio maana wanakwambia kabisa ' IT IS SOLD AS IT IS', Na yale ya kwenye yadi watu wanaonekana kuyaaminia sana, well yanaweza kuwa na unafuu kulinganisha na yale ya mnada lkn inabidi uwe mwangalifu kweli, twende sasa..........


Sanda ninakuja tena, naomba nisikilize
kuna jambo nimeona, wala usilipuuze
si kama nakudanganya, nenda ukapeleleze
Magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

usizugwe na idadi, yanapokuwa 'pakini'
Sijaona la zaidi, moyoni hayajawini
uchache umaridadi, nduguyo siyaamini
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

Angalia breki nyuma, kabla kulinunua
usije pata kununa, kwa nyuma linasumbua
Ukadhani ni hujuma, kumbe hukupambanua
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

Injini zabadilidhwa, ya 'fuso' kwa ya 'nisani'
Lengo ni kuwaridisha, mnaokwenda yadini
kwa ndani yanang'arishwa, kumbe ni ya hali duni
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

sisemi yote ni duni, sanda hapa nielewe
Yapo yabebayo kuni, na mihogo ya wenyewe
kwa hili sikurubuni, Wateja yatafutiwe
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

sindano mwana wa ganzi


Ha ha ha ha ha ha!unaogopa Malori ya kubeba shehena sio!!!???.....na ya kubeba taka he he he he he nayale ya mnadani................!!!!!lol

Umeniacha hoi!
 
Magari ya mnadani unapotaka kulinunua ndugu yangu kuwa muangalifu, mara nyingi yana hitilafu ndio maana wanakwambia kabisa ' IT IS SOLD AS IT IS', Na yale ya kwenye yadi watu wanaonekana kuyaaminia sana, well yanaweza kuwa na unafuu kulinganisha na yale ya mnada lkn inabidi uwe mwangalifu kweli, twende sasa..........


Sanda ninakuja tena, naomba nisikilize
kuna jambo nimeona, wala usilipuuze
si kama nakudanganya, nenda ukapeleleze
Magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

usizugwe na idadi, yanapokuwa 'pakini'
Sijaona la zaidi, moyoni hayajawini
uchache umaridadi, nduguyo siyaamini
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

Angalia breki nyuma, kabla kulinunua
usije pata kununa, kwa nyuma linasumbua
Ukadhani ni hujuma, kumbe hukupambanua
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

Injini zabadilidhwa, ya 'fuso' kwa ya 'nisani'
Lengo ni kuwaridisha, mnaokwenda yadini
kwa ndani yanang'arishwa, kumbe ni ya hali duni
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

sisemi yote ni duni, sanda hapa nielewe
Yapo yabebayo kuni, na mihogo ya wenyewe
kwa hili sikurubuni, Wateja yatafutiwe
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli

sindano mwana wa ganzi

si ndani yanangarishwa,ni nje nakuambia,
tena huwa kama mchwa,ya china hata india,
akili yako mkichwa,kulipanda asilia,
Acha liitwe gari,pikipiki hata meri,
 
Magulu nakushukuru, jamvini kusogelea
Mbona ulisusa duru, wapi ulipotelea
Hoja zakosa nuru, wewe usipotokea
karibu tena karibu, ukumbi sasa ni wako

Ni kipi kilikupata, tafadhali elezea
wengi tulikutafuta, ndugu tumekuzoea
sasa mengi tutapata, magulu umerejea
Karibu tena karibu, ukumbi sasa ni wako

sindano mwana wa ganzi


MAGULUMANGU

Sindano mwana wa ganzi, magulu ninakuita
Nasubiri zako tenzi, uniondoe utata
Na sote tuwakufunzi, je nani wakutupata
E ndugu magulumangu, mistari sijapata

Mistari sijapata, nini unachongojea
Irushe yako karata, zinifike zako hoja
kichelewa takufata, lengo ni tuwe pamoja
E ndugu magulumangu, mistari sijapata

Sindano mwana wa ganzi
 
Punguza zako jazba,upate kunisikia
Si zile yadi za jaba,huko uende chukua
Kwakuwa ni kaitaba,eti waenda nunua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua


Kuna yale ya heshima,hata bei wayajua
Bora tumia hekima,uchague la kufaa
Ni aghali zake bima,hilo upate tambua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua

Punguza wako wahaka,natumai waelewa
Usijefanya haraka,utakamatwa na chewa
Pole pole ni Baraka,utapata ulopewa
Umakini watakiwa,si kila yadi watua






Ni vipi wayasifia, magari yale ya yadi
Mbwembwe wayamiminia, kuwa ni yamaridadi
Ulaya lishatumia, na sasa hayana hadhi
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo

Elfu kwa maelfu, maili yametembea
Huku kwetu twayasifu, mjini twagereshea
Huu kwangu ni upofu, ya yadi nayabezea
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo

Dereva walisha kaa, ndani wakayaendesha
Yalivyo pata chakaa, kwetu wakayasogesha
Mie leo nashangaa, wengi yawahamasisha
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo


sindano mwana wa ganzi
 
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari hili lavutia, kwa hilo nakubalia
Rangi yake kahawia, machoni imetulia
Wengi wanaliwazia, na sifa kulisifia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kilitazama kwa mbele, pembeni limetanuka
Utapatwa na vipele, mwilini kusisimka
Natetemekwa vidole, nikipanda sita shuka
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Kwa nyuma linapendeza, napenda wake mbinuko
Na mwendo likiongeza, lapepea kama puto
Ni kweli sijalikweza, gari hili moto moto
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Muda nilipo patia, gari hili nilipanda
Tena nikashikilia, katikati nikatanda
Kelele nilisikia, ila gari halikwenda
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Gari lilikakamaa, lilishindwa nifikisha
Pale nilipo tazama, mafuta linavujisha
Si kama nalisakama, mashineni kulitisha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Nimebaki na majuto, gari limekinaisha
Sina tena ule moto, wa gari kulipaisha
Mwili bado umzito, bora nisinge liwasha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Bora kupanda bajaji, popote wajipitia
Hazina mwingi mtaji, injini ni ndogo pia
Beteri ukisha chaji, wajitambia na njia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

KLORO na SPRINI, mwaonaje hii hoja
SHOSI naye WAKIJIJI, mchango wenu nangoja
MAGULU uko kundini, LIZZY pia tupamoja
Gari hili gari gani, najuta kulipandia

Na wote nisowataja, msiache kuchangia
Nipeni nyingi faraja, hoja sitapuuzia
Safari niloipanga, katu haikutimia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia


Malenga wenu

Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)

Twashukuru Yakuonea.,
Maneno kuntu kutugea;
Ushairi kutumia;
Lugha yetu kukuzia...!
 
Hilo gari used au brand new?? Natania bana

Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa

Hata kama ni used au brand new, usipokuwa mwangalifu majority yako hivyo. Hakuna cha service bali bahati tu. Ndio ulimwengu wa kileo.
 
Yadi hizi yadi gani, unazo zungumzia
Ni zile za baniani, ya zama watuuzia
Au hizi za njiani, ilala na mwenge pia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Hata kikuta pajero, sio walikimbilia
wasema kipenda roho, wadhani utatulia
Litakupa mgogoro, majuto utajutia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Benzi gari ya makini, dunia inatambia
Leo iweje kundini, yadini watuuzia
Hapa kuna ulakini, kiwango imechujia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Yangu nitainunua, mpya toka kwa 'dila'
Popote tatanulia, mashine haina hila
Pozi nitawazidia, za yadi zina msala
Gari nyingi yadini, zina viwango vyake ni duni

Msiojuwa viwango, za yadi mwang'ang'ania
Ondoa yako matongo, hayo walishatumia
Kaulize kule ng'ambo, huku wameyatupia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni


sindano mwana wa ganzi


Punguza zako jazba,upate kunisikia
Si zile yadi za jaba,huko uende chukua
Kwakuwa ni kaitaba,eti waenda nunua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua


Kuna yale ya heshima,hata bei wayajua
Bora tumia hekima,uchague la kufaa
Ni aghali zake bima,hilo upate tambua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua

Punguza wako wahaka,natumai waelewa
Usijefanya haraka,utakamatwa na chewa
Pole pole ni Baraka,utapata ulopewa
Umakini watakiwa,si kila yadi watua
 
Nami ni ninakushukuru, kwa hilo ulochangia
Mola atakunusuru, mema atakupatia
Maisha yawe ya nuru, kwako na wazazi pia
e ndugu mndumsolo, nakushukuru kwa dhati

Twashukuru Yakuonea.,
Maneno kuntu kutugea;
Ushairi kutumia;
Lugha yetu kukuzia...!
 
Hata kama ni used au brand new, usipokuwa mwangalifu majority yako hivyo. Hakuna cha service bali bahati tu. Ndio ulimwengu wa kileo.

hapa nagonga senksi umesema kweeeliii.........
 
wamesema waswahili,kupanga ni kuchagua
Uepuke ubahili,gari lako kununua
Sije kuwa la wawili,mwisho kaja kujutia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa

Nimeona kiwandani,wazi ya kijaribiwa
Wamejaribu nje ndani,bila wewe kuelewa
Wamepata burudani,kabla wewe kuletewa
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa

Sikila 'dila' minifu,hapo takuja jutia
Wengine wadanganyifu,wataka kuyapitia
Wamezidi maradufu,ufisadi kufanyia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa





Yadi hizi yadi gani, unazo zungumzia
Ni zile za baniani, ya zama watuuzia
Au hizi za njiani, ilala na mwenge pia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Hata kikuta pajero, sio walikimbilia
wasema kipenda roho, wadhani utatulia
Litakupa mgogoro, majuto utajutia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Benzi gari ya makini, dunia inatambia
Leo iweje kundini, yadini watuuzia
Hapa kuna ulakini, kiwango imechujia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni

Yangu nitainunua, mpya toka kwa 'dila'
Popote tatanulia, mashine haina hila
Pozi nitawazidia, za yadi zina msala
Gari nyingi yadini, zina viwango vyake ni duni

Msiojuwa viwango, za yadi mwang'ang'ania
Ondoa yako matongo, hayo walishatumia
Kaulize kule ng'ambo, huku wameyatupia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni


sindano mwana wa ganzi
 
Sasa hapo ndo utajua mchina ni balaaa muziki mpaka kwenye bodaboda, hata mimi ile gari niliyoshindwa kusafirika nayo nafikiri kulikuwa na mikono ya wachina, maana kwa jinsi ilivyokuwa inaonekana usingedhani kama mashine iko vile


Hiyo gari gari gani, unayoisema wewe?
Ukute hujui gari, ndo sababu ya kiwewe
Kumbe wewe wa bajaji, gari kwako vipi wewe?
Rudia wako usafiri, siparamie vya wenyewe!
 
Wewe umepewa lifti, mbio kupiga honi
Ni lazima uwe fiti, bila kuona soni
usije pigwa shuti, uone bora mkokoteni
unajuta kulipandia, kwani ulipandishwa?

Nunua gari lako, uli customize nakwambia
liwe la aina yako, uturi kulipakia
wasilete shokoshoko, wezi kujipakia
huwezi lipiga mnada, kwa jinsi utavolipenda
 
Jidu wanifurahisha, magari hujajulia
kiwango ninakushusha, ya yadi umezoea
Gari likijaribishwa, upya umeshapotea
Zile zijabirishwazo, zaitwa gari za 'demo'

Gari unalinunua, 'maileji' iko zero
kama ni kulichubua, takuwa yako mikono
Hakuna kuchakachua, viwango ndio kipimo
zile zijaribishwazo, zaitwa gari za 'demo'

Jipya halitakuwa, njiani likishatinga
Thamani litatolewa, watauziwa wajinga
'waranti' hutagaiwa, huwezi hata kuringa
Zile zijaribishwazo, zaitwa gari za 'demo'



Sindano mwana wa ganzi


wamesema waswahili,kupanga ni kuchagua
Uepuke ubahili,gari lako kununua
Sije kuwa la wawili,mwisho kaja kujutia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa

Nimeona kiwandani,wazi ya kijaribiwa
Wamejaribu nje ndani,bila wewe kuelewa
Wamepata burudani,kabla wewe kuletewa
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa

Sikila 'dila' minifu,hapo takuja jutia
Wengine wadanganyifu,wataka kuyapitia
Wamezidi maradufu,ufisadi kufanyia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa
 
Gari ninazijulia, udereva ndo fani
kwa kati nikikalia, gia kuzitia ndani
Iweje wanisagia, Tausi acha utani
magari ya siku hizi, mengi mshike mshike

sindano mwana wa ganzi



Hiyo gari gari gani, unayoisema wewe?
Ukute hujui gari, ndo sababu ya kiwewe
Kumbe wewe wa bajaji, gari kwako vipi wewe?
Rudia wako usafiri, siparamie vya wenyewe!
 
Wewe umepewa lifti, mbio kupiga honi
Ni lazima uwe fiti, bila kuona soni
usije pigwa shuti, uone bora mkokoteni
unajuta kulipandia, kwani ulipandishwa?

Nunua gari lako, uli customize nakwambia
liwe la aina yako, uturi kulipakia
wasilete shokoshoko, wezi kujipakia
huwezi lipiga mnada, kwa jinsi utavolipenda


This is one of the reason why i always admire you hahaha...... nimependa mistari mama.........Sitaki gari ya customize bana, nataka gari itakayokuwa na factory fitted accessories, huku ku- custimize ndo mwazo wa kuchakachua unakuta benzi ina injini ya bajaji
 
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia


Malenga wenu

Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)


Salamu nawatumia, magwiji mlochangia,
Swali nimelipitia, majibu yanavutia,
Nami nikaazimia, ujumbe kuwapatia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Muda nimeutumia, swali kulifikiria,
Ndipo iliponijia, hadi nikashangilia,
Jibu nikalipatia, la fumbo alilofumbia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Linafanana na kia, ndivyo ametuambia,
Gharama ni rahisia, si ghali tumesikia,
Miye namkubalia, la chee kalipandia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

La rangi ya kahawia, gari akalisifia,
Magari tunajulia, hakuna ya kahawia,
Ni mbao kazisifia, mkokoteni karukia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Tena akatuambia, mbele limetanukia,
Lipi liko kama kia, mbele limejiachia?
Yale ya kusukumia, kwa mbele na nyuma pia,
Gari siyo gari “lile”!
Gari ni mkokoteni!

Nyuma akalisifia, mbinuko unavutia,
Wallahi sijasikia, gari linabinukia,
Jinsi ninavyojulia, mkokoteni kasifia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Tena akalipandia, kati akajiachia,
Wapi umeshasikia, kupanda ukatandia,
Mkokoteni ukipandia, kati utatanulia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Gari alilopandia, kelele alisikia,
Mbele halikuhamia, kashindwa kusukumia,
Limekosa girisia, mkweche kaudandia!
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Pole ninakugaia, kwa uliyojitakia,
Gari ulilopandia, si gari nakuambia,
Tairi zilizugia, wewe ukalidandia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Kelele ulizosikia, mgosi anavutia,
Wewe ukafikiria, benzi umelidandia,
Nne ukajikunjia, sigara unavutia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni.

Safari ikikujia, kwanza anza ulizia,
Tafiti na tafutia, kabla hujalidandia,
Ujue kama ni kia, au lori la skania,
Gari siyo gari lile,
Ni gari mkokoteni!

Beti ninaziachia, fumbo nimefumbulia,
Natumai utaachia, gari la kufikiria,
Kisha utajipangia, la ukweli kupatia,
Gari ulilodandia,
Ni gari mkokoteni!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Back
Top Bottom