Najuta kumkaribisha demu wangu JF

Najuta kumkaribisha demu wangu JF

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Demu wangu hakuwa hata anajua kama duniani kuna jukwaa la JF,

Nikamshawishi ajiunge na akajiunga, tokea ajiunge wanajukwaa wengi wa kiume wamekuwa wakimsumbua sana kwa pm, wakipiga mistari,

Wengine wamefikia hatua hadi ya kumtumia namba za simu, nikitembelea profile yake nakuta vistors kibao wa kiume.

Kama mnavyojua miluzi mingi humpoteza mbwa, ninahofu anaweza nipotea kwa mtindo huu, kinachonitisha zaidi niliamua kutengeneza ID asiyoijua nami nikaanza kumtongoza, kanitumia namba yake na ninachat naye sana na ameshaonesha dalili zote za kunikubali, mtihani ni kuonana naye, naogopa kuweka appointment halafu kweli atokee, nitazimia.
 
Kama ulimpatia kwenye hii mitandao ya kijamii ni halali yako kusema ivyo.
 
Si ushasema ni demu tu sasa kama unataka kujua yaliyomo weka appointment na akija jidai we kama vile umepita hapo kumcheki mshikaji wako one time then muulize anafanya nini hapo!!!????

Usikae sana muage timka yeye akiwepo uone reaction yake then mtumie text kuwa arudi home as umekamilisha zoezi lako!!!!!!!

Halafu fanya yauridhishayo moyo wako sababu ukweli utakuwa nao!!!!!!!
 
Teh teh teh ama kweli neno ningejuaaaaaaaaaaa huja mwisho wa safari
 
Kizuri kula na nduguzo kama kibaya kula mwenyewe. Ile kitu siyo uwanja, nyumba au gari aina hati miliki atiii!!!!
 
duh pole, ila inaonekana unampenda sana, me nafikiri mueleze ulichogundua na ambavyo umesikitishwa na kukosa kabisa imani nae, then majibu yake baada ya hapo ndo yatakupa kusuka au kunyoa
 
Demu wangu hakuwa hata anajua kama duniani kuna jukwaa la JF, nikamshawishi ajiunge na akajiunga, tokea ajiunge wanajukwaa wengi wa kiume wamekuwa wakimsumbua sana kwa pm, wakipiga mistari, wengine wamefikia hatua hadi ya kumtumia namba za simu, nikitembelea profile yake nakuta vistors kibao wa kiume. Kama mnavyojua miluzi mingi humpoteza mbwa, ninahofu anaweza nipotea kwa mtindo huu, kinachonitisha zaidi niliamua kutengeneza ID asiyoijua nami nikaanza kumtongoza, kanitumia namba yake na ninachat naye sana na ameshaonesha dalili zote za kunikubali, mtihani ni kuonana naye, naogopa kuweka appointment halafu kweli atokee, nitazimia.
Kwa nini umemfananisha na mbwa, alafu unamuogopa mbwa usizimie ?!!!!!!?
 
sasa mbona kaishasoma hapa! au ndo ulikuwa unamfikishia ujumbe kiaina?
 
Ukiona demu wako anatongozwa jisifie sana either ni mkarimu or ni mrembo sana,hongera sana

kwa mfano wewe ntakutongoza sababu ya urembo wako. forget about ukarimu, waweza japo kunifikiria?
 
Si ushasema ni demu tu sasa kama unataka kujua yaliyomo weka appointment na akija jidai we kama vile umepita hapo kumcheki mshikaji wako one time then muulize anafanya nini hapo!!!????

Usikae sana muage timka yeye akiwepo uone reaction yake then mtumie text kuwa arudi home as umekamilisha zoezi lako!!!!!!!

Halafu fanya yauridhishayo moyo wako sababu ukweli utakuwa nao!!!!!!!

Olesaidimu kamaliza kila kitu.
 
Chakukufanya uzimie nikipi? sasa umekuja hapa kumu alert kua unajua au unamtishia nyau mtumzima mwenzio?
 
Back
Top Bottom