Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Sasa we dogo mpaka unaoa mwanamke aliyezaa tayari hukuona mabinti ambao bado hawajazaa uoe? Hawa masingo maza wana watu wao wa kuwaoa, huolewa na majibaba yaliyoachwa na wake zao au huongezwa wake wa pili tatu au vimada tu. Jibaba lenye mtoto/watoto halijuti kuoa singo maza kwa kuwa nalo lina mtoto/tayari, na kama mke aliondoka na mtoto/watoto huanza upya kuishi na single mother mwenye mtoto/watoto. Wanaume wengi hupendelea wenye idadi ya watoto isiyozidi watoto walio nao tayari na pia hutegemea hali ya afya ya mwili na akili ikoje ongeza na hali ya uchumi wa single mothera ikoje
 
Nichukue fursa hii kuandika kwamba single mother wanaoleka vema tu, ni wanawake kama wanawake wengine wenye sifa za kuolewa. Wanaolewa bila kujali idadi ya watotn walio nao mradi tu wanakidhi vipengele vya sifa za kuwa wife material
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako huu Kiongozi. Najuta sana kufanya hili Kosa ukizingatia Mimi Sina mtoto nje. Sijui nilijichanganya vipi? But baado nna mda naamini nitarekebisha.
Pole sana, ila kwenye kufanya maamuzi vaa pia viatu vya huyo dada wa watu, uliemchukua kwao kwa heshima unamuacha kisa mtoto ambae ulimkuta nae na ukakubaliana na hali halisi.
Usifanye maamuzi kutokana na hisia, safiri hata ukae mbali na familia kidogo ukiwa unatafuta maamuzi sahihi mkuu
Mungu akuongoze ukafanye lililo sahihi kwako na kwa mkeo.
 
Unakutana na binti mzuri kakamilika idara zote, utaanzaje kumkataa kumuoa kama anataka ndoa kisa tu ana mtoto? Huyo mtoto inawezekana muhuni alimuotea alikuwa anapita tu bila kuoa mara paap binti kanasa mimba na hakuitoa. Ukute muhuni hana taimu na mtoto wake au binti hajui baba wa mtoto alipo, muhuni alikula mara moja tu akapotea kusikojulikana. Hata kama muhuni anajulikana alipo poa tu akitaka kuja kuchukua mtoto wake achukue tu ila kupasha kiporo ni marufuku
 
Kalee tu mwana kata kubariki sana.
 
Back
Top Bottom