Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Mbona mkuu huna sababu za ku hate huyo.mtoto , na huna sababu za kumchukia huyo mama maan huna sababu za msingi zaid ya selfish

Ila kama ulilogwa kuoa labda lakn hakuna baya kwakuw hakuna changamoto za msingi za kujuta

Usimchafue single mother wawatu wajibika kwakuw ulijua kbs ana mtoto na uli accept
Nimejilazimisha kumpenda huyu mtoto lakini nimeshindwa.
 
Nafsi mkuu haikubali.....hasa pale unakuta Dogo anaumwa hamjalala usiku kucha. Ila unasikia Baba yake jana alikuwa kalewa anagombana na Bar Maid.

Lakini Mtoto anaitwa kwa jina la mlevi sio lako wewe unayehustle.
Watu wengi tu mkuu wamelelewa na wazazi sio wao hadi wamefikia mafanikio.
Huyo baba mlevi ni wazi hataweza kumjengea njia nzuri mwanae hivyo kama una nafasi na mtoto yupo poa fanya hivyo.
Nimesoma na watu wengi tu wa familia moja ila majina ya mwisho yanatofautiana. Muhimu ile hali ya upendo na undugu ilikuwepo.
 
ukiachana na mtoto huyo single mother anachangamoto gani nyingine? je,

1. anampelekaga mtoto kwa baba yake?

2. Anakunyima sakrament?

3. Mapenzi yake yameegemea wapi zaidi?
1&2 Hana shida 3 mapenzi yake yapo kwa mtoto zaidi kuliko Mimi. Hii inanifanya nifikirie mbali sana.
 
Watu wengi tu mkuu wamelelewa na wazazi sio wao hadi wamefikia mafanikio.
Huyo baba mlevi ni wazi hataweza kumjengea njia nzuri mwanae hivyo kama una nafasi na mtoto yupo poa fanya hivyo.
Nimesoma na watu wengi tu wa familia moja ila majina ya mwisho yanatofautiana. Muhimu ile hali ya upendo na undugu ilikuwepo.
Unajua ́maumivu aliyopitia Mama yake au baba yqke wa kambo?
Msichukulie mambo poa
 
WanaJF
Habari zenu, heri ya Ramadan na Kwaresma, matumaini yangu wote wazima, waliyo na changamoto Mungu akawape njia.

Ni kijana barubaru wa miaka 28 mwenye nguvu na Afya.

Wakuu kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyo jieleza, nilioa huyu single mother mwaka mmoja uliyo pita baada ya kujiridhisha tabia zake zinafaa kuwa mke na mm bila hiyana nikachukua nikaweka ndani, nikatia pamba maskioni kuzuia kelele za "KUOGOPA SINGLE MOTHER" kumbe nilikua najidanganya nafasi yangu.

Wakuu kila kukicha nikimtazama huyu mtoto wake Roho yangu inauma kwa uchungu wa majuto ya kuoa huyu single mother ni kama nilirogwa hivi kuoa huyu mwanamke, kivipi yaani natunza mbegu za mwanaume mwingine naye yupo tu anakula Bata at the end mtoto aje kunikana mimi siyo baba yake, kwanini hata sikuchukua mdogo wangu nikae naye , kuliko kuhudumia damu ambayo siyo yangu. Wakuu najuta sana.

Niwe Mkweli nafsi yangu inajuta sana. Nahitaji msaada wa kisaikolojia nijinasue kutoka hapa nilipo kwama, imefika hatua hata kukaa nyumban siwezi kabsa.
Pia naomba wale waliyo wai pitia hii situation walijinasuaje? Mnisaidie.
Aisee pole sanaa, kwa jinsi ulivyoandika inaonyesha kama kweli upo SERIOUS.
Kwa kweli hiyo scenario inahitaji moyo sanaa. Mimi nilikubali matokeo nilimpenda mdada mmoja alikuwa ni mwenye kila sifa ya kuwa mke lakini ilinibidi nimuache tuu kwa sababu AKILI ilikuwa inakataa kila nikilazimisha naona hii issue sina misuli ya kulibeba hili Suala. Ila nilimpenda sanaa na kweli alikuwa na heshima! Ila daaah...namlaumu sanaa yule aliyemuacha na mtoto wa kiume. Amemchafua mdada wa watu mzuri tuu! 😪😪😪
 
Mkuu tatizo ulilonalo ni la kisaikolojia zaidi, huenda unasoma sana threads zinazohusu single mother hapa JF au watu unaoishi nao kila siku wanatoa negative comments kuhusu single mother
Jitahidi sana ku control akili yako, kama huyo mwanamke hazingui komaa naye tuu, swala la huyo mtoto lisikuumize kichwa
 
Mwanaume mwenye mtoto hana shida sababu Baba ni yule yule.
Mwanamke mwenye mtoto ni shida sababu Baba ni tofauti
Angekuwa ni mwanamke ameolewa mwanaume mwenye mtoto akawa anapitia changamoto kama hizi ungetoa ushauri mwingine au ndo huu huu both sides?
ke
 
WanaJF
Habari zenu, heri ya Ramadan na Kwaresma, matumaini yangu wote wazima, waliyo na changamoto Mungu akawape njia.

Ni kijana barubaru wa miaka 28 mwenye nguvu na Afya.

Wakuu kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyo jieleza, nilioa huyu single mother mwaka mmoja uliyo pita baada ya kujiridhisha tabia zake zinafaa kuwa mke na mm bila hiyana nikachukua nikaweka ndani, nikatia pamba maskioni kuzuia kelele za "KUOGOPA SINGLE MOTHER" kumbe nilikua najidanganya nafasi yangu.

Wakuu kila kukicha nikimtazama huyu mtoto wake Roho yangu inauma kwa uchungu wa majuto ya kuoa huyu single mother ni kama nilirogwa hivi kuoa huyu mwanamke, kivipi yaani natunza mbegu za mwanaume mwingine naye yupo tu anakula Bata at the end mtoto aje kunikana mimi siyo baba yake, kwanini hata sikuchukua mdogo wangu nikae naye , kuliko kuhudumia damu ambayo siyo yangu. Wakuu najuta sana.

Niwe Mkweli nafsi yangu inajuta sana. Nahitaji msaada wa kisaikolojia nijinasue kutoka hapa nilipo kwama, imefika hatua hata kukaa nyumban siwezi kabsa.
Pia naomba wale waliyo wai pitia hii situation walijinasuaje? Mnisaidie.
1. Lakini kuhusu mtoto wake si uliliona kabla au ulishinikizwa?
2. Jambo unaloliwaza ni la mbele (probability). Kwann unahukumu mapema?
3. Ukiamua kufanya jambo jipe muda, tafakari halafu chukua maamuzi. Ni kama ulilazimishwa kuishi na single mother hivi.
 
Una roho mbaya, hapo unaangalia ugali wako tuuu. Wanaume hawako hivyo kuangalia food na minor thing kua achana na tabia za kike kuangalia nani analula ugali wako.
 
Back
Top Bottom