Najuta kupoteza muda wangu kuangalia Ujinga uliopo Kwenye series ya money heist

Mkuu inaonekana kwenye tasnia hii upo vizuri. Umeshuka nondo za maana.
Sasa hebu pendekeza series angalau tupotezepoteze muda kwa wkend hii

Series kali na tamu zenye maudhui kama pb 24hrs n.k
Mkuu sipendekezi bali nataja zile ambazo mimi nimeziangalia na zikanivutia! Naamini filamu/music is all about personal taste... nilizopenda mimi kwako zinaweza kuwa Upumbavu Mtupu kama mleta mada alivyosema kuhusu Money Heist!

Kwa nilizoangalia, nimezipenda zifuatazo:-

Spy Drama/Series and Related

1. The Americans:-


Kama hujaingilia, basi nitoe kwanza angalizo kabka hujatumia bundle yako!! Hii ni 100% SPY DRAMA with Spies operating in a foreign soil (KGB Spies in the US)!

Na kwavile ni 100% Spy Drama basi usitarajie yale ya 24 or from any action movie coz' that's not how spies operate in foreign country!

All in all, hiyo ndo my favorite Spy Series!

2. Homeland

Na yenyewe ni Spy Series! Hii actions zipo na ukiangalia how CIA now operates in the Middle East huwezi kushangaa kukuta actions though hapo juu nimesema that's not how spies work in a foreign soil work! Sababu kubwa bila shaka maeneo hayo ni unstable lakini kwa nchi kama Iran kwa mfano, there's no way CIA wanaweza kuwa violent kwa sababu hiyo itakuwa ni ku-blow cover yao! Na inapotokea violency basi ni through proxies.

Even in a real world kule ME, CIA wanakaanga mbuyu, wanawapa proxies!

3. The Spys (Mossad)... Is kinda boring lakini sababu ni zile zile ambazo nimetaja kwenye #1 hapo juu... that's how spies in foreign soil work!

4. Strike Back na Seal Team: Hizi nimezeweka pamoja kwa sababu ideas zinafanana! Special Military Unit inapewa mission most likely to a foreign soil, nao wanaenda ku-excute! Hawa ni Elite Soldiers and not pure spies, but huwezi kuwa na mission ng'ambo bila ya kuanza intelligence... for this matter military intelligence! And I hope you know what does soldiers do to their targets!

If it were me, I'd start with Strike Back from British Defence Intelligence Service.

5. S.W.A.T:- As the name suggests, hawa ni kikosi kazi cha LAPD na kazi zao ni kama za hao #4, the only difference wao mission zao ni ndani ya nchi huku ku-deal na district criminals!

6. The Blacklist: Hii sidhani kama inahitaji maelezo manake na yenyewe ni maarufu kama ilivyo 24

7. The Last Ship:- Dunia ilivyokuwa imetaharuki kuhusu COVID-19 ndicho kinatokea kwenye The Last Ship where Admiral Tom Chandler's led team ilikuwa kwenye mission ya kutafuta tiba dhidi ya serious pandemic ambayo ilishaangamiza 80% of world population!

Haikuwa mission rahisi kama kukaa maabara kufanyia utafiti sample hizi na zile, bali ilikuwa ni deadly mission k

8. Alias:- Good stuff to watch; hawa nilipenda sana idea yao ambapo Operatives wa SD-6 kwa muda mrefu waliamini wapo chini ya CIA kumbe ni SD-6 is just a criminal organization! Creator wa Alias ndie Creator wa Lost... kwahiyo kama umewahi kuingalia Lost basi nadhani unaweza kufanya maamuzi ikiwa the same creator anaweza kufanya kazi mzuri!!

9. Tom Clancy's Jack Ryan- Great Stuff to watch! Nilipenda sana pale walipotupia jicho nje ya maeneo yaliyozoeleka kama vile Middle East, Russia and Asia! Kwenye Season 2, walihamia Venezuela na ilikuwa ni bonge season. It's CIA Stuff!

10. Deep State... British Spy/Espionage series

11. Blindspot
: Good stuff too

12. Fauda... Israel Series! Sina shaka unafahamu tunapoitaja Israel mkono wa kulia basi kushoto kuna Palestine

13. Ozark... Bonge la show

14. Killing Eve... Good stuff

Political Drama. Hapa chini ni my favorite Political Drama

1. House of Cards

2. The West Wing

3. The Bodyguard

4. Scandal

5. Designated Survival

6. Ingobernable... Mexican

Crime Drama, and Drugs related

1. Sopranos... Mafia Stuff; one of the best series of all time.

2. Breaking Bad... Season 1 inaweza kukuboa, lakini ukivuka salama season 1, I guess hautajuta unless kama sio taste yako! Sawa na hiyo hapo juu, na yenyewe ni one of the best series of all time.

3. The Wire... Great series

4. Power... nashangaa kidogo watu wanavyoilalamikia Money Heist eti ina sex stuff za kumwaga, sasa Power sijui watasemaje, manake ilifikia hadi aunt yake 50Cents kum-text 50 "what's fvck is that? Why didn't you tell me"!! Shangazi ali-mind kuona dushe la mwanae live!!!

5. Queen of The South

6. Narcos

Legal Drama...

1. Suit

2. The Practice

Everything Else...

1. Empire... Music

2. Grey's Anatomy... Medical

3. The Good Doctor... Medical

4. Shameless... Comedy Drama

5. Silicon Valley... Comedy Drama from tech guys

6. Locked-up... Spanish series! Angalizo ni kwamba, hao waliokuwa locked up ni mademu, kwahiyo don't be surprised utakapokutana na mambo ya usagaji.

7. Orange is a New Black... It's American, but like #6 above.

8. Game of Throne... Fantasy Drama! Kama wewe ni mmishenari, na hupendi kuona tupu za waanadamu zinagusana, then don't watch it kwa sababu ni show inayozungumzia karne hizo ambazo mwanamke alikuwa anaonekana kama chombo tu cha kustarehesha.

Na yenyewe ni one of the greatest shows in history, huku ikiwa imezoa matuzo makubwa lukuki!

9. The Walking Dead... Zombies but great series.
 
Mkuu niseme tu hii package imeshiba sana.
Breakingbad nimeshaimaliza{kwa kuitizama zaidi ya maramoja}
Blacklist nipo season ya 7 ep 11
Strike back nmeishia season 2
Homeland ilinishinda sijui kwanini

Sasa nikimalizana na hizo naanza na hizo ulizonitajia hapo moja baada ya nyingine.

Shukrani sana
 
Homeland wengi iliwashinda, na wengine waliachana nayo a moment Sgt Brody aliouawa! Binafsi wakati mwingine huwa naangalia series just for learning... mazombi kwa mfano, hayo akina The Walking Dead, sio mishe zangu kabisa but wakati mwingine nalazimika kuangalia!

Nami kuna season moja sema tu siikumbuki, ilibaki kidogo tu niachane nayo kabla hawajaanza kupita tena kwenye njia zangu!
 
Inasemea LOST?
 
Umetisha aisee
 
Mkuu hukumsikia Makonda jana Kasema Esther Bulaya aliwa na Halima mdee
 
Hebu pendeoeza series nyingine tofauti na hizo ulizotaja.

Meanwhile... Angalia zifuatazo
Tredstne
Hanna

Zafaa kwakupotezea muda wakati tunasubiri series tamu nyinginezo
Hanna kama wine inaanza kwa kuboa kama huna subira unaweza acha ila ilivyochanganya sasa balaa.
 
Mkuu Umeelezea Kitaalamu sana,
 
Hii series tumepigwa mchana kweupe
 
Mjinga mmoja ametumia muda wake kipumbavu kuangalia ujinga wa wajinga wenzie ajabu wamekuja na wajinga wengine kumsapoti katika ujinga wao wote ni wajinga na huu pia mtaona ni ujinga kwa kua ni wajinga[emoji41] Kama unataka uhalisia usiangalie movie kachokoze polisi
 
Umeishia darasa la ngapi?
 
Money heist nilijilazimu kuiangalia kulingana na promo iliyokuwa inapewa lakn nilivyoanza tu kuiangalia nikaiona ya ovyo na hata sikumaliza episode zote hakuna series pale najuta kupoteza muda wangu mdogo kuangalia hizo episode na bando langu
 
Yeah angalau Banshee...
 

Nimeelewa wap nnapokosea kumbe ni perception yangu kichwani ya kutaka money heist iwe kama 24 au PB ndo inayonitesa aicee
 
Nimemaliza kuiangalia hii series kwakweli wamejitahidi sana ingawa sioni kama inaifikia Prison break

Na wala sio mbaya kama mleta mada anavyojaribu kueleza pia inaonekana mleta mada hakaelewe vizuri maudhui ya series haswa aliposema eti wameingia ndani na hawana mpango wowote wa kutoroka
Pia anaonekana kukereka na Tokyo kupigwa miti bila sababu ya msingi
 
Storyline yake sio mbaya. Nadhani shida ipo kwa Director. Wameweka matukio mengi sana yasio make sense. Kuna scene moja ya Tokyo ametoroshwa akakosa muelekeo baada ya kumpigia sana simu professor bila mafanikio. Akili yake ikamtuma arudi kule bank. Yani bank nzima imezungukwa na mapolisi lakini yeye akawapita na pikipiki yake mpaka ndani ya bank bila kuguswa hata na risasi moja. Hii scene ilikua ya kipuuzi sana. Hata ile "plan paris" ya kumtorosha raquel mahakamani ina makosa mengi sana ya kiufundi.

Ofcourse kila movie huwa na goofs, lakini inatakiwa hizo mistakes zisionekane kirahisi na mtazamaji kama zinavyoonekana kwenye money heist. Kwa sababu makosa ya kiuhalisia yakiwa mengi yanapelekea movie kuwa boring. Unaweza angalia series kama the blacklist mpaka season ya 7 usishtukie kosa hata moja. Na ndio kitu kinafanya Hollywood wazidi kuwa juu kwenye production!

Lakini upande wa character selection, money heist wamejitahidi sana. Binafsi, waigizaji bora kwangu kwenye money heist nawapa raquel (yule inspector) na Arturo (aliyekua manager wa bank). The way raquel ana.play emotional scene lazima akuchukue. Na huyu Arturo ameweza sana kufanya watazamaji tumchukie kwa kiherehere chake (ananikumbusha yule king Joffrey wa Game of Throne). Jamaa anajua kuigiza kiherehere mpaka unatamani umpige ngumi kila unapomuona. Hata Berlin ana style nzuri sana ya kuigiza smart, binafsi nadhani yeye ndio angependeza zaidi kuwa professor.

Sijajua kwa upande wako lakini binafsi huwa napendelea zaidi performance kuliko storyline. Yani mimi kuna movie huwa nabaki nazo miaka nenda rudi kwa sababu ya performance ya waigizaji iliyotukuka.

Kama ww ni mpenzi pia wa single movies hata za zamani jaribu kuangalia movie moja hivi inaitwa "the pianist" ya 2002 kuna mwamba humo ndani (jina lake halisi ni Adrien Brody) ameigiza haijapata kutokea. Alishinda mpaka oscar kwa performance yake!

Lakini kuna movie pia ambazo ni fikirishi kama "the hidden figures", 2016 ni nzuri, "beautiful mind", 2000 (hii nayo ina performance moja hivi imesimamia kucha). "Pursuit of Happiness", 2006 na "the banker", 2020

Kwa upande wa spain kuna jamaa mmoja hivi anaitwa Javier Bardem, huyu mwamba naye ni bingwa wa kuigiza jaribu kuangalia movie yake ya "Loving Pablo", 2017 utamkubali.

Kama hujawahi kuangalia movie yoyote kati ya hizo hapo juu, jaribu kuzitafuta..watu wameigiza vizuri sana humo ndani!
 
Jamaa wa Fort Meade walihusika kutoendelezwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…