Storyline yake sio mbaya. Nadhani shida ipo kwa Director. Wameweka matukio mengi sana yasio make sense. Kuna scene moja ya Tokyo ametoroshwa akakosa muelekeo baada ya kumpigia sana simu professor bila mafanikio. Akili yake ikamtuma arudi kule bank. Yani bank nzima imezungukwa na mapolisi lakini yeye akawapita na pikipiki yake mpaka ndani ya bank bila kuguswa hata na risasi moja. Hii scene ilikua ya kipuuzi sana. Hata ile "plan paris" ya kumtorosha raquel mahakamani ina makosa mengi sana ya kiufundi.
Mkuu Laskaboza, kwamba Money Heist ina scenes nyingi za hovyo nakubaliana na wewe!!
Ukijiuliza lile swali la msingi katika utengenezaji filamu kwamba "hivi hii scene ingekuwa ni kwenye real world, ningefanya kama alivyoona Mwandishi?" Ukijiuliza hilo swali, utakuta Money Heist ina scenes nyingi ambazo hazi-make sense in a real world.
Kinyume chake, hiyo scene uliyoitolea mfano, kajaribu kuiangalia tena na utaona ina-make sense! Unfortunately sikumbuki ilikuwa episode ipi lakini naikumbuka ile scene!
Mosi, Tokyo hakutokea eneo la tukio kama Tokyo basi alikuwa ameji-impersonate as a Police Officer in a police uniform huku kichwa chote kikiwa kimefunikwa na bike protective gear.
Na wakati anaingia eneo la tukio, team mzima ya mapolisi ilikuwa ndani ya hema lakini polisi mmoja aliyekuwa nje, akawa amem-suspect Tokyo lakini hakuwa na uhakika kwa sababu alikuwa kichwa chote kipo kwenye protective gear!
Afande alipoanza kum-suspect Tokyo, akajaribu kutaka kumsimamisha... Tokyo akaona isiwe taabu, akakanyaga mafuta! Baada ya kukanyaga mafuta, ndipo yule afande akapata uhakika kwamba "huyu ni intruder" lakini nae wala hakufahamu kwamba ni Tokyo kwa sababu wakati anapiga radio call, alisema "...another unauthorized vehicle is entering the perimiter" wakati ile ilikuwa ni "no-pass zone" for unathorized vehicles.
Na kama ujuavyo mambo ya kijeshi... you can't just shoot kwa kitu usichokifahamu bila order ya kufanya hivyo! Lucky for Tokyo, hadi Snipers wanapata "a shoot order" ilishakuwa kind of too late (though it's within seconds) coz' tayari Tokyo alikuwa close to gate!
Na mbali ya Sniper Team, pale chini kulikuwa na team nyingine wakisubiri order! A moment wanapewa order kwamba " a target is in your range" hapo hapo wakaanza ku-shoot toward a high speeding bike!
Lakini sekunde chache baadae, wakajikuta wanashambuliwa kutoka nyuma na Tokyo's Team ambao walikuwa wameshafungua gate na kuwafyatulia risasi jamaa kama namna ya ku-divert attention yao, na walifanikiwa kwa sababu wakalazimika kugeuka kutupiana risasi na wale waliokuwa ndani wakiwashambulia wao!!
Na ukiangalia hata yule Team Leader wakati anatoa order to shoot, nae wala hakuwa na uhakika kwamba ni Tokyo... it's just a military intuition kwamba atakuwa " a daughter's mother"!
So, kwangu ile scene naona kama ina hitilafu, basi itilafu zake ni za kifilamu zaidi kuliko illogical errors!