Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

wabunge wa viti maalum maamuzi yatatolewa baada ya uchaguzi mkuu, wote waliambiwa waende majimboni wakahamasishe ili kuzoa viti vingi. kwa hiyo mchango wa mgombea viti maalumu ndiyo utakao judge nani awe na nani asiwe, hiyo ni katika kutekeleza falsafa ya siyefanya kazi na asile, huenda Nakaaya ameshindwa kufanya kazi hiyo na ameona kuwa hatapata viti maalum. kwa hisani ya watu wa marekani.
 
hivi huyu 'binti mdogo bado' ana umri gani?
 

Asante Mkuu, hii hapa kutoka YOUTUBE.
[video]http://www.weloveafricans.com/video_player/videoid/14284/nakaaya-feat-m1---mr-politician[/video]
 
Last edited by a moderator:
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.

kalogwa???????????????????????????????????????????????????????????????????????????/
 

I hear you mkuu, ile lugha ilikuwa kali na ingeleta atention za mods bila sababu
 

Akikua ataacha, mi namshangaa pamoja na kuwa ni haki yake kuchagua ila vipi juzi tuu alikua mstari wa mbele kuwaponda viongozi wa siasa walioko madarakani kwa wimbo wake na leo ghafla anajiunga nao? well kama nilivyosema akikua ataacha, kwenye blog yake nilisoma jinsi alivyokua na mapambano na maisha yake kwa ujumla na mahusiano yake ila najaribu kumwelewa huyu mwananchi mwenzangu na kumwachia nafasi ya kujisoma na kujitambua, All the best with the turn you took and we will accept u if u decide to come back as u went. U said it all before in your blog so we need not ask u nothing now what with the confusion. Siasa sio Bongo fleva yahitaji moyo na uzalendo.
 

Kuna kazi kweli mkuu ... redio, tv, promoters zote wako kwenye kampeni.
Inatia huruma akikumbushwa haya yote lakini ndio hivyo tena, dawa imetoka kwenye chupa ya mswaki.
 
Hii kuhama chama inaweza hata kumnyang'anya washabiki wa muziki wake. Labda awe ameamua kufanya siasa kazi na ahadi ya uDC

Inaweza kumsaidia kutembea na JK kwenye kampeni zake mikoa ilosalia kama Flora Mbasha, Marlow na TOT, atapata mshiko wa kutosha kwa night zilizobakia.
 
[video]http://www.weloveafricans.com/video_player/videoid/14284/nakaaya-feat-m1---mr-politician[/video]


Anaimba very logical song lakini hamaanishi kumbe ni njaaa jamani! lakini si cha ajabu, maana CCM ndo wenyewe kwa zile milion 60. Lazima dau limepanda saaana. Ila watanzania hatudanganyiki! Natamani sana nione watu kama hawa baadae wawepo wakati Tanzania ikipiga hatua kubwa kiuchumi chini ya serikali tofauti na ccm.
 
MSANII wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari ambaye mapema mwaka huu alijiunga na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amejiondoa katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nakaaya jana alijiengua Chadema na kujiunga na CCM muda mfupi, kabla ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Rais Jakaya Kikwete hajahutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, ndiye aliyeweka wazi kuhamia kwa Nakaaya katika chama hicho wakati alipokuwa akitangaza utaratibu wa mkutano huo kabla
ya Kikwete kuhutubia.

"Mheshimiwa mgombea wa urais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, nitamkaribisha Mwenyekiti
wa Mkoa akukaribishe ili kabla ya kuhutubia, uje umkabidhi kadi mmoja wa vijana wetu maarufu, msanii Nakaaya Sumari ambaye alikuwa amepotea na sasa ameamua
kurejea katika chama chetu," alisema Chatanda.

Kwa upande wake, Nakaaya aliyejipatia umaarufu kwa kibao chake cha ‘Mr Politician', alisema amerejea CCM na kushukuru kwa kupokelewa tena.

Kuonesha umahiri wake katika sanaa, msanii huyo aliimba mashairi machache ya kuisifu
CCM, akitumia falsafa ya mwaka huu ya Rais Kikwete ya ‘Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi.' Baada ya kumaliza hotuba yake, Rais Kikwete alimpongeza Nakaaya kwa kujiunga na CCM na kumkaribisha katika chama hicho, na kueleza kuwa atajiunga na kundi la wasanii wenzake kuhamasisha wananchi waichague CCM.

NB: Bila shaka kaahidiwa kitu na JK, sijui tunaenda wapi?

Source: HabariLEO
 
Hana Jipya alikuwa natafuta umaarufu wa kukutana na JK na leo hii wapo Hoteli Moja sasa Huko anaimba wimbo au........................Anapewa nini??? Taarifa baadaye
 
Dau lake kuhama ilikuwa kiasi gani? Nadhani kuna wafuatiliaji tayari wanalijua hili..
Nimesikia msimu huu wameambiwa nyota yao #6..hivyo inawezakana dau likawa mil 6 au 60..sijui! hebu mtujuze
 
Dau lake kuhama ilikuwa kiasi gani? Nadhani kuna wafuatiliaji tayari wanalijua hili..
Nimesikia msimu huu wameambiwa nyota yao #6..hivyo inawezakana dau likawa mil 6 au 60..sijui! hebu mtujuze

kuna mtu kaniambia kuwa katanguliziwa milioni 30 na atapewa milioni 30 baada ya kampeni. Sitaki kuamini hili ila hata kama ni kweli, Nakaaya amefanya maamuzi yake na mimi binafsi namtakia kila la heri huko ccm
 
Nakaaya amefanya uamuzi ambao ni mzuri kwake. Ndiyo uzuri wa demokrasia. Vyovyote vile ilivyokuwa pressure ilikuwa kubwa sana kwake. Somebody had to give.
 
Wanaojiunga na CCM kipindi hiki, poleni sana, CCM iko mwishoni sana kuanguka hata kama hamna vyama vya upinzani, ni lazima CCM kuanguka, muda unaruhusu CCM kuanguka. CCM haina muda mrefu wa kuanguka.

Dalili ya CCM kuanguka ni pamoja kubeba watu kwenye magari tayari kupelekwa kwenye kampeni kama magunia, kukakataa kushiriki kwenye midahalo, kukataa kuumlizwa maswali wakati wa kampeni, rushwa kuongezeka sana.

Narudia kusema CCM imebakiza muda mfupi sana. Tusubiri, mimi ninaipigania nchi yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…