Hello JF salaam!
Nimekuja kwenu nipate mawili matatu huenda nikawa na tatizo. Nilikuwa na mwili wa wastani siyo bonge sana wala mwembamba sana.Kimbembe kimeanza kama miaka miwili nyuma naona mwili wangu unazidi kupromoka tu siku hadi siku japo chakula napata na pia naupa mwili muda mwingi wa kupumzika hasa nyakati za usiku.
Mwanzoni nilihisi labda ni kwa sababu ya misongo ya mawazo ndipo nikaamua kujijengea desturi ya kuepuka mambo yanayoweza kunisababishia hizo stress kwa kujumuika na marafiki zangu wa karibu, kufanya mazoezi ya mwili na viungo na pia kufanya mambo ambayo yanaupa moyo wangu furaha(hobbies). Nimefanya hivyo yapata miezi saba mpaka sasa lakini hola tu sioni changes na mwili ndo hivyo unazidi kuyoyoma tu.
Infact, sipendi kuwa bonge nataka niendelee kumaintain mwili niliokuwa nao lakini kwa dalili hizi za karibia kila ninaekutana nae ananiuliza mbona umepungua hivyo nahisi ni dhahiri shairi nimepunguwa kwa kiasi kikubwa. Hii hali kwakweli inanitisha imefikia mahala umenifanya nianze kuonekana mdogo hata kwa niliowazidi umri hata pale napoongozana na dogo langu anaonekana mkubwa mi mdogo japo siyo vibaya lakini kwa upande wangu inanitafakarisha sana ukizingatia kwamba sikuwa hivyo hapo kabla.
Kiafya niko vizuri kabisa na huwa nina desturi ya kuchukua vipimo kila baada ya muda fulani na mpaka naandika uzi huu nilianza kwenda kucheki afya kwanza kabla ya kuja kwenu kuwaomba mawili matatu. By the way, nisiwe more talkative kiasi cha kuwakera naomba kusikia toka kwenu ni kwa namna gani naweza kurudisha mwili wangu(mwili wa wastani) kutoka kwenye huu nilio nao kwa sasa?? Na pengine ni kipi hasa kinaweza kuwa kimechangia mwili wangu kupungua kama nilivyoeleza huko juu??
Karibuni niko tayari kupokea ushauri wenu na kufanyia kazi.